Machinga Ubungo wapigwa mabomu.............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Machinga Ubungo wapigwa mabomu..............

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mahatma Gandhi, Apr 4, 2012.

 1. Mahatma Gandhi

  Mahatma Gandhi Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuanzia jana ilikuwa ni kilio kwa wafanyabiashara wadogowadogo na mamachinga wanaofanya biashara zao maeneo ya Ubungo(Dar) karibu na mitambo ya kuzalisha umemena kandokando ya barabara pale askari Polisi walipowafukuza kwa mabomu ya machozi(na kuchukua bidhaa zao).Serikali inadai kuwa wasifanyie biashara karibu na barabara na pia mitambo ya Tanesco kwani ni hatari.Lakini tujiulize,hawa WAMEJIAJIRI ili kuondo utegemezi na kujipatia kipato ili kupunguza umaskini(ahadi ya CCM 2005) ila serikali inakinzana na juhudi zao.Sasa je serikali imeandaa mikakati gani ya kuwasaidia??mi najua hakuna nchi yoyote kubwa iliyoendelea bila kuwa na sekta isiyo rasmi(informal sector) katika uchumi.Au hizi ni hasira za CCM kuangukia pua kule Arumeru na maeneo mengine ya uchaguzi?.........tatafakali!!!!:yell:
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 6,999
  Trophy Points: 280
  Mkuu kuna mambo ya kisiasa lakini sio hili
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Sheria za nchi ni lazima ziheshimiwe, naona serikali sasa imeota meno na kuanza kubweka.
   
 4. i

  iMind JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Wakipata tatizo hapo walipo, utakua wa kwanza kuilamu serikali kwamba haikuchukua hatua.Pamoja na kutafuta riziki, lakini lazima riziki itafutwe kwa njia halali na utaratibu uliowekwa. Sasa kila mtu akijiamlia kufanya anavyojisikia eti kwa kisingizio cha kujitafutia riziki, Nchi itakalika kweli. Fikiria Chukua hatua.
   
 5. y

  yien New Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  siku zote sherikali ilikuwa wapi kuwaondoa machinga ubungo?wamewaandalia sehemu za kwenda kuendeshea biashara zao?Serikali haiono kuongezea uporaji,ubakaji na unyanganyi kwa kutumia Bisibisi,Mapanga,Nondo toka kwa machinga Mitaani kwa kuwaondoa bila ya kuweka utaratibu maalum?.
   
Loading...