isajorsergio
Platinum Member
- Apr 22, 2018
- 4,125
- 6,250
| Mexico / Estados Unidos Mexicanos / United Mexican States
Ni taifa linalopatikana bara Amerika Kaskazini na kwa kiasi Amerika ya Kati, likiwa na mipaka baina ya Marekani upande wa Kaskazini, bahari ya Pasifiki - Kusini Magharibi, Guatemala, Belize na bahari ya Karibi 'Caribbean' upande wa Kusini Mashariki pia ghuba ya Mexico - Mashariki.
Mexico ni yenye ukubwa wa eneo zipatazo 1,972,550 Km[SUP]2 [/SUP]sawa na 761,606 Sq Mile's ikiwa nyumbani kwa watu takribani millioni 128,932,753 kufikia Juni 7, 2020.
Bendera ya Mexico
Taifa hili lililoundwa na muungano wa majimbo 'States' 31 yenye asili ya Azteki 'Aztec' lisilokuwa na lugha rasmi bali zenye kuzungumzwa na wengi ambazo ni Kihispaniola, Mayan na Nahuatl huku likitumia Peso ya KiMexico (MXN) ambayo ni pesa rasmi, Peso 1 ni sawa Centavos 100.
Mexico DF ©N3otr3x
Kauli kuu ya taifa hili (Motto) ni "La Patria es Primero" | "Nyumbani Kwanza", mji mkuu ni Mexico City mji unaohodhi masuala ya serikali kuu na nyumbani kwa watu takribani millioni 24.
| Uchumi, Biashara, Kilimo, Maendeleo, Utalii na Uwekezaji
Mexico ni moja ya mataifa 15 yenye uchumi imara huku ikiwa kinara namba sita katika uzalishaji wa mafuta, namba nne katika uzalishaji wa umeme kupitia bwawa la Manuel Moreno Torres, namba tatu katika utandazaji wa solar na namba sita katika uzalishaji wa vifaa vya kielektroniki nyuma ya Uchina, Japan, Marekani, Korea Kusini na Taiwan.
Taifa hili lenye kusheheni viwanda vya runinga, tarakilishi, vishkwambi, moduli za mwanga (LCD & LED), bodi za saketi na magari kupitia mji wa Puebla.
Mastretta Halst ©Jeff Dion
Puebla City mji wenye zaidi ya viwanda 70 vya magari chapa ya KiMexicana Dina S.A na Mastretta huku ikiwa na viwanda vya General Motors, Ford, Chrysler, Volkswagen, Nissan, KIA, BMW, Mercedes-Benz na kiwanda cha urudufu chapa Audi.
Asilimia 30% ya magari yanayoonekana Marekani ni bidhaa bora ya KiMexicana (Made in Mexico).
| Kilimo na Ufugaji
Mexico ikiwa na ardhi yenye rutuba mzalishaji wa nyanya, mahindi, maharage, parachichi, pilipili, matunda, kahawa, ngano, miwa, ndizi, mayai, maziwa na nyama.
Mbegu za Chia ©Gerdukes
Chimbuko asilia la mbegu za Chia 'Chia Seeds', ardhi yenye kutoa maharage aina 63 na sehemu ya tafiti chini ya shirika la chakula na dawa.
| Utalii
Pango la Grotto ©Alade Cuervo
Utalii ndani ya Mexico unachagizwa na historia ya kale ya Azteki 'Aztec', Mayan na Nahuatl kupitia Pramidi za Teotihuacan, ghuba ya California na peninsula ya Yucatan. Mexico ni taifa la saba kuwa na maeneo mengi ya urithi wa dunia.
Teotihuacan ©Annca
Uwapo Mexico utashuhudia miji iliyoendelea kama Guadalajara, León, Puebla, Monterrey, Murclia, Ciudad Juarez, Hermasillo, Chihuahua, Saltillo, San Luis Potosi, Aguascalientes, Tijuana, Merida, Mexicali, Culiacan na Veracruz iliyoungwa vyema na miundombinu ya barabara, umeme, gesi na treni.
Mji wa Guanajuato ©Cello5
Barabara ndani ya taifa ni takribani kilomita 370,000 huku kilomita 119, 200 ni za kiwango cha rami, kilomita 11,100 njia tatu, 10,100 njia nne na kilomita 2,000 zikiwa na njia 6 na kuendelea.
Gota de Plata ©Jjnanni
| Elimu, Sayansi na Teknolojia
Mexico yenye elimu ya kiwango cha kati, ikiwa na wasomi kwa asilimia 92% na vyuo bora kama National Autonomous University of Mexico, University of Guadalajara, Monterrey Institute of Technology and Higher Education na Universidad Panaméricana.
Chuo kikuu cha Guanajuato ©Photobella
Ni taifa lenye uwezo wa juu katika sayansi ya anga za mbali, vifaa vya ulinzi na usalama na uwezo wa kuchakata mabomu ya atomiki.
Polisi wa KiMexicana ©Emilia Donaila
Kupitia jeshi la taifa la KiMexicana linazalisha bunduki, vilipuzi, mabomu, mifumo ya ulinzi, ndege na magari ya kijeshi. Mexico inatumia mifumo, mitambo na vifaa vya kijeshi, ulinzi na usalama vilivyotengenezwa ndani ya taifa kwa asilimia 99.9%.
| Teknolojia na Sayansi ya Mawasiliano
Kama taifa Mexico ni msambazaji wa mifumo ya teknolojia ya mawasiliano katika ukanda wa Karibi 'Caribbean' na Latini ikiwa na satelaiti kadhaa chapa Satmex ambazo husaidia dunia katika usambazaji wa intaneti na urushaji wa matangazo kidigitali pia kampuni za mawasiliano Teléfonos de México (Telmex), Axtel, Maxcom, Alestra, Marcatel na AT&T MX.
Asilimia 90% ya vijana kuanzia miaka 14 na kuendelea wanamiliki simu, asilimia 65% ya miaka 20 na kuendelea wakimiliki tarakilishi.
Makao makuu ya Televisa ©Prodsco
Mexico ni nyumbani kwa kituo nambari moja cha kimataifa katika uandaaji, uchakataji, uzalishaji na urushaji wa maudhui yenye lugha ya Kihispaniola kinachofahamika kama Televisa.
| Sanaa, Michezo, Uandishi, Filamu na Muziki
Mexico ni sehemu ya sanaa toka enzi za Azteki 'Aztec', Mayan na Nahuatl huku ikiwa imesheheni wachoraji kama Joaquin Clausell, Frida Kahlo, Diego Rivera, Federico Cantú Garza, Juan O'Gormani, Rufino Tamayo, Verónica Ruiz de Velasco na Francisco Toledo.
Uwanja wa michezo Azteca ©Manu Carillo
Wasanifu wa majengo Mario Pani, Eugenio Peschard na Enrique de Moral pamoja na waandishi nguli mfano wa Carlos Fuentes, Juan Rulfo, Bruno Traven, Luis Spota, Alfonso Reyes na Valeria Luiselli.
| Michezo na Burudani
Carlos Vela ©Rigoy BK
Mchezo wenye wafuasi wengi ni mpira wa miguu unaowakilishwa vyema kimataifa na wachezaji Javier Hernandez Chichalito, Carlos Vera, Raúl Jimenez, Hirving Lozano, Andrés Guardado, Miguel Layún na Cristian Calderon.
Miguel Layún ©Maria Michelle
| Filamu na Picha
Ni taifa lililozalisha wapiga picha nguli Manuel Álvarez Bruno, Hector Garcia Cobu na Graciela Iturbide. Huku likiwa taifa nyumbani kwa watayarishaji, waongozaji na wachakataji filamu Guillermo Arriaga, Alejandro Gonzalez Iñarritu aliyezitikisa filamu za Babel, Birdman na The Relevant.
Alfonso Cuarón ©Rafa Suarez
Pamoja na mwamba Alfonso Cuarón mshindi wa tuzo za Academy na Filmax aliyezichakata filamu za Harry Potter, Gravity, The Prisoner of Azkaban na Children of Men.
Lupita Nyong'o ©LA Times
Muigizaji wa kimataifa na mshindi wa tuzo ya Oscar Lupita Nyong'o ni mzaliwa na raia wa Mexico.
Carlos Santana ©Roci Ho
Katika muziki Mexico inatambulishwa vyema na Dulce María kutoka katika familia ya mchoraji Frida Kahlo, Thalía, Marco Antonia Solis na gwiji Carlos Santana aliyetamba na The Game of Love, Maria Maria, Pires Par Um Jeito, Oye Como Va na Why Do Not You and I.
Hii ndio Mexico 🇲🇽