Maboresho jukwaa la kazi na tenda

Paul S.S

JF-Expert Member
Aug 27, 2009
6,402
3,242
Wadau mwaka mpya umeenza nami napenda kutoa maoni machache kuhusu jukwaa hili.
Zamani jukwaa hili lilikuwa ni sehemu nzuri sana ya kupata habari kuhusu nafasi mbali mbali za kazi, ilifikia hatua huna haja ya kununua magazeti iliupate kusoma nafasi za kazi kwani wadau walizibandika fasta kila watakapo ziona.
Lakini sasa hali imekuwa tofauti kabisa hatubandiki tena nafasi isipokuwa tunaomba nafasi,
Utakuta mtu anaanzisha post inasema "Nafasi ya kazi" ukufungua ndani unakuta yeye ndio anaomba atafutiwe kazi, na hii imelifanya jukwaa kuwa la blah blah na kupoteza ile credibility yake kama source ya kupata matangazo ya kazi.
Sipingi watu kuomba wasaidiwe kazi ila wito wangu kwenu ni kuwa iwapo kila mdau ataona nafasi sehemu na kujitahidi kuibandika humu kama ilivyokuwa awali naamini wengi watafaidika kwani nafasi zitakuwa nyingi kuliko ilivyo sasa.
Ntakuwa mchoyo wa fadhila kama sita lishukuru jukwaa hili kusaidia kumpatia ajira mdogo wangu, hivyo natambua umuhimu wake.
Tubadilike
 
Ahsante sana mdau kwa kuliona tatizo hili "kubwa" labda nami kwa nyongeza ningeomba pia na majina ya wanaoitwa kwenye interviews mbalimbali yabandikwe ili kuenda sambamba na lengo hili la kubandika matangazo ya kazi. Zamani nilipokuwa nafuta ajira ilkuwa ni rahisi kwangu kupata taarifa za nafasi za kazi lakini baada ya kutuma maombi nilikuwa nakuna kichwa wapi nipate fedha ya kununua magazeti kuangalia ya waliobahatika kuitwa kwenye interview. MUHIMU SANA WADAU.
Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom