Macho ya kinabii yatumike kuboresha vetting zetu nchini

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,109
22,561
Salaam, Shalom!!

INTRODUCTON.

Napoongelea macho ya kinabii, Siongelei hao mnaowaita wazee wa kamati, HAPANA. Pia sichanganyi dini na siasa, sababu Asili ya Siasa ni Mbinguni, sasa Mwana wa Mungu nakupa codes Kutoka JUU, ambazo zaweza kututoa hapa kwenye mkwamo.

Wakati Nchi zilizoendelea zikipiga hatua Kwa kufanya uchaguzi sahihi wa nini mtoto asomee Kwa kuhusisha uchanganuzi makini juu ya mtoto mdogo chini ya umri wa mwaka mmoja, wazazi wa kitanzania Bado tunapeleka watoto shule Kwa mkumbo na mazoea!!

AFYA
Hivi Hawa madaktari wanaosahau mkasi ndani ya tumbo la mgonjwa wakati wa operation, ni madaktari halisi au walitumwa na wazazi wao kuwa madaktari?

BIASHARA
Tumefikaje hapa Leo wafanyabiashara wanapoficha mafuta Ili wapate faida mara dufu bila kujali athari wanazosababisha Kwa Taifa na JAMII Kwa ujumla?

Wafanyabiashara Hawa ni wafanyabiashara Kutoka tumboni mwa wazazi wao kama mission Yao duniani, au wameingia kwenye biashara baada ya kufeli mitihani darasani?

UJENZI
Majengo wajengayo engineers wetu yanaporipotiwa kuanguka yenyewe, je wahusika ni Engineers Kwa Kuzaliwa au wa kutengenezwa?

Bankers wanapopelekwa kusimamia engineers kujenga Bwawa letu, je ni uamuzi sahihi?

Tunaona hatimaye nyufa zikijitojeza, je miaka 60 ya uhuru hatuna engineers wa Kuzaliwa tuwasomeshe watusaidie?

SIASA
Je, ni sawa viongozi wa kisiasa kumiliki na kuanzisha na biashara ya kubahatisha, maarufu kama betting?

Je ni wanasiasa Kwa Kuzaliwa au ni wa kutengenezwa au wamerithishwa siasa Kwa kusukumizwa?

TIBA ASILI
Ni sawa wapiga ndumba wanaojitambulisha kama wataalamu wa TIBA asili kuacha viringe na kukimbilia kupata nafasi za kisiasa?

UVUVI
Je, wanaovua samaki Kwa kutumia Sumu, ni wavuvi wa asili Kwa Kuzaliwa au ni wavuvi wa kujituma au kusukumizwa au wa kurithi?

SIASA.

Ni sawa, Professor kuacha kufundisha chuoni Ili kwenda kugombea ubunge?

Mtu huyo aliingiaje huko au aliwahi jua alizaliwa awe nani?

ELIMU
Imekuwaje asiye mwalimu Kwa Kuzaliwa kuingia darasani? Kwanini kupoteza muda kufanya shughuli ambayo Si fani Yako uloitiwa tangu tumboni?

Wazazi, Serikali na JAMII Kwa ujumla tukirudi kwenye msingi huu Nchi yetu itapiga hatua Kwa haraka sana.

MADA: UMUHIMU WA MACHO YA KINABII ULIVYOLETA TIJA KWA TAIFA LA ISRAEL.

SIASA
Daudi, mtoto aliyezaliwa na mke mdogo wa Yesse, mchunga Kondoo, hakujua chochote juu ya hatima yake yake mbeleni.

Mzazi wa Daudi Mzee Yesse naye hakujua kuwa Kutoka viunoni mwake atatokea mfalme,

Nabii wa Mungu aitwaye Samweli anakwenda nyumbani Kwa Yesse na kuwambia wamtafute mtoto mdogo Daudi mchunga Kondoo porini ndiye aje kuwa mrithi wa mfalme aliyekuwepo wakati huo aitwaye Sauli.

Na mtoto huyo Daudi akaja kuwa Mfalme Bora kabisa kuwahi Kutokea,

Daudi alikuwa Nabii, pia askari shujaa na kiongozi mwenye BUSARA.

Iweje katika Taifa letu viongozi wapigane vikumbo kugombea Urais ilhali Rais yupo na wautake urais bila kuwa chaguo la Mungu katika nafasi hiyo?

Jicho la Nabii linahitajika hapa!!!

UONGOZI
Kisa Cha Ben Hadad, Elisha na Hazaeli ktk (2 Wafalme 8:7,8,9....) Na (2 Wafalme 13:22).

Ben Hadad, Mfalme wa Shamu katika Nchi ya ISRAEL anaugua, anamtuma Hazael msaidizi au Waziri wake aende Kwa Nabii Elisha Ili aulizwe ikiwa atapona katika ugonjwa Ule au atakufa.

Hazaeli anafika Kwa Nabii Elisha, Baada ya kufikisha ujumbe, Elisha anamjibu Hazael kuwa Mfalme atakufa, lakini anamwambia Hazael usimwambie kuwa atakufa, mwambie nimesema atapona.

Na Baada ya kusema hivyo, nabii anamwangalia Usoni Hazael Kisha analia Kwa uchungu,

Hazaeli anauliza unalia nini, Nabii anamwambia Nakuona miaka michache ijayo, utakuwa Mfalme baada ya Ben Hadad kufariki na utakuwa mwiba juu ya watu wangu,

Hazael anahamaki na kusema Mimi?

Macho ya Nabii Yana uwezo wa kuona MBELE na MBALI sana.

Turudi katika mstari turekebishe Nchi yetu.

UTUMISHI/UNABII
Mama mzazi wa Samweli anaenda hekaluni na kuweka nadhiri Kwa Mungu Ili Mungu amjalie mtoto wa kiume Kwa nadhiri kuwa, mtoto huyo atakapozaliwa awe mtumishi wa Mungu madhabahuni.

Na Kweli mtoto Samweli anazaliwa, na Mama anaenda mkabidhi hekaluni alelewe na kukulia hekaluni chini ya Eli mtumishi.

Leo hii Hawa manabii fake wametoka katika familia na JAMII zetu, tumekosea wapi?

Kwanini hatupati Manabii wengi mfano WA Mwl Mwakasege?

Kwanini hatuwapimi watoto tangu utoto wao kujua kusudi la Mungu juu Yao ?

Je huyu ndugu Pascal Mayalla asili Toka tumboni ni mwandishi wa habari, au ni huyu aliyegombea ubunge Jimbo la kawe?

Karibuni🙏 Amen.

ITAENDELEA....
 
Nabii mkuu Joe Devie anasemaje kuhusu hili ?

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
20230921_010300.jpg
 
Napoongelea macho ya kinabii, Siongelei hao mnaowaita wazee wa kamati, HAPANA. Pia sichanganyi dini na siasa, sababu Asili ya Siasa ni Mbinguni, sasa Mwana wa Mungu nakupa codes Kutoka JUU, ambazo zaweza kututoa hapa kwenye mkwamo.

Wakati Nchi zilizoendelea zikipiga hatua Kwa kufanya uchaguzi sahihi wa nini mtoto asomee Kwa kuhusisha uchanganuzi makini juu ya mtoto mdogo chini ya umri wa mwaka mmoja, wazazi wa kitanzania Bado tunapeleka watoto shule Kwa mkumbo!!

AFYA
Hivi Hawa madaktari wanaosahau mkasi ndani ya tumbo la mgonjwa wakati wa operation, ni madaktari halisi au walitumwa na wazazi wao kuwa madaktari?

BIASHARA
Tumefikaje hapa Leo wafanyabiashara wanapoficha mafuta Ili wapate faida mara dufu bila kujali athari wanazosababisha Kwa Taifa na JAMII Kwa ujumla?

Wafanyabiashara Hawa ni wafanyabiashara Kutoka tumboni mwa wazazi wao kama mission Yao duniani, au wameingia kwenye biashara baada ya kufeli mitihani darasani?

UJENZI
Majengo wajengayo engineers wetu yanaporipotiwa kuanguka yenyewe, je wahusika ni Engineers Kwa Kuzaliwa au wa kutengenezwa?

Bankers wanapopelekwa kusimamia engineers kujenga Bwawa letu, je ni uamuzi sahihi?

Tunaona hatimaye nyufa zikijitojeza, je miaka 60 ya uhuru hatuna engineers wa Kuzaliwa tuwasomeshe watusaidie?

SIASA
Je, ni sawa viongozi wa kisiasa kumiliki na kuanzisha na biashara ya kubahatisha, maarufu kama betting?

Je ni wanasiasa Kwa Kuzaliwa au ni wa kutengenezwa au wamerithishwa siasa Kwa kusukumizwa?

TIBA ASILI
Ni sawa wapiga ndumba wanaojitambulisha kama wataalamu wa TIBA asili kuacha viringe na kukimbilia kupata nafasi za kisiasa?

UVUVI
Je, wanaovua samaki Kwa kutumia Sumu, ni wavuvi wa asili Kwa Kuzaliwa au ni wavuvi wa kujituma au kusukumizwa au wa kurithi?

SIASA.

Ni sawa, Professor kuacha kufundisha chuoni Ili kwenda kugombea ubunge?

Mtu huyo aliingiaje huko au aliwahi jua alizaliwa awe nani?

ELIMU
Imekuwaje asiye mwalimu Kwa Kuzaliwa kuingia darasani? Kwanini kupoteza muda kufanya shughuli ambayo Si fani Yako uloitiwa tangu tumboni?

Wazazi, Serikali na JAMII Kwa ujumla tukirudi kwenye msingi huu Nchi yetu itapiga hatua Kwa haraka sana.

UMUHIMU WA MACHO YA KINABII YALIVYOLETA TIJA KWA TAIFA LA ISRAEL.

SIASA
Daudi, mtoto aliyezaliwa na mke mdogo wa Yesse, mchunga Kondoo, hakujua chochote juu ya hatima yake yake mbeleni.

Mzazi wa Daudi Mzee Yesse naye hakujua kuwa Kutoka viunoni mwake atatokea mfalme,

Nabii wa Mungu aitwaye Samweli anakwenda nyumbani Kwa Yesse na kuwambia wamtafute mtoto mdogo Daudi mchunga Kondoo porini ndiye aje kuwa mrithi wa mfalme aliyekuwepo wakati huo aitwaye Sauli.

Na mtoto huyo Daudi akaja kuwa Mfalme Bora kabisa kuwahi Kutokea,

Daudi alikuwa Nabii, pia askari shujaa na kiongozi mwenye BUSARA.

Iweje katika Taifa letu viongozi wapigane vikumbo kugombea Urais ilhali Rais yupo na wautake urais bila kuwa chaguo la Mungu katika nafasi hiyo?

Jicho la Nabii linahitajika hapa!!!

UONGOZI
Kisa Cha Ben Hadad, Elisha na Hazaeli ktk (2 Wafalme 8:7,8,9....) Na (2 Wafalme 13:22).

Ben Hadad, Mfalme wa Shamu katika Nchi ya ISRAEL anaugua, anamtuma Hazael msaidizi au Waziri wake aende Kwa Nabii Elisha Ili aulizwe ikiwa atapona katika ugonjwa Ule au atakufa.

Hazaeli anafika Kwa Nabii Elisha, Baada ya kufikisha ujumbe, Elisha anamjibu Hazael kuwa Mfalme atakufa, lakini anamwambia Hazael usimwambie kuwa atakufa, mwambie nimesema atapona.

Na Baada ya kusema hivyo, nabii anamwangalia Usoni Hazael Kisha analia Kwa uchungu,

Hazaeli anauliza unalia nini, Nabii anamwambia Nakuona miaka michache ijayo, utakuwa Mfalme baada ya Ben Hadad kufariki na utakuwa mwiba juu ya watu wangu,

Hazael anahamaki na kusema Mimi?

Macho ya Nabii Yana uwezo wa kuona MBELE na MBALI sana.

Turudi katika mstari turekebishe Nchi yetu.

UTUMISHI/UNABII
Mama mzazi wa Samweli anaenda hekaluni na kuweka nadhiri Kwa Mungu Ili Mungu amjalie mtoto wa kiume Kwa nadhiri kuwa, mtoto huyo atakapozaliwa awe mtumishi wa Mungu madhabahuni.

Na Kweli mtoto Samweli anazaliwa, na Mama anaenda mkabidhi hekaluni alelewe na kukulia hekaluni chini ya Eli mtumishi.

Leo hii Hawa manabii fake wametoka katika familia na JAMII zetu, tumekosea wapi?

Kwanini hatupati Manabii wengi mfano WA Mwl Mwakasege?

Kwanini hatuwapimi watoto tangu utoto wao kujua kusudi la Mungu juu Yao ?

Karibuni🙏 Amen.
Umesema vyema.shida ni kwa sababu Nchi haina dini.la pili hatuna mfumo mzuri wa kuendesha unabii bila kujichanganya!! Lakini nikwambie kuwa tunao manabii wa kweli kabisa .wapo waliyotabiri kifo Cha JPm na namna itakavyokuwa .ndiyo maana ninapoona watu wanasema eti alikufa kwa korona nacheka tu!;

Kipindi Cha Nyerere Kuna manabii walikuponya taifa Hili na majanga makubwa

Sasa mfano kiongozi walinzi wake ni majini ukimpelekea unabii wa kimbingu si atakuchinja kama punguani herode alivyomfanya Yohana mbatizaji?
 
Hapo ndipo lilipo tatizo.
 
Bandiko zuri ila watakaokuelewa sasa ni wachache mno, hisia ya 6 hazifanyi kazi
Ni WAJIBU wa mwalimu kuhakikisha mwanafunzi anaelewa pamoja na tofauti za uelewa kati ya mwanafunzi na mwanafunzi!!
 
Nabii mkuu Joe Devie anasemaje kuhusu hili ?

USSR

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
Najiuliza ndugu USSR, ulitumia vigezo Gani kuwapeleka shule wanao?

Are u sure kwamba wapo Mahali sahihi?

Je unajua madhara ya kumpeleka mtunza hazina au banker kwa Kuzaliwa akawe Engineer wa majengo?

Masanja mkandamizaji Kwa Mfano ,amepoteza zaidi ya miaka 20 na ushehe darasani akisomea alichosemea kumbe anapoteza muda na alikuwa anapoteza Bure pesa za wazazi.

Ingekuwa vipi wazazi wangegundua nini Hasa mission ya masanja duniani tangu utoto na kuwekeza huko,

Tungepata faida kiasi Gani katika level ya Taifa na JAMII Kwa ujumla?
 
Nawauliza ndugu Watanzania wenzangu,

Hivi hakimu wa Kuzaliwa Toka tumboni mwa mamaye, unaweza kumuhonga Ili apotoe HUKUMU?
 
Rabbon, pa kuanzia ni kwenye katiba..katiba iunde uwepo wa taasisi ya urais kuwa na chombo chake cha ushauri juu ya uongozi wa nchi..(supreme presidential advisory council) chombo hiki kinaundwa na viongozi wa kiimani, wenye umri mkubwa na rekodi isiyotiliwa shaka kwenye utumishi wao..si jambo la ajabu kujua kwamba viongozi hawa hutumia muda mwingi kuongea na Mungu na hivyo Mungu atasema na watu wake na viongozi kupitia wao juu ya lolote linahusu nchi yetu, uongozi, uchumi, hatari, uovu, nk..
 
Rabbon, pa kuanzia ni kwenye katiba..katiba iunde uwepo wa taasisi ya urais kuwa na chombo chake cha ushauri juu ya uongozi wa nchi..(supreme presidential advisory council) chombo hikikinaundwa na viongozi wa kiimani, wenye umri mkubwa na rekodi isiyotiliwa shaka kwenye utumishi wao..si jambo la ajabu kujua kwamba viongozi hawa hutumia muda mwingi kuongea na Mungu na hivyo Mungu atasema na watu wake na viongozi kupitia wao juu ya lolote linahusu nchi yetu, uongozi, uchumi, hatari, uovu, nk..
Naunga mkono wazo lako 100%. Maana Kuna TABIA imejengeka na inashika Kasi viongozi kurithishana madaraka,

Karume Senior, kampa Karume junior, Mwinyi senior naye akamtoa Mwinyi junior, sasa tukifikiri huu ndio mwelekeo, tutakuja KUONGOZWA na walevi, maana kiwanda Cha kiuno kina mambo Si haba!!!

Sikatai kuwa Rais anaweza kuzaa Rais, maana tumeona katika maandiko Mfalme DAUDI akimrithisha mwanaye Suleiman Ufalme.

Lakini pia Si Kweli kuwa Kila Rais anaweza kutuachia Rais Kutoka viunoni mwake, mfano Mzuri, Mfalme Sauli alikuwa na mtoto wake Alieitwa Nathanael Rafiki mkubwa wa Daudi, hakupata KIBALI kumrithi babaye, alikuwa mtu wa kawaida tu na maisha yakaenda.

Macho ya kinabii yanahitajika hapa!!
 
Back
Top Bottom