Mada moto Channel 10: Edward Lowassa ndani ya UKAWA. Polepole amfananisha na malaya...

Polepole is genius aisee...hata wanaopiga simu wanamchana Msigwa kuwa ni mchungaji tapeli. Msigwa kapaniki
 
Pole pole ana hoja,anajibu kwa hasira kama mbogo na hoja anazojenga ni dhaifu mno.

Hii hoja anayojenga kwamba kiongozi mkuu wa nchi asiwe na tuhuma,na tusitegemee mahakama kwa hili.

Nashindwa kuelewe kama mtu akituhumiwa na watu,awe disqualified kwenye uongozi.Navyojua mimi,mahakama ndo chombo pekee kinachotakiwa kusafisha tuhuma kwa mujibu wa sheria.

aende zake kule, mnafiki kweli jamaa, mwaka huu hatudanganyiki tutakuwa kama WAKENYA waliamua kuwapa kura uhuru na ruto pamoja na kujazwa tuhuma kibao dhidi yao
 
Msigwa: Hatuna kosa la kumsafisha EL.Mwembeysnga tulisema watu 11, kwa nini hawasemwi. Lowasa hajakuwepo serikalini miaka8 lakini ufisadi umezidi. Hatuna muda wala kosa la kumsafisha. Tunakwenda kushinda
 
Hivi itakuwaje kama itatokea kila mjumbe wa tume akaja mbele ya umma na kusema maoni yaliyotolewa na viongozi wa nchi hii wakati wa maoni ya katiba mpya, HP asijikweze na ujumbe wake wa TUME na kujiona yeye ndo mwenye maamuzi ya mwisho wa Watanzania!
 
Lowassa achafuliwe, aogeshwe, ila tutampa kura za kutosha kabisa na wananchi tumedhamiria hivyo kabisa, ccm inatuhuma ngapi? Uchafu mtupu,

pole pole na vibaraka wake wajue watanzania wana kitu kichwani hawa yumbishwi na majungu,umbea,na fitna za watu kwaajili ya maslahi yao, tukutane oct 25
 
Msigwa: Hatuna kosa la kumsafisha EL.Mwembeysnga tulisema watu 11, kwa nini hawasemwi. Lowasa hajakuwepo serikalini miaka8 lakini ufisadi umezidi. Hatuna muda wala kosa la kumsafisha. Tunakwenda kushinda

nimei penda ihi, tupo 1
 
Back
Top Bottom