Mahatma Gandhi
Member
- Jan 16, 2012
- 25
- 15
Kuanzia jana ilikuwa ni kilio kwa wafanyabiashara wadogowadogo na mamachinga wanaofanya biashara zao maeneo ya Ubungo(Dar) karibu na mitambo ya kuzalisha umemena kandokando ya barabara pale askari Polisi walipowafukuza kwa mabomu ya machozi(na kuchukua bidhaa zao).Serikali inadai kuwa wasifanyie biashara karibu na barabara na pia mitambo ya Tanesco kwani ni hatari.Lakini tujiulize,hawa WAMEJIAJIRI ili kuondo utegemezi na kujipatia kipato ili kupunguza umaskini(ahadi ya CCM 2005) ila serikali inakinzana na juhudi zao.Sasa je serikali imeandaa mikakati gani ya kuwasaidia??mi najua hakuna nchi yoyote kubwa iliyoendelea bila kuwa na sekta isiyo rasmi(informal sector) katika uchumi.Au hizi ni hasira za CCM kuangukia pua kule Arumeru na maeneo mengine ya uchaguzi?.........tatafakali!!!!:yell: