Leo channel Ten kipindi kinahusu kilichofanyika baada ya miaka 50 na mgeni mualikwa ni Humphey Polepole
Polepole: Ni miaka 51, inasemekana hakuna kilichofanyika na kusema hawa sasa wameshindwa katika miaka 50. Kukubali mafanikio ambayo umeyafikia ni ustaarabu pia changamoto.
Sifa moja ya binadamu ni kujikubali, Tangu tunaanza sidhani kama mwaka 2000 watu wengi tulikuwa tunamiliki kama sasa, leo hadi bibi yangu Nundu anamiliki simu. Kutoka Tabora hadi Iringa ilikua lazima ufike Dodoma kwa Treni ndio uanze kuunganishe mabasi kwa muda mrefu.
Nakumbuka mama akiandaa maandazi ya kula njian kwa sababu tulikuwa tunalala safari ya Tabora, leo tunasema miaka 50 hakuna kilichofanyika! Tujitendee haki kama taifa.
Ukiangalia hali ilivyokuwa zamani na ilivyo leo kuna tofauti kubwa, Mwalimu Nyerere ameliongoza taifa hili nusu ya miaka baada ya kupata uhuru ambapo maneno yake yanatumika kwenye kampeni za UKAWA na CCM.
Toka mwaka 64 inazaliwa Tanzania na tukawa na katiba ya mpito mpaka 67 linazaliwa Azimio la Arusha mpaka 77 na tunaingia vita vya Uganda baada ya hapo. Vita ambayo iliturudisha nyuma kabisa. Vita za ukombozi pia zilitugharimu kwa sababu ilibidi tuvunje uhusiano na Uingereza. Tukajenga reli ya Tazara ikiwa ndio reli ya kwanza ya standard Gauge.
Mzee Mwinyi anaingia kuja kureebisha uchumi, uchumi wa soko huria kila mtu ashiriki kwenye uzalishaji, Mkapa akajenga uchumi imara na kazi ya Jakaya ikaja kuimarisha na kutengeneza sheria kuhakikisha uchumi wtu unaratibiwa na sheria.
Maendeleo ni hatua, tulikuwa na mainjia wawili na leo ni zaidi ya 10,000. Tunazungumza kilometa 1300 za lami leo tunazungumzia 20,000. Viwanda vitakuja kujibu tatizo la ajira, ndio viwanda anazungumza Magufuli, kama ulichukua kiwanda na ukashindwa utarudisha kiweze kuendelezwa.
Maswali na maoni
- Kaka amenikata kauli, katika miaka 50 najua kuna mazuri yamefanyika lakin pia kuna mabaya. Kwa asilimia kubwa hakuna kilichofanyika lakini sio hakuna kilichofanyika. Viwanda vilikuwepo, kwa nini vinakufa, matatizo ni mengi kuliko mafanikio.
- Asante kwa kipindi na mada hii nzito, nina respect kubwa kwa Polepole lakini sasa anaenda kushoto, nashangaa anasema tusijilinganishe. Huwezi kusema sekondari tumejenga aafu ndio tutrain walimu, huwezi kujenga hospitali wakati huna wauguzi. Tulikuwa na viwanda vimekufa, barabara zilikuwepo, kilichofanyika ni kuweka lami.
- Nikushukuru, Polepole kidogo anatuchanganya, angekuja kwetu sisi wananchi kwenye uhalisia uone watu wanavyopata shida. Tulinganisha maendeleo kulingana na rasilimali tulizonazo na miaka tuliyonayo.
- Niungane na Polepole, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, wanasiasa wajaribu kuwa wakweli. Kigoma leo kijijini sana naangalia channel ten na sio kwa kutumia solar bali umeme kwa huduma ya REA. Watanzania tujaribu kuwa wakweli.
- Ukweli ni kwamba tunarudi nyuma kama viwanda vinakufa, ukifika hapa Tanga viwanda vyote utafikiri magofu.
- Shida ya Polepole anaegemea upande mmoja, Nyerere viwanda aliacha vinafanya kazi, alivyokuja Mkapa alileta ubinafsishaji, Je! Ulisaidia! Miaka 50 Dar es Salaam hamna maji!
- Watanzania tunapaswa kuacha ushabiki wa vyama na kuangalia zaidi mtu anaegombea ni wa namna gani. Kusema miaka 50 hamna kilichofanyika wakati matibabu yameongozeka, mashule yameongezeka, miondombinu imeongezeka. Watu waangalia mtu gani anastahili kuongoza taifa letu, UKAWA hata wakipata madaraka kuna mambo hawataweza kufanya kwa asilimia 100.
Polepole: Kuna hii dhana ya mabadiliko, CCM imeweza kuiishi kwa rushwa kutokuwa kigezo cha kupata madaraka, matajiri pia wameshindwa kuhodhi utawala. Amekuja kuibuka mtu kwa vigezo, mabadiliko ya mwalimu Nyerere aliyoysema mwaka 1995 yamedhihirika miaka 20 baadae.
Viwanda vyetu vilikufa si kwa sababu ya uzembe wetu na ubadhilifu pekee bali madiliko kwenye dunia dhidi yetu, kila kitu ni hatua na wananchi ni vizuri kuzifahamu. Ni bora kuwauliza kwani wewe ulivyokuwa madarakani ulifanya nini?
Polepole: Video ya Lowassa, kama mimi nahusika na video! Juma Mwapachu amesema Lowassa ameteleza, mimi nasema ameanguka chini.
Hapana mimi nilitaka kuwaambia watanzania kuwa mimi ni Mlutheri lakini haiwezekani kumchagua mtu kutokana na dini yake, vipi Waislamu na madhehebu yao. Mimi sihusiki na hio video na hatufanyi siasa makanisani.
Last edited by a moderator: