Ni kweli ndani ya miaka 50 yapo yaliyofanyika lakini makosa ni memgi sana. Tulitakiwa tuwe tumekwenda mbele zaidi ya hapa tulipo sasa.
ELIMU yetu iko chini ukilinganisha na ile ya mkoloni waliyosoma kina Nyerere. Iko chini kulinganisha hata na jirani zetu Kenya, Uganda.
UCHUMI wetu upo chini sana kuliko jirani zetu, kuliko hata Rwanda iliyokumbwa na machafuko kwa muda mrefu.
VIWANDA aliyopora Nyerere kutoka kwa wawekezaji vimekufa vyote kwa uzembe na ujinga wetu wala si kwa sababu ya madiliko kwenye dunia dhidi yetu, kwani Kenya hawakupitiwa na mabadilko hayo?
Nyerere hakuacha viwanda vinafanya kazi, vilishakufa isipokuwa alivipa ruzuku ili vionekane vinafanya kazi. Vilikuwa mzigo kwa taifa (havikuwa-productive)
KUMILIKI SIMU Bibi Nundu siyo maendeleo, ni matokea ya technologia mpya ambapo sisi tumepokea kama tulivopokea UKIMWI tutake tusitake. Waliogundua simu ndiyo wanajivunia maendeleo sababu wanapiga mpunga wa nguvu.
VITA ya Uganda ilikuwa ya kujitakia wenyewe kwa uswahiba wa Nyerere na Obote, matokeo yake ikatugharimu maisha na uchumi.
Kwa ufupi, jinsi nchi hii ilivyo na rasilimali nyingi MADINI, MISITU, MAZIWA, MITO, BAHARI, GESI,MBUGA ZA WANYAMA, MLIMA MREFU AFRIKA n.k katika miaka 54 ya uhuru tulistahili tuwe mbali sana kimaendeleo kuliko nchi nyingi. Kuna baadhi ya nchi zimeendelea sana kutokana na rasilimali zetu na ujinga wetu
Napingana kabisa na kauli hii eti: CCM imeweza kuiishi kwa rushwa kutokuwa kigezo cha kupata madaraka Nadhani huyu Polepole alikuwa anaishi nje ya Tanzania, namshauri ajaribu kugombea hata ujumbe tu wa serikali ya mtaa kupitia CCM aone mziki wake.