Jengo la TANESCO ni bora likageuzwa kuwa Ubungo Machinga Center kusaidia watu kujiajiri na ku-boost uchumi wa nchi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,023
144,381
Katika hali ya sasa ambapo kuna taarifa kuwa uchumi wa nchi hauonyeshi dalili nzuri kwa siku zijazo, watu hawana ajira na biashara nyingi, hasa biashara ndongo ndongo, zimeathiriwa na bomoabomoa;ni vizuri jengo hili badala ya kulibomoa, ligeuzwe kuwa kituo cha cha biashara cha wamachinga au hata Ubungo Commercial Centre kwa wafanyabiashara wakubwa.

Jambo moja ambalo watu hawalitizami kwa mapana yake ni athari za bomoabomoa kupisha ujenzi wa reli ya kisasa pamoja na ujenzi wa barabara ya juu maeneo ya ubungo huku biashara zinazokufa au kuathirika kutokana na ujenzi wa hii miradi mikubwa zikipotoe bila kuwa na mkakati wa kuzi-replace.

Biashsara zinazopotea kutokana na ujenzi wa hii miradi sio tu zilikuwa zinatoa ajira kwa watu,bali zingine zilikuwa zinachangia katika kujenga uchumi wa nchi kwani serikali kuu na Halmashauri zilikuwa zinaingiza kipato kupitia biashara hizi.

Hivyo basi,ili kupunguza athari kwa maisha ya watu na ili ku-boost uchumi wa nchi,jengo hili la gorofa zipatazo 9 ni bora sasa tukalifanya kuwa ni kituo cha wafanyabiashara wadogo(Ubungo Maching Center) au Ubungo Commercial Center kwa ajili ya wafanyabishara wakubwa.

Floor chache za chini zinaweza kutengwa kwa ajili ya wamachinga ambao sasa wanakazimika kujibana katika njia za wapita kwa miguu baada ya kukosa sehemu za kufanyia biashara baada ya kubomolewa vibanda vyao kwa watakaotaka na floor za juu zikatumiwa na wafanyabiashara wwakubwa au hata zikatumika kama maofisi,n.k

Pia nashashauri gharama zitakazotumika kubomoa jengo hili ni bora zikatumika kufanyia marekebisho madogo katika jengo hili ili liweze kutumika kibiashara kama kwa kujenga vyoo, n.k kwa maana ya kuweka miundombinu itakayoliwezesha jengo hili kutumika kibiashara.

Watanzani wenzangu,ni lazima tutambue kuwa miradi hii japo ni jambo jema,lakini ina athari kubwa sana katika shughuli za kiuchumi za watu na Taifa kwa ujumla huku watu wakipoteza vitego uchumi vyao na kibaya zaidi hatuna viwanda vipya vinavyofungulia ambavyo vingeweza kuajiri hawa watu na bahati mbaya hata kilimo ambacho kingeweza kuajiro watu wengi nacho kinasuasua.

Tena serikali ingeweza kuamua kupangiaha jengo hili kwa gharama ndogo ili kuwawezesha watu wengi kulitumia kibiashara na serikali ikaja kukusanya kodi badala ya kulivunja.

Hata kama jengo hili si la serikali kama tunavyosikia, lakini naamini bado serikali inaweza kufikia makubaliana na mmliliki wa jengo hili kuwa halitavunjwa bali litumike kupangisha wafanyabiashara kwa gharama nafuu ili watu wengi zaidi walitumie kufanya biashara na kujipatia vipato na wakati huo huo serikali kuu au Manispaa iwe inakusanya kodi au ushuru kutoka kwa wafanyabiasha watakaowekeza mitaji yao katika jengo hili.

Tutambue tu mradi huu mradi wa reli ya kisasa pamoja na nia njema iliyopo, unakwenda kuathiri biashara ya mabasi na malori kule kote ambako reli hhii itapita, na kwa mtazamo wangu, mikopo ya mabenki kwa sekta hii ya usafirisha inaweza kuathirika na hata baadhi ya wamiliki wa mabasi na mlori wakajikuta wanashindwa kurudisha mikopo kama wapo waliochukua na hata mabenki yanaweza kupunguza utoaji wa mikopo kwa sekta hii kwa hofu ya kupata hasara na hii yote itaathiri uchumi wa nchi iwapo kweli hali itajitokeza kama ninavyofikiri japo mimi si mchumi wala mtalaamu wa mambo ya mabenki.

Kwa hali hii,ni bora serikali ikaanza kuchukua hatua za kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na ujio wa hii miradi pale inapowezekana kwa kuanza na hii jengo la TANESCO kama nilivyoshauri hapo juu.

Kwakuwa jengo hili bado limesimama na TANESCO wameshahama,ni bora sasa uamuzi wa kulivunja ukasitshwa na barabara ya juu ikapitishwa kwa kuwekwapa jengo hili na wakati huo huo eneo hili likawa ni kituo cha biashara na hivyo litachangia katika ku-boost uchumi wetu.

Tuue ndege wawili kwa jiwe moja.

Tusisahau miundombinu hii pekee haitotuvusha maana hata nchi kama Ethiopia wana treni za kisasa na miundombinu kama hii ila umasikini uko juu,watu hawana ajira na kila siku wanatoroka nchini mwao kusaka ajira na maisha bora katika mataifa mengine yakiwemo ya Africa.
 
Mpuuzi wewe
nyie sijui Aliye waroga kisha kufa au la!
Yaani Kutwa upuuzi upuuzi
hamjui mlicho lipigania jana leo mnakiponda
mkifanyiwa hili mnageuza lile!
 
We kamanda elewa kuwa ile interchange road itakayopatikana pale itakuwa na faida nyingi kule hiyo machinga complex unayowaza!!
 
Katika hali ya sasa ambapo kuna taarifa kuwa uchumi wa nchi hauonyeshi dalili nzuri kwa siku zijazo, watu hawana ajira na biashara nyingi, hasa biashara ndongo ndongo, zimeathiriwa na bomoabomoa;ni vizuri jengo hili badala ya kulibomoa, ligeuzwe kuwa kituo cha cha biashara cha wamachinga au hata Ubungo Commercial Centre.

Jambo moja ambalo watu hawalitizami kwa mapana yake ni athari za bomoabomoa kupisha ujenzi wa reli ya kisasa pamoja na ujenzi wa barabara ya juu maeneo ya ubungo huku biashara zinazokufa au kuathirika kutona na ujenzi wa hii miradi mikubwa zikipotoe bila kuwa na mkakati wa kuzi-replace.

Biashsara zinazopotea kutokana na ujenzi wa hii miradi sio tu zilikuwa zinatoa ajira kwa watu,bali zingine zilikuwa zinachangia katika kujenga uchumi wa nchi kwani serikali kuu na Halmashauri zilikuwa zinaingiza kipato kupitia biashara hizi.

Hivyo basi,ili kupunguza athari kwa maisha ya watu na ili ku-boost uchumi wa nchi,jengo hili la gorofa zipatazo 9 ni bora sasa tukalifanya kuwa ni kituo cha wafanyabiashara wadogo(Ubungo Maching Center au vinginevyo) au Ubungo Commercial Center.

Gharama zitakazotumika kubomoa jengo hili ni bora zikatumika kufanyia marekebisho madogo katika jengo hili ili liweze kutumika kibiashara kama kwa kujenga vyoo, n.k kwa maana ya kuweka miundombinu itakayoliwezesha jengo hili kutumika kibiashara.

Watanzani wenzangu,ni lazima tutambue kuwa miradi hii japo ni jambo jema,lakini ina athari kubwa sana katika shughuli za kiuchumi za watu na Taifa kwa ujumla huku watu wakipoteza vitego uchumi vyao na kibaya zaidi hatuna viwanda vipya vinavyofungulia ambavyo vingeweza kuajiri hawa watu na bahati mbaya hata kilimo ambacho kingeweza kuajiro watu wengi nacho kinasuasua.

Tena serikali ingeweza kuamua kupangiaha jengo hili kwa gharama ndogo ili kuwawezesha watu wengi kulitumia kibiashara na serikali ikaja kukusanya kodi badala ya kulivunja.

Hata kama jengo hili si la serikali kama tunavyosikia, lakini naamini bado serikali inaweza kufikia makubaliana na mmliliki wa jengo hili kuwa halitavunjwa bali litumike kupangisha wafanyabiashara kwa gharama nafuu ili watu wengi zaidi walitumie kufanya biashara na kujipatia vipato na wakati huo huo serikali kuu au Manispaa iwe inakusanya kodi au ushuru kutoka kwa wafanyabiasha watakaowekeza mitaji yao katika jengo hili.

Tutambue tu mradi huu mradi wa reli ya kisasa pamoja na nia njema iliyopo, unakwenda kuathiri biashara ya mabasi na malori kule kote ambako reli hhii itapita, na kwa mtazamo wangu, mikopo ya mabenki kwa sekta hii ya usafirisha inaweza kuathirika na hata baadhi ya wamiliki wa mabasi na mlori wakajikuta wanashindwa kurudisha mikopo kama wapo waliochukua na hata mabenki yanaweza kupunguza utoaji wa mikopo kwa sekta hii kwa hofu ya kupata hasara na hii yote itaathiri uchumi wa nchi iwapo kweli hali itajitokeza kama ninavyofikiri japo mimi si mchumi wala mtalaamu wa mambo ya mabenki.

Kwa hali hii,ni bora serikali ikaanza kuchukua hatua za kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na ujio wa hii miradi pale inapowezekana kwa kuanza na hii jengo la TANESCO kama nilivyoshauri hapo juu.

Kwakuwa jengo hili bado limesimama na TANESCO wameshahama,ni bora sasa uamuzi wa kulivunja ukasitshwa na barabara ya juu ikapitishwa kwa kuwekwapa jengo hili na wakati huo huo eneo hili likawa ni kituo cha biashara na hivyo litachangia katika ku-boost uchumi wetu.

Tuue ndege wawili kwa jiwe moja.
Wewe wa hovyo sana, nenda ilala pale machinga complex ujue upuuzi wa wamachinga, tena wakafie mbali kabisa..!
 
Hayo ni mawazo yako 'usie na akili', wenye 'akili zao' wanabomoa kupisha ujenzi wa flyover kupunguza msongamano wa magari kabla ya kuhamia dodoma.
 
Mkuu nimekuelewa sana sema huyu MTU tuliyeachiwa na mkwere hana huruma na sisi. Hasikii saut ya adhana wala ya mchota maji msikitini.

Tunasubiri nusura ya Mwenyezi mungu muweza Wa yote
 
Mpuuzi wewe
nyie sijui Aliye waroga kisha kufa au la!
Yaani Kutwa upuuzi upuuzi
hamjui mlicho lipigania jana leo mnakiponda
mkifanyiwa hili mnageuza lile!
861f13aa756139e1f32564bc2ba0cac4.jpg
 
Hapo ndipo leo umekuja na wazo la kujenga nchi, saa zingine lakini huwa unajitoa ufahamu maksudu, haya ndo mawazo, sijasoma contents lkn kichwa cha habari kimejieleza, hata mi naunga mkono wazo lako mkuu
 
Back
Top Bottom