Muongozo na ushauri kwa wanafunzi udahili vyuo vikuu 2017/18

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,179
2,940
Habari wakuu,

Kuna wadogo zetu walimaliza kidato cha sita na matokeo yao yanatarajia kutoka karibuni, kwa sasa wanakaribia kwenye mchakato wa kujaza vyuo na uchaguzi wa shahada watazochukua. Ni ngwe muhimu sana kwenye maisha yao, kwa sababu ndio itayochagua awe nani baadae kitaaluma.

Shahada gani na chuo gani anaweza kwenda ni changamoto nyingine hasa kipindi hiki ambacho ushindani umekuwa mkubwa hadi kwa kozi za sayansi kinyume sana na kipindi cha nyuma pia kurudisha mpango wa zamani kuomba chuoni badala mfumo wa TCU inaweza kushikilia nafasi nyingi sana na watu wenye ufaulu mzuri na kuwaacha wengine kutaharuki na kufanya makosa kwa kuchagua ilimradi kwenda chuo kwani kuna changamoto kubwa ya watu kwenda kusoma vitu wasivyotarajia dakika za mwisho na wengine kuahirisha kabisa masomo mpaka mwaka unaofata.

Hapa jukwaani kuna wanavyuo wengi ambao kwa sasa wanasoma vyuo na shahada ambazo wengine wangependa kwenda, kuna wahitimu wa hivyo vyuo na wanajua mazingira ya vyuo husika pia changamoto gani wamezipata kwenye hivyo vyuo na kuelekea kwenye ajira kulingana na shahada walizosoma, mwisho wapo wanaohusika wa hii michakato ikiwemo vyuoni au kwenye baadhi ya mamlaka za usimamizi wa elimu ya vyuo vikuu kama TCU au bodi ya mikopo.

Kwa pamoja naamini tunaweza kuwapa mwanga hawa wadogo zetu wapunguze idadi ya makosa yanayotokana na kutokuwa na ufahamu. Kwa heshima ningependa kuwaita @LORDVILLE LISANDIME tzhumoally CDG Marco Polo mchepukomatope Chungu cha bibi na wengine wote katika kufikisha lengo la mada hii.

Karibuni!

Kwa vigezo, bofya=> HAPA
 
Kwani hao form six nao ni member wa jf?

Sent from my Infinix NOTE 3 using JamiiForums mobile app
 
Members wa humu kwenye inshu za muhimu huwa response ndogo sana ila ingekuwa mambo ya kudiss wavulana wa dar au kugegeda hapa kungekuwa na comments sana

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
Nenda kujadili mada moja kwa moja,acha kusemea mioyo ya wengine.
 
Wahitimu wengi wa kidato cha sita najua hawamo humu. Wengi wanapatikana Instagram.

Mdogo wangu kahitimu diploma ya sheria kutoka chuo cha mahakama Lushoto, sijui ni chuo kizuri cha kusomea digrii.
 
Ushauri wangu kwa waliosoma arts ni kwanza uoga ndio umasikini wenyewe, kwa hyo katika kuchagua kozi au chuo ni vema kutanguliza matakwa ya ndoto zao kuliko matakwa ya woga na ushauri wenye kujielekeza katika woga pia

chagua kozi ambayo ni ndoto yako , usiogope habari za mkopo wala ajira maana kwa mfumo wa sasa hamna mtu yuko safe wala garanteed kupata mkopo wala ajira kwa chochote anachokisomea au alichokisomea ni suala la kujiongeza tu na bahati binafsi.

OVA
 
Wahitimu wengi wa kidato cha sita najua hawamo humu. Wengi wanapatikana Instagram.

Mdogo wangu kahitimu diploma ya sheria kutoka chuo cha mahakama Lushoto, sijui ni chuo kizuri cha kusomea digrii.
sheria bongo kwa degree ni
Udsm
Saut
Mzumbe
Tumaini

Ova
 
Habari wakuu,

Kuna wadogo zetu walimaliza kidato cha sita na matokeo yao yanatarajia kutoka karibuni, kwa sasa wanakaribia kwenye mchakato wa kujaza vyuo na uchaguzi wa shahada watazochukua. Ni ngwe muhimu sana kwenye maisha yao, kwa sababu ndio itayochagua awe nani baadae kitaaluma.

Shahada gani na chuo gani anaweza kwenda ni changamoto nyingine hasa kipindi hiki ambacho ushindani umekuwa mkubwa hadi kwa kozi za sayansi kinyume sana na kipindi cha nyuma pia kurudisha mpango wa zamani kuomba chuoni badala mfumo wa TCU inaweza kushikilia nafasi nyingi sana na watu wenye ufaulu mzuri na kuwaacha wengine kutaharuki na kufanya makosa kwa kuchagua ilimradi kwenda chuo kwani kuna changamoto kubwa ya watu kwenda kusoma vitu wasivyotarajia dakika za mwisho na wengine kuahirisha kabisa masomo mpaka mwaka unaofata.

Hapa jukwaani kuna wanavyuo wengi ambao kwa sasa wanasoma vyuo na shahada ambazo wengine wangependa kwenda, kuna wahitimu wa hivyo vyuo na wanajua mazingira ya vyuo husika pia changamoto gani wamezipata kwenye hivyo vyuo na kuelekea kwenye ajira kulingana na shahada walizosoma, mwisho wapo wanaohusika wa hii michakato ikiwemo vyuoni au kwenye baadhi ya mamlaka za usimamizi wa elimu ya vyuo vikuu kama TCU au bodi ya mikopo.

Kwa pamoja naamini tunaweza kuwapa mwanga hawa wadogo zetu wapunguze idadi ya makosa yanayotokana na kutokuwa na ufahamu. Kwa heshima ningependa kuwaita @LORDVILLE LISANDIME tzhumoally CDG Marco Polo mchepukomatope Chungu cha bibi na wengine wote katika kufikisha lengo la mada hii.

Karibuni!

Kwa vigezo, bofya=> HAPA
Mkuu subiri kwanza matokeo ya toke ndo utakaoamua mustakabali wa maisha yao,kwamba wakasomee kitu gani na chuo gani kutokana na ufaulu wao
 
Jamani hivi huu mfumo wa kuaapply chuo utakuwa online au mwanafunzi anaenda mojakwamoja chuoni na nyaraka zake naomba kujua kwa wanaofahamu

Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom