Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,372
Katika hali ya kushangaza,mbunge wa Kasulu,mh.Moses Machali, amemkabidhi spika,mh.Makinda,CD inayoonyesha namna waziri wa TAMISEMI,mama Hawa Ghasia,alivyokuwa akijibiwa vibaya na watendaji wa Halmashauri ya Kasulu.Mh. Machali alikabidhi CD hiyo jioni hii bungeni wakati akichangia taarifa ya kamati ya bunge ya bajeti iliyowasilishwa bungeni asubuhi ya leo.Mh.Machali alikabidhi CD hiyo kama ushahidi wa waziri husika kushindwa kutumia madaraka yake kuwawajibisha walio chini yake licha ya uzembe wa watendaji hao.Mh.Machali amefikia hatua ya kudai labda mh.waziri wa TAMISEMI huwa anapokea bahasha kutoka kwa watendaji hao na ndio maana anashindwa kuwachukulia hatua na mpaka kufikia hatua ya kumjibu waziri huyo ovyo kwenye vikao.
Mbunge mwingine nae akichangia taarifa hiyo aliishambulia TAMISEMI kwa kushindwa kumchukulua hatua mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga(kama sikosei) ambae anatuhumiwa kununua piki piki nne kwa jumla ya shilingi milioni 48 ikiwa na maana ya pikipiki moja kununuliwa kwa shilingi milioni 12.Kilichowakera wabunge ni uamuzi wa TAMISEMI kumuahimisha mkurugenzi huyo badala ya kumchukulia hatua za kinidhamu.
Katika hatua nyingine,mbinge wa Karatu mh.Natse ameiita wizara hiyo ya TAMISEMI kuwa ni "sleeping giant" kutokana na uzembe wa TAMISEMI na watendaji katika halmashauri mbali mbali.
Kwa kifupi,wabunge wengi wameonyesha kutoridhishwa na utendaji wa waziri wa TAMISEMI na watendaji wengine hasa wakurugenzi kwenye Halmashauri mbalimbali nchini.
MY TAKE:
Hivi katika ile oridha ya mawaziri mizigo mbona huyu wa TAMISEMI hayupo?
Nape na Kinana wako serious kweli na mawaziri wazembe?