Machinjio kufungwa mashine maalum

Machinjio kufungwa mashine maalum

Mbogo Junior

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2012
Posts
250
Reaction score
66
Kuna uwezekano mkubwa machinjio yote ya serikali kufungwa mashine maalum za kuchinjia wanyama za kuendeshwa na nguvu ya umeme. Hii ni kutokana na kushindwa kupata muafaka wa jambo hili.
Nawasilisha.
 
nasapoti hiyo kitu. tuachane kabisa na watu wa dini fulani tu ndio wachinje....au kama wanataka kuchinja basi wasipate ujira wala wasiondoke na hata kilo moja ya nyama....manake hilo ndo mojawapo ya tatizo....mchinjani hatoki mikono mitupu...hahahaha. ndo maana watu wametoa ndita wanaona wananyang'anywa tonge mdomoni.
 
Bado kuna watakaotaka "haki" ya kuchinja..
 
Nafikiri hili ni jambo la msingi ili kuwe na usawa wa dini zote nyama zitakuwakwenye packages zinasambazwa IT CAN BE THE SOLUTION
 
.......tatizo sio kuchinja, ....tatizo unamshukuru nani kabla ya kuchinja !
 
Kwa mujibu wa baadhi ya dini unapochinja mnyama kuna maneno yanasemwa,na mnyama anaelekezwa uelekeo fulani,je kama mashine ikifungwa na haijaelekezwa huko na maneno hayatamkwi si itakuwa ni tofauti na maelekezo ya dini yao? Na kama mashine ikielekezwa uelekeo huo au maandishi yakawekwa kwenye kisu cha mashine si wa dini nyingine wataona hawajatendewa haki? Na operator wa mashine atatoka dini ipi ili kuwe na usawa?
 
Halafu hiyo mashine itatakiwa kuwa operated na purely mpagani.

Hakuna maneno ya kuomba wala kushukuru maana hawa wanyama tulishapewa na Muumba toka mwanzo wa dunia,tunaotaka kushukuru tutashukuru kikiiva!!

Mpagani wetu wa kuchinja yeye kazi yake ni kubonyeza tu kitufe, kichwa cha ng'ombe kule!
Kisha anaita, Mwingine....! Mwingine....!
 
Bado kuna watakaotaka "haki" ya kuchinja..

kweli kabisa nacho amini hizo machine lazima zitatakiwa zisomewe dua na dini flani ili kujiaminisha kuwa nyama hiyo itakayo chinjwa na mitambo hiyo iwe halali! Mfano mnyama mkali kama nyati huwa anapigwa risasi ambayo mpigaji huisomea dua ili kuihalalisha.sasa hiyo mitambo itasomewa dua na nani kati ya hizi dini kuu mbili?
 
Mi sidhani kama suala la kuchinja ni ishu kiasi hicho, suala la kuchinja liwe ni kazi kama kazi zingine watu waombe hiyo kazi na waajiriwe kama wanavyojiriwa watu wengine serikalini bila kujari dini ya mtu.
 
Halafu hiyo mashine itatakiwa kuwa operated na purely mpagani.

Hakuna maneno ya kuomba wala kushukuru maana hawa wanyama tulishapewa na Muumba toka mwanzo wa dunia,tunaotaka kushukuru tutashukuru kikiiva!!

Mpagani wetu wa kuchinja yeye kazi yake ni kubonyeza tu kitufe, kichwa cha ng'ombe kule!
Kisha anaita, Mwingine....! Mwingine....!
Hata ile asilimia ndogo ya Waislamu wa Tanzania wanaomuona Mkristo na Myahudi kuwa ni katika ahlul kitaab nao mtawakosa!

Kwao wao wanaweza kula kilichochinjwa na Mkristo lakini hakuna ikhtilaaf yoyote miongoni mwa Waislamu kuwa kilichochinjwa na mpagani ni haramu.

Sakata linaelekea patamu...!
 
Karne ya 21 tunadiscuss nani wa kuchinja nazani ata wazee wetu wanatushangaa kwa kupoteza mda kudiscuss very time wsting issues kama izi
 
nasapoti hiyo kitu. tuachane kabisa na watu wa dini fulani tu ndio wachinje....au kama wanataka kuchinja basi wasipate ujira wala wasiondoke na hata kilo moja ya nyama....manake hilo ndo mojawapo ya tatizo....mchinjani hatoki mikono mitupu...hahahaha. ndo maana watu wametoa ndita wanaona wananyang'anywa tonge mdomoni.

kwa hiyo na nyie mlikuwa mnataka shingo
 
Kwa mujibu wa baadhi ya dini unapochinja mnyama kuna maneno yanasemwa,na mnyama anaelekezwa uelekeo fulani,je kama mashine ikifungwa na haijaelekezwa huko na maneno hayatamkwi si itakuwa ni tofauti na maelekezo ya dini yao? Na kama mashine ikielekezwa uelekeo huo au maandishi yakawekwa kwenye kisu cha mashine si wa dini nyingine wataona hawajatendewa haki? Na operator wa mashine atatoka dini ipi ili kuwe na usawa?

Kama shida ni kutaamka maneno sio tatizo, hayo maneno si yanarekodiwa kwenye disk, mashine kabla haijachinja ina play hayo maneno na inaanza kazi. Mambo yote yanawezekana kwenye dunia ya digitali.
 
Back
Top Bottom