Mada kwa waliowahi kuanguka mbele ya watu(sio kwa maradhi) ulijisikiaje na ulichukua maamuzi gani baada ya tukio?

Niliwahi kuanguka nikiwa shule natoka jikoni nikiwa nimeshikilia sahani ya wali uso ulijaa vumbi lakini cha ajabu wali haukumwagika😅😆.. Sikupata aibu yoyote .
Hahahaaa mwalimu alianguka assemble alikua anamkimbiza jamaa mmoja mtukutu hatari
 
Mi nilianguka kutoka kwenye air tanzania nikatua sokoni watu wakajua yesu karudi wakaanza kutimua mbio
 
Wakat Nasoma olevel kuna kipindi tulikua tunasafisha mbwalo(Hall) kwa ajili ya Mahafali

Wanaume tukaambiwa tukalete Maji tulikua tunatumia madumu ya njano yamekatwa Upande

Sasa Kuna sehemu kuna mtalo (mdogo tuu unaweza kuluka) na kulikua na vijidaraja cha kuvukia

Nikaona kupanga Msululu wa kuvuka Pale kwenye moja ya kidaraja jau

Si nikaluka Na Dumu Langu lenye maji bwana, nikashangaa niko Chini na nimelowa Sababu yamekatwa Upande watu wote Wananishangaa Mimi
Nakumbuka pemben ya mtalo kulikua Kuna Madarasa nje wamejazana wanawake kibao wakanicheka

Nikajinyanyua huku nachechemea mdogo mdogo Siku geuka nyuma nikazunguka mpaka darasan Kwang nikatulia
 
Mvua ilinyesha nilikuwa natoka dukani, ile nafika getini chali....kumbe kulikuwa na Mama yeyoo kaniona akapiga yowe Watu ndio ikabidi waangalie ni nini..nilisikia aibu lakini nilimlaumu sana yule Mama yeyoo.
 
nilipewa baiskel ambayo haina breki kutoka kwa rafiki yangu kwa lengo la kuibariki kwa kupiga round mbili tatu na mwenyewe hakuniambia kama hakuna breki.

niliendesha kuushuka mteremko,aiseee nilipokuja kugundua chombo haina breki ndivyo na yenyewe ilivyozidi kukimbia zaidi.

kwa wenyeji wa ubungo nilipofika usawa wa kanisa la gwajima kutokea rombo/kibo nilikuta wafanya biashara wametandaza bidhaa zao chini enzi hizoooo za JK kama ilivyo kariakoo.

baada ya kuwakwepa woooote ki JAMES BOND kulaleki niliparamia kwenye banda la muuza miwa nadhani yule mwana hata nisahamu kwa jinsi nilivyo-m-surprise.

kilichotokea baiskeli ilibaki ndani mimi nikatokezea upande wa pili wa banda kutokana na speed kali nikawa nimedondoka pale.

siku hiyo nilijaza watu sitasahau kwa aibu niliyoipata kwani badala ya kuwa baraka ya baiskeli ikawa balaa la baiskel

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pole 😄 😄 😄
 
Nimecheka Sana
 
Daaaaah! Me niliangukaga stand ya mabasi tena nilitumbukia mtaroni,ebhanaeeeh,hiyo aibu niliyohisi (kama natak kufa kabisa😄) uzur mtaro ulikuw mkavu (hauna maji)sasa kuna wazee wa kahawa wapo pembeni hapo wanavyotoa pole huku wacheka ndo kabisaa wakaniharibu kisaikolojia😂😂😂😂.tangu hapo nikawachukulia wazee wanaokaa vijiwe vya kahawa sometimes hawana busara kabisa even if wamenipa pole zao za kiwaru(kinafki)😄😄😄😄tangu hilo tukio litokee nimejifunz kuwa makini kweli wakat wa kutembea hasa public fckn areas...😁😁🚶🏿🚶🏿🚶🏿
 
Kuna demu mmoja tukiwa shule alidondoka tukawa tunacheka akawa anaona aibu kunyanyuka. Ikabidi tukamnyanyue, eti anajifunika uso tusimuone.
😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom