Machali amkabidhi spika Makinda CD inayoonyesha Waziri Ghasia akijibiwa vibaya na watendaji!

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Katika hali ya kushangaza,mbunge wa Kasulu,mh.Moses Machali, amemkabidhi spika,mh.Makinda,CD inayoonyesha namna waziri wa TAMISEMI,mama Hawa Ghasia,alivyokuwa akijibiwa vibaya na watendaji wa Halmashauri ya Kasulu.Mh. Machali alikabidhi CD hiyo jioni hii bungeni wakati akichangia taarifa ya kamati ya bunge ya bajeti iliyowasilishwa bungeni asubuhi ya leo.Mh.Machali alikabidhi CD hiyo kama ushahidi wa waziri husika kushindwa kutumia madaraka yake kuwawajibisha walio chini yake licha ya uzembe wa watendaji hao.Mh.Machali amefikia hatua ya kudai labda mh.waziri wa TAMISEMI huwa anapokea bahasha kutoka kwa watendaji hao na ndio maana anashindwa kuwachukulia hatua na mpaka kufikia hatua ya kumjibu waziri huyo ovyo kwenye vikao.

Mbunge mwingine nae akichangia taarifa hiyo aliishambulia TAMISEMI kwa kushindwa kumchukulua hatua mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga(kama sikosei) ambae anatuhumiwa kununua piki piki nne kwa jumla ya shilingi milioni 48 ikiwa na maana ya pikipiki moja kununuliwa kwa shilingi milioni 12.Kilichowakera wabunge ni uamuzi wa TAMISEMI kumuahimisha mkurugenzi huyo badala ya kumchukulia hatua za kinidhamu.

Katika hatua nyingine,mbinge wa Karatu mh.Natse ameiita wizara hiyo ya TAMISEMI kuwa ni "sleeping giant" kutokana na uzembe wa TAMISEMI na watendaji katika halmashauri mbali mbali.

Kwa kifupi,wabunge wengi wameonyesha kutoridhishwa na utendaji wa waziri wa TAMISEMI na watendaji wengine hasa wakurugenzi kwenye Halmashauri mbalimbali nchini.

MY TAKE:
Hivi katika ile oridha ya mawaziri mizigo mbona huyu wa TAMISEMI hayupo?

Nape na Kinana wako serious kweli na mawaziri wazembe?
 
mmmh kali? Nitarudi akili yote ipo kigoma na wahujumu wa ziara kubwa ya rais dr slaa.
 
Huyu mama Ghasia mwenyewe ana majibu machafu sana. Wacha naye aipatepate.
 
mmmh kali? Nitarudi akili yote ipo kigoma na wahujumu wa ziara kubwa ya rais dr slaa.

Rais? rais wa wapi? hivi nyinyi bavichwa mnaona urais ni kitu rahisi rahisi saaaana hata mtu ambaye ameshindwa kuitawala ndoa yake kisha kumchukua kimada na kuzini nae basi anaweza kuwa rais? bado mnahitaji ukombozi wa kiakili kwanza ili mjitambue na pia mfahamu kwamba Padri Silaha kamwe hawezi kuwa rais wa nchi hii.
 
Wasameheni.Daima ccma haiwez fanya maamuz magumu. Kiufupi ccm ni janga.
 
NIPISHE BHANA, Unajua unachoandika sio but endelea na personal attack unazani utafanikiwa kila mtu mzima ufanya maambo manne yote au moja wapo
  • kuvuta sigara (uvutaji)
  • kula sanaaaa chakula
  • kunywa pombe na vilevi
  • kufanya mapenzi plus kuchukua wake za watu n.k
niambie kunakitu kati ya haya hufanyi wewe mburula, kuna mapadre wanakula ngada sanaa, na mashekhe wanakula sana chairfire lakin waumini wao wanasikiliza sera zao sio vitendo vyao.... jenga hoja achana na personal attack, ukishindwa NIPISHE

Rais? rais wa wapi? hivi nyinyi bavichwa mnaona urais ni kitu rahisi rahisi saaaana hata mtu ambaye ameshindwa kuitawala ndoa yake kisha kumchukua kimada na kuzini nae basi anaweza kuwa rais? bado mnahitaji ukombozi wa kiakili kwanza ili mjitambue na pia mfahamu kwamba Padri Silaha kamwe hawezi kuwa rais wa nchi hii.
 
yote 9 kumi hizi piki piki 4 kwa milioni 48., kila 1 milion12 nadhan ni bora sana kwa bei hizo wangenitafuta mimi nikawauzia magari mazuri tu shilini milion 6 hadi nane kwa gari moja na milioni 4 zingebaki kila kwenye milioni 12..,
 
Back
Top Bottom