Mada maalum: Karibu tujadili masuala yote kulekea vyuo vikuu 2016/17

we jamaa ww bn so unataka chuo kiwape hostel bure imekua shule ya sekondari hiyo kuna tofaut kubwa kati ya bweni na hosteli kwa msaada tu sua jipange hata kama una jina bodi ww nenda umejiwekea akiba usije enda bila kitu ukitegemea huruma ya chuo welcome solomon mahlangu campus welcome main campus
 
Nipo kwenye harakati za kulipa karo na malipo mengine kwa shemeji yangu aliyechaguliwa kusoma degree chuo kikuu cha ushirika Moshi.
Chuo hiki kimeunda utaratibu mgumu kiasi wa malipo. Malipo yamegawanywa kwa mafungu na kila fungu lina akaunti tofauti katika benki tofauti. Mfano:

Tuition fees, faculty depreciation na registration fees vyote viko fungu moja na vinalipiwa crdb benki.
Medical capitation, tcu quality assurance viko akaunti moja na kulipiwa crdb akaunti tofauti na ya fees.
Kiingilio cha chama cha wanachuo kina akaunti yake exim bank.

Kwa nini vyote havilipiwi kwenye akaunti moja crdb? Hii kugawagawa imenisumbua na kutumia muda wangu mwingi sana.

Hiyo kugawana wasigawane kwenye akaunti ila wagawane chuoni baada ya malipo. Au hiyo hawawezi?Yaani nilitaka hivi: Malipo yote yafanywe kwenye akaunti moja siyo kugawagawa.

Hivi je, na vyuo vingine ni hivyohivyo?
 
Simaanishi wapewe hostel bure, maana yangu ni kanuni ya ubinadamu kutumika! Kwa mfano chuo kinaweza kuwahifadhi kwa muda wa wiki moja wakati wanasubiria matokeo ya bodi ya mikopo. Baada ya wiki moja bila shaka bodi itakuwa imeweka mambo wazi. Baada ya hapo MTU akijikuta hana mkopo na kujilipia hawezi basi anaamua kuahirisha chuo na kurudi nyumbani. Kuliko kumwacha mwanafunzi anahangaika na facility IPO iliyogharimiwa kwa kodi za watanzania! Si ubinadamu MTU akakutembelea halafu ukamwacha kulala nje wakati nafasi ya muda ya kumhifadhi IPO!
 
Back
Top Bottom