Machali, Arfi kugombea ubunge kwa ACT-Wazalendo

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,305
6,503
Na Kulwa Mzee, Kigoma

Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amewatangaza wabunge Moses Machali ( NCCR-Mageuzi) na Saidi Arfi wa mpanda mjini ( CHADEMA) kuwa ni wagombea wa ubunge kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 25 mwaka huu.

Zitto aliwataja wabunge hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana mjini Kigoma, ambapo aliwatambulisha watangaza nia mbali mbali na kusema kuwa sasa chama hicho kumejipanga kupambana na makucha ya unyonyaji wa rasilimali za taifa kwa kuwa na kikosi cha wabunge wenye uchungu na nchi.

" Leo kuna watangaza nia mbali mbali ambacho ni kikosi chetu , pamoja na hili napenda kumtangaza Saidi Arfi kuwa mgombea wetu wa ACT-Wazalendo Mpanda mjini na Moses Machali, Kasulu mjini," alisema Zitto na kushangiliwa na umati wa wananchi katika mkutano huo.

Chanzo: Mtanzania, June 18, 2015
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
9,531
24,113
Sijaamina bado kama Moses Machali atamfata ZZK mpaka nimsikie mwenyewe.
Ila kwa hilo Zee la kifipa, limeshajichokea hata CCM anaweza kugombea.
 
ramadhani msengi

Senior Member
Apr 15, 2015
158
31
Siasa mchezo mchafu,,na sio hao tu,wapo kibao wajameni,cdm wasipoangalia dogo atakibomo chama hawataamini.ndo maana viongozi wote wa cdm wa ngazi za juu wapo site kuhakikisha wanachunga kondoo wao vema
 
tanga kwetu

JF-Expert Member
May 12, 2010
2,194
1,432
wamepitwa bila kupingwa chamani kwenye hayo majimbo? ina maana ni marufuku mwana-ACT kutangaza nia kwenye hayo majimbo? wanatangazwa kabla hawajahama vyama vyao? hawzi kuwatia matatani?
 
sifongo

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,896
5,297
Machali naomba usiache hii siku ikapita bila kuweka mambo sawa, Kafulila keshasawazisha khs ESCROW maana kijana Zitto haeleweki siku hz.
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
21,052
16,997
Alienda kuosha aibu za kuzomewa na kufurushwa Geita na Kagera...! Machali kanisikitisha kweli...!!
 
GreenCity

JF-Expert Member
May 28, 2012
5,604
4,246
wamepitwa bila kupingwa chamani kwenye hayo majimbo? ina maana ni marufuku mwana-ACT kutangaza nia kwenye hayo majimbo? wanatangazwa kabla hawajahama vyama vyao? hawzi kuwatia matatani?

Aisee, yaani mbunge wa chama kingine anatangazwa na mtu mwingine kugombea nafasi hiyo kupitia chama tofauti!!
 
Independent-Mind

JF-Expert Member
Mar 10, 2015
712
207
Hivi Zito huwa anatumia yale majani makali ? huchelewi kusikia hao watu kesho wanakanusha kwa nguvu zote

Mkuu you are too naive,Moses atakuja kukanusha leo hapa kesho anakuja tena anakuambia baada ya kufikiria sana nimeona hivi na vile kumbe ilishakuwa mipango ya kitambo wanacheza na akili za wananchi tu
"Msiwaamini wanasiasa"-ZZK
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
47,947
63,139
Machali naomba usiache hii siku ikapita bila kuweka mambo sawa, Kafulila keshasawazisha khs ESCROW maana kijana Zitto haeleweki siku hz.

Nyinyi mnaishi Dunia gani? Machali ameshakanusha leo asubuhi kwenye power breakfast clouds fm, amesema Zitto ni wa kupuuzwa.
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
47,947
63,139
Mkuu you are too naive,Moses atakuja kukanusha leo hapa kesho anakuja tena anakuambia baada ya kufikiria sana nimeona hivi na vile kumbe ilishakuwa mipango ya kitambo wanacheza na akili za wananchi tu
"Msiwaamini wanasiasa"-ZZK

Kwahiyo Zitto siyo mwanasiasa ndio maana unamwamini? Tutusa kweli wewe.
 
Msulibasi

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
5,638
6,471
machali atamfuata zzito hana ujanja ccm itapita kiulaini baada ya mtifuano wa ukawa na act
 
mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,305
6,503
machali atamfuata zzito hana ujanja ccm itapita kiulaini baada ya mtifuano wa ukawa na act

Umeshamjua Mufuruki? Baada ya kumjua umeamua nini? Naamini leo hutaangalia mdahalo....sory kwa kukutoa nje ya mada kidogo. Tukirudi kwenye mada Kigoma walishaikataa CCM Siku nyingi....Safari hii ni zamu ya Wazalendo
 
badoo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
510
245
Sijaamina bado kama Moses Machali atamfata ZZK mpaka nimsikie mwenyewe.
Ila kwa hilo Zee la kifipa, limeshajichokea hata CCM anaweza kugombea.

Mnashangaza kila atakaetoka chadema mtampa jina baya,lkn kwanini watoke?wewe mpiga debe nje hutoweza kuyajua ya ndani,chadema kina mambo mengi ya manyanyaso,naamini ht mbowe atoke leo chadema mtampa jina baya tu,ninachoamini kuwa wengi wa chadema watatoka tu japo kwa sasa wanafanya Siri lkn uwazi utabainika tu,hongereni kwa kuwa wazalendo.
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom