Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,640
- 697,994
Mara zote tunaowaamini sana ndio wanaotuangusha ama kutuumiza sana.. Waulize wote waliowahi kujitapa
Nina boda wangu
Nina fundi wangu
Nina mganga wangu
Nina mtu wangu nknk
Hawa ni watu walijihakikishia uamifu kwako lakini rohoni mwao ni umbwa mwitu wakali mno.. Na nyakati zinapotimia utawaona katika uhalisia wao
Wa kumwamini pekee kwa asilimia 100 ni Mungu mwenye enzi yote, lakini sisi viumbe wake tuna kasoro kubwa kwenye hilo eneo.. Tuaminiane kwa machale sana..
Mjomba ni mama lakini Saddam Hussein alisalitiwa na mjomba wake wa damu ziwa moja na mama yake mzazi toka nitoke!
Katika maisha pia ukiondoa kundi la unaowaamini, kuna makundi mengine ya namna hiyo hujiinua hasa pale yanapokuona una kitu cha kuwapa kutokana na nafasi yako ama uwezo wako.. Kamwe haya makundi hayaendi kwa fukara
Makundi ya kusifu na kuabudu
Makundi ya kujifanya watetezi wako
Makundi ya kujifanya walinzi wako nk
Kwenye mfumo wa viumbe hai kuna wazuri na wabaya.. Kiumbe hai kama chawa si kiumbe chema hata kidogo.. Hiki ni papasi ni kupe chenye kazi moja tuu kikunyonye damu kinenepe wewe ukonde upate maradhi hakijali...!
Pamoja na hulka ya binadamu kupenda kusifiwa( ni hitaji la kiasili la mwanadamu) epuka sana kuwa na kundi linaloitwa chawa! Kama chawa mdudu asivyo na faida mwilini ndio chawa mtu asivyo na faida yoyote katika maisha yako
Kama mzazi kuna nyakati kipimajoto cha changamoto hupanda na kufikia nyuzijoto 1000, si kutokana na makosa yako la hasha bali kutokana na kuangushwa na wale uliowaamini kwa asilimia 2000 huku wakipewa chapuo na makundi ya kusifu na kuabudu na chawa!
Kuna ukweli huja kujifunua mambo yakiwa yameshakorogeka na kuharibika mno!
Hata uwe na watoto 20 wenye ujuzi wa kila fani, unapowakasimu majukumu usiwaamini kwa asilimia zote! Nawe ujiridhishe kwa kuwafuatilia ili wasije kukuangushia jumba bovu
Maumivu ya kusalitiwa kimyakimya na wanafamilia ni makali kuliko kelele za unayedhani ni adui wa kutengenezewa anayejaribu kukuambia hapo unapigwaaa.. Gutukaaa...
SASA ufanyeje uchungu wa kuumizwa na kusalitiwa sometimes hupunguzwa na machozi! Lakini kama mzazi huwezi kutoa machozi yako mbele ya familia.. Wala huwezi kujifungia chumbani ulie.. Watajua tuu
Wala huwezi kukimbilia ukweni.. Huna hakika kama wana upendo wa dhati nawe!
Sasa ufanyeje? Kuponya haya majeraha? Utamtafuta mama ukalie weee mpaka uchoke na kama mama hayupo utamatafuta mjomba hata kama yuko mbali
Utaenda huko ukapumzike kwa muda na kujitafakari, ujitafute na kumlilia Mola wako kwenye mitihani ya walimwengu..!
Mjomba ni mama lakini hawezi kuaminika kwa asilimia 100 kama mama.. Ni vema kuwa makini mzazi asije akaruka ndogo na kukanyaga kubwa.
Sent using Jamii Forums mobile app