mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,306
- 6,514
Na Kulwa Mzee, Kigoma
Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amewatangaza wabunge Moses Machali ( NCCR-Mageuzi) na Saidi Arfi wa mpanda mjini ( CHADEMA) kuwa ni wagombea wa ubunge kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 25 mwaka huu.
Zitto aliwataja wabunge hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana mjini Kigoma, ambapo aliwatambulisha watangaza nia mbali mbali na kusema kuwa sasa chama hicho kumejipanga kupambana na makucha ya unyonyaji wa rasilimali za taifa kwa kuwa na kikosi cha wabunge wenye uchungu na nchi.
" Leo kuna watangaza nia mbali mbali ambacho ni kikosi chetu , pamoja na hili napenda kumtangaza Saidi Arfi kuwa mgombea wetu wa ACT-Wazalendo Mpanda mjini na Moses Machali, Kasulu mjini," alisema Zitto na kushangiliwa na umati wa wananchi katika mkutano huo.
Chanzo: Mtanzania, June 18, 2015