Yanga mwendo umeumaliza ila tuwafundishe wapambanaji wetu waache mentality ya unyonge

Smt016

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
2,308
3,034
Awali ya yote natoa pongezi zangu kwa uongozi wa Yanga, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki kwa kuendeleza ushirikiano kwa kuhahakikisha timu ya Yanga inafanya vizuri.

Kwenye mechi za robo fainali Gamondi kaonesha kuwa mpira ni mbinu na ufundi haijalishi umewakosa wakina nani.

Naomba nirudi kwenye mada, wengi nimeona wanalalamika Yanga kunyimwa goli kwa angle zinazofanana ila mimi naomba niwe tofauti kidogo japo kwenye hili.

1) nimeona watu wanalalamikia VAR ila mimi binafsi sijaona tatizo la VAR bali nimeona tatizo kwa mwamuzi wa kati.

Baada ya lile shuti kupigwa na mchezaji wa Mamelodi kuondoa mpira kwenye hatari, watu waliopo kwenye chumba cha VAR ndio waliosababisha mpira usimame kwa kumuamrisha mwamuzi wa kati kuwa inawezekana ni goli.

Kwenye hili tukio, kama watu wa VAR wangekuwa wapo upande wa Mamelodi usingeona wakishughulika na kucheck tukio ambalo sio favorite kwa mwenyeji lakini watu wa VAR walithubutu kulichunguza tukio ambalo ni hatari zaidi kwa mwenyeji.

Kwasababu ni mawasiliano na wanatoa mawasiliano kule ndani hawana nguvu ya kuingia uwanjani kutoa maamuzi na pia hatuwezi kuelewa anachosema ni kipi, inawezekana pia wakampa taarifa mwamuzi wa kati kuwa ni goli lakini mwamuzi pekee akaamua kukataa.

2) Kulikuwa na kitu kidogo sana cha kuunganisha ili Yanga icheze nusu fainali lakini hiyo kitu imeshindwa kutumika ipasavyo. Kitu chenyewe ni kujitambua na kujiona Yanga pia ni timu kubwa. Wachezaji walikuwa katika unyonge mno yaani walijiona wao wanastahili haya kwasababu ni timu ndogo na pia waliridhika kwa walipofikia hivyo waliona tumepambana ila sio bahati yetu kufuzu. Baada ya mwamuzi wa kati kukataa goli, wachezaji wa Yanga walipaswa ku react kwa kumshawishi refa aende akaangalie kwenye screen ili akajiridhishe, tunaona mara nyingi tu wachezaji hulazimisha mwamuzi aende kwenye screen ndipo walizike na maamuzi. Laiti kama ingefanyika hilo na refa akaenda basi leo tusingeangaika na mabarua kwasababu nina uhakika lazima angeweka mpira kati maana angejisikia aibu maana lazima angefanya preview kwa angle tofauti tofauti.

Pale ingekuwa timu yeyote ya uarabuni au hata Tp Mazembe, wasingekubali mpaka refa aende kwenye screen lakini wachezaji wa Yanga wameshika tu viuno wanashangaa. Ile nafasi ardhimu sana mmepata kutokana na jitihada zenu za mapambano ila mwisho mmeshindwa kumalizia jambo dogo kabisa kwasababu ya kujiona timu ndogo, kujiona mlipofikia sio haba.

Hili wachezaji wajifunze siku nyingine kudai haki yao, na viongozi mbadilike muone Yanga kwasasa ni kubwa sio kifedha bali kiubora hivyo ni wajazeni wachezaji mentality ya kukataa unyonge wa kimaamuzi endapo VAR ipo, ndiyo iliyoletwa kama suluhisho ya kupata haki kwasasa. .

Mwisho, turudi kutetea makombe ya NBC na FA ya klabu bingwa yamepita tujirekebishe tulipokosea na kurudi imara zaidi msimu ujao.

La mwisho naomba uzi huu usijadiliwe na watu walioshinda TATU MZUKA, waende kujadiliana jinsi ya kugawana zawadi za tatu mzuka walizopewa na aliyezoeana nae.
 
GKfAkJqXYAEOetn.jpg
 
Back
Top Bottom