Safi sana mkuu MANI, ni vizuri atumie njia hii kama sehemu ya troubleshooting.Kabla ya kuituhumu gear box ni vemaMkuu hiyo gari haikuwa na guarantee? Tafuta fundi wa uhakika au kama huhitaji hiyo 4 wheel unaweza kutoa shaft za mbele kuliko kufungua gear box inaweza ikazalisha zaidi ya hayo.
HAKI ZA DEREVA ANAPOKAMATWA NA TRAFFIC
- Trafiki hana idhini ya kukulazimisha kumkabidhi leseni yako
-Akikukuta na kosa na kukuandikia notification na ukalipa ni lazima akupe risiti ya serikali
-Hana haki ya kukuulizia kuhusu road licence hiyo ni kazi ya TRA kwakuwa siku utakapoenda kulipa utalipia na faini
-kama huna leseni una haki kisheria kuipeleka kituoni ndani ya Massa 72 ya kazi tangu ulipotakiwa kufanya hivyo
-Akikusimamisha una haki ya kusimama sehemu ile ambayo utaona ni salama na si lazima usimame anapotaka yeye
- Sio kila kosa ni la kuadhibiwa, mengine ya kuonywa au kuelimishwa
Hapo kwenye issue za road licence matrafic kumbe wanatuonea eehh. Kuna trafic alinilamba buku tano yangu kiulani.
Na vp kuhusu insurance nayo wana haki ya kukulipisha faini km itakuwa imekwisha.?!
Kwa nini taa za Dash board huwa zinga rangi nyekundu, orange, green na blue?
Hivi kwa nini House Girl kuachiwa mtoto sio ishu lakini huwezi kusikia House girl kaachiwa gari?
Uzi mzuri sana, nimesoma comment zote,
Sasa mkuu nipe ushauri na uzoefu wako, nataka kuchukua runx, ila itatumika zaid barabara ya vumbi, je inafaa? Vp uimara wake? Vifaa vinapatikana? Je wewe ni fundi wa magari?
View attachment 226222
Kazi ya N hapo ni nini? Suzuki escudo 2007 model
Basic outer body partsView attachment 225630
Kuna ile mada ina ufafanuzi kuhusu tires, traction, thread ratio nk. Mambo ya upepo nk. Kuna mtu anazo?
Hapana mimi sio fundi, runx si ndio kizazi cha ist, Allex, duet nk? Ni gari ambazo hazitaki shida wala mikikimikiki, kwa ushauri nunua gari yeyote kizazi cha corolla100, 110 au hata GX 100 kavu! GX vvti itakutesa
Mi sina lakini naweza sema neno hapo! Kwa usalama zaidi tairi haipaswi kutembea zaidi ya km elfu 40 ikizidi sana ni 50, traction inasaidia velosity ya speed na uchakavu wa tairi hivyo ni vema ukafunga kama mshale unavyoelekeza, tread ratio nayo ni muhimu na ukubwa pia, unapofunga tairi oversize ulaji wa mafuta huongezeka au kasi ya gari hupungua
Upepo pia ni muhimu kwa stability ya gari barabarani na uchakavu was tairi pia mara nyingi inashauriwa upepo wa tairi za mbele usizidi 30 na was tairi za nyuma usizidi 35
Ndugu Mimi Nina Honda Crv 2002 upepo nimeweka tairi za mbele 40 na tairi za nyuma 40, je kwa usalama inafaa?
Mmmh hapana weka hiyo ratio niliyosema hapo juu kumbuka gari inapokuwa kwenye mwendo msukumo huongezeka kwenye tairi hivyo waweza sababisha bust
Sawa ndugu! Sababu nilikwenda pale wanapojaza upepo nikawauliza normal upepo kwa matairi inatakiwa ngapi? Akasema 40 kwa kila tairi.
Mmh hapana hiyo sio kubwa na hata kashata zake haziwezi kuhimili huo mzigo labda kama hiyo gari isikae juani wala kutembea barabarani
Kwa macho huwezi kuona na kama tairi ni mpya lakini kama tairi zimeshaanza kuchoka si salama kabisa! Upepo standard ni front wheels 30, rear wheels 35
Mmmh hapana weka hiyo ratio niliyosema hapo juu kumbuka gari inapokuwa kwenye mwendo msukumo huongezeka kwenye tairi hivyo waweza sababisha bust