Amoxlin
JF-Expert Member
- May 30, 2016
- 3,782
- 4,108
Amani iwe nanyi ndg zangu.
Leo nimeona nizungumzie kidogo hawa wakubwa zetu makazini kwani asilimia kubwa walioajiriwa wanakumbana na changamoto nyingi na wengine wanaenda kukabiliana nao kesho.
Binafsi nilishafanya kazi na mabosi watatu tofauti na nilikumbana na yafuatayo.
-Bosi wa kwanza alikuwa ni jinsia ya kiume (kama mimi), hatukufahamiana kabla ila alikuwa ni mchapakazi sana japo alikuwa ni mlevi wa sketi, hakuna ilokatiza mbele yake akaiacha.
Aliwajali watumishi wake wote bila kubagua jinsia na alipenda kuwawezesha wanapokwama sambamba na kuchukua mawazo yao na kuyafanyia kazi. Nilimpenda sana na kila mtumishi alimpenda ila kizuri hakidumu, aliaga dunia angali kijana.
-Bosi wa pili alikuwa mwanaume pia, alikuwa ni mtu wa kusimamia maadili mwanzo mwisho. Huyu alikuwa hataki umbea wowote, ukienda kumsema mtu anamwita uongee yote mbele yake. Alikuwa na wapelelezi wake kila kona na alifanya kazi kitaalamu zaidi.
-Bosi wa tatu alikuwa mwanamke mtu mzima kidogo. Huyu alifanya niione dunia chungu, alikua haambiliki wala hashauriki. Baadhi ya watumishi waliamua kuacha kazi bila kufukuzwa tokana na tabia yake.
Analojua yeye ndo hilohilo hataki ushauri wowote. Ukimshauri jambo anageuza maneno kwamba umemwambia yeye hajui kitu. Likitokea tatizo lolote hataki kuambiwa muhusika ni yupi, anayemhisi yeye ndie huyohuyo hata kama hahusiki.
Alipenda wafanyakazi vilaza ambao watatii amri zote hata za kijinga. Vilaza nao walikuwa wapambe wake ili wasifukuzwe kazi.
Nadhani wengi wamekumbana na maswahibu mengi makazini.
Tupeane uzoefu kidogo ili tusife moyo.