Machimbo ya dhahabu bado nayadai

Machimbo ya dhahabu bado nayadai

Yuda Legacy

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2023
Posts
775
Reaction score
2,771
Licha ya kuchimba sana dhahabu Chunya na kusekesa Lakini dhahabu imekuwa ni adhabu kwangu kwa kukaa kwangu kote polini nimeambulia kupata nyunga tu za point moja zimezidi sana point saba

Licha ya kupiga sana sululu huku gold detector yenye ukubwa wa 7000 hapa nazungumzia Gp7000 ile ya kisasa kabisa Lakini bado dhahabu ni ngumu kupatikana je dhahabu ni nini jibu= dhahabu ni adhabu.

Licha ya kupona kufukiwa ndani ya long base ukiwa na kitochi tu huko chini na uki risk maisha yako kwa hali ya juu na chini Lakini kupata dhahabu sio rahisi kama wana jf wanavyo jidai wana yajua vizuri machimbo ya dhahabu Lakini kiuhalisia hakuna wajualo

Mpaka mda huu ninao zungumza nilikuwa nipo sehemu zangu nina ofisi kubwa na maisha yanaenda akaja jamaa yangu mmoja wa mda kidogo ndani ya Toyota IST kali nikamuuliza vipi mbona adim na maisha umeyapatia sana akasema yeye yuko chunya machimbo mda wote na story yake ilinivutia na Mimi kuingia kwenye biashara ya dhahabu ooh hapa ndipo nilipo kosea duka mpaka sasa limefilisika

Nimebaki mabega tu na shimo ndio kwanza linaanza wachimbaji wananipigia simu wanataka unga wa kula kambini na Mimi HELA sina.

Hadithi za machimbo ya dhahabu ni tamu kusikiliza nimeweka hela Kumbe nimefukia mazima hata elusion ndio kwanza sijafika hali iko Hivi ama kweli biashara ya dhahabu kashamzoba au kanyampasila au kachumbagira (Rip marehemu mkandala rufufu)

MPAKA SASA NAHITAJI NIWE NA MILLION 50 ILI KUENDELEZA SHIMO LANGU NA NIMETUMIA MILLION 28 KESHI NIKIWA NA HIYO HAMSINI NI MPAKA KWENYE UCHENJUAJI MSAADA PLEASE KWA ANAE JUA SHORT CUT.

FB_IMG_1697870043878.jpg
 
Dhahabu ni biashara kama biashara zingine tu, tatizo watu wanadhani ukiingia kwenye dhahabu sasa hivi unakuwa kama achimwene which is wrong.

Pia fanya slow slow usiwe na hasira nayo ,kuna mtu alitegemea kupata gram 500 ellution akaishia kupata gram 31 na nyuma ana madeni kibao

Pia ili usiumie kichwa usiendeshe biashara ya kuchimba dhahabu kwa kutumia pesa za kukopa.

Uchimbaji wa dhahabu ni biashara ya kubet mwanzo mwisho

1.Mawe unaachimba,-pesa inaenda
2.unasaga,- pesa inaenda
3.unaozesha- pesa inaenda
4.ellution( unavuna ulichopanda)- je kitarudisha fedha ulizotumia kwenye process 1,2,3 and 4? Na ukapata faida? Hapo ndo betting ilipo.
 
hamna betting kwenye dhahabu mkuu kila kitu kiko wazi kabisa, ni wewe tu kuamua kama unabet au hubet.
 
Watu wanatoa makafara ya wanyama,watu,mf. Mfanyakazi ,rafiki,na malaya wale wachunaji , jingine unaweza kuwa unanyota ya biashara hujafungua kwa kutoa fungu la kumi nakumuomba mola wako akupe ulinzi maana kila mtu anahitaji riziki, pia hujamwita mchungaji au shekhe abariki kazi ya mikono yako,wengine wanazingira na mambo ya giza
 
Naomba unitoe ushamba kidogo hapa
Mimi sio mkulima ila huwa nasubiri watu walime nikiwa mjini najaza store zangu halafu wakati wa mahitaji ya chakula nauza kwa faida kubwa
Sasa kwa mfano nikakupa hizo 50m badala ya kwenda kufukiwa na kifusi ukafungua duka lako hapo la kununua dhahabu taratibu haiwezekani

Nauliza tu maana nimeona wasomali wakimbizi Australia wameenda na kuanza kununua Opal stones kwa wenyeji huku wakiwaacha wao wahangaike ila waaminifu sana hao jamaa

Sasa turudi bongo je linawezekana?
 
Licha ya kuchimba sana dhahabu Chunya na kusekesa Lakini dhahabu imekuwa ni adhabu kwangu kwa kukaa kwangu kote polini nimeambulia kupata nyunga tu za point moja zimezidi sana point saba

Licha ya kupiga sana sululu huku gold detector yenye ukubwa wa 7000 hapa nazungumzia Gp7000 ile ya kisasa kabisa Lakini bado dhahabu ni ngumu kupatikana je dhahabu ni nini jibu= dhahabu ni adhabu.

Licha ya kupona kufukiwa ndani ya long base ukiwa na kitochi tu huko chini na uki risk maisha yako kwa hali ya juu na chini Lakini kupata dhahabu sio rahisi kama wana jf wanavyo jidai wana yajua vizuri machimbo ya dhahabu Lakini kiuhalisia hakuna wajualo

Mpaka mda huu ninao zungumza nilikuwa nipo sehemu zangu nina ofisi kubwa na maisha yanaenda akaja jamaa yangu mmoja wa mda kidogo ndani ya Toyota IST kali nikamuuliza vipi mbona adim na maisha umeyapatia sana akasema yeye yuko chunya machimbo mda wote na story yake ilinivutia na Mimi kuingia kwenye biashara ya dhahabu ooh hapa ndipo nilipo kosea duka mpaka sasa limefilisika

Nimebaki mabega tu na shimo ndio kwanza linaanza wachimbaji wananipigia simu wanataka unga wa kula kambini na Mimi HELA sina.

Hadithi za machimbo ya dhahabu ni tamu kusikiliza nimeweka hela Kumbe nimefukia mazima hata elusion ndio kwanza sijafika hali iko Hivi ama kweli biashara ya dhahabu kashamzoba au kanyampasila au kachumbagira (Rip marehemu mkandala rufufu)

MPAKA SASA NAHITAJI NIWE NA MILLION 50 ILI KUENDELEZA SHIMO LANGU NA NIMETUMIA MILLION 28 KESHI NIKIWA NA HIYO HAMSINI NI MPAKA KWENYE UCHENJUAJI MSAADA PLEASE KWA ANAE JUA SHORT CUT.

View attachment 2818592
Karibia kila anayefurahia ladha ya mafanikio, anajua pia ladha ya magumu, machungu, kukata tamaa, kuvunjwa moyo, kusalitiwa, kudhulumiwa, n.k. Kama wapo wasio na uzoefu wa hizo ladha, watakuwa wachache sana, au wameridhishwa tu mafanikio. Ni kama vile ni kamtihani wanakopitishwa kwanza wahusika kabla ya "kukabidhiwa" mafanikio.

Ukiweza, fungua na biashara nyingine huko huko machimboni ili isaidizane na kazi yako kuu kwa sasa ya uchimbaji dhahabu.
 
Ni kweli boss sikupingi
 
Naomba unitoe ushamba kidogo hapa
Mimi sio mkulima ila huwa nasubiri watu walime nikiwa mjini najaza store zangu halafu wakati wa mahitaji ya chakula nauza kwa faida kubwa
Sasa kwa mfano nikakupa hizo 50m badala ya kwenda kufukiwa na kifusi ukafungua duka lako hapo la kununua dhahabu taratibu haiwezekani

Nauliza tu maana nimeona wasomali wakimbizi Australia wameenda na kuanza kununua Opal stones kwa wenyeji huku wakiwaacha wao wahangaike ila waaminifu sana hao jamaa

Sasa turudi bongo je linawezekana?
Inawezekana mkuu ila mimi nilielekezwa kwenye mwamba ndio kuna hela kubwa hasa yale makinikia ukiyapeleka kuchenjua uhakika wa kukamua kilo tatu za dhahabu upo hapo ndio niliona utam uliko Kumbe kuna moto wake ni balaaa itoshe tu kusema wenzetu wazungu pale Katika mgodi wa bulyanhulu hela wamefukia sio za kitoto

Kwahiyo million 50 inawezekana kuwa middle broker yani kuwa mnunuzi wa kati tu.
 
Back
Top Bottom