Mabondo ni zao gani la samaki aina ya sangara?

Mabondo ni zao gani la samaki aina ya sangara?

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,280
Tarehe 13/3/2018 nilisikiliza taarifa ya habari saa mbili usiku kutoka startv.

Habari ilisema kwamba wafanyabiashara wanalalamika kwa kunyanyaswa wakikutwa na mabondo na hutozwa faini ya sh milioni mia moja.

Habari ikaendelea kwamba kilo moja ya mabondo huuzwa sh laki moja kwa kilo.

Nikawa najiuliza: Hayo mazao ya sangara yaitwayo mabondo yanayouzwa kilo sh laki moja ni nini hasa? Na je matumizi yake ni kwa viwanda au chakula kwa binadamu?

Kwa anayejua naomba anieleze mabondo ni nini hasa na kazi yake ni ipi?
 
Bado nashindwa kupata maana hasa ya mabondo
Tuanze hivi;
Samaki walio wengi kama sio wote kwenye ogani zao za ndani wana organi maalum kwa ajili ya kuhifadhi hewa. Mfuko huu huitwa mfuko wa hewa (Air bladder) na huu ndo kwa maeneo ya kanda ya ziwa huitwa bondo.

Mfuko huu hutofautiana kwa ukubwa na ugumu wa kiwambo chake kutokana na aina ya samaki. Mfano sato (tilapia ) wana bondo dogo sana na lina kiwambo chepesi/laini.

Sangara kwa upande wake ana bondo kubwa na kiwambo chake ni kigumu. Ukubwa na ugumu wa bondo lake huendana na umri/ukubwa wa samaki. Samaki mkubwa ana bondo kubwa na kinyume chake.

Bondo linatumika kutengeneza malighafi za kiwandani mfano plastic, viatu, mikanda N.K.

Nadhani walau nimejitahidi kueleza kidogo, japo waweza uliza ambacho hujaelewa.
 
Vizuri,kazi yake hilo kwa sangara sababu yeye hupenda kina kirefu ni kumfanya kuelea na kuzama majini kiurahisi,akitaka kuja juu anajaza upepo hvyo anakua mwepesi akitaka kwenda chini anatoa upepo anakua mzito.
Mchangiaji mmoja kasema inatengenezewa nyuzi za kushonea wagonjwa ila sidhani kama wanatengenezea yeboyebo asee isingekua na bei ghali hvyo.
 
Hahahaha mtakutana wapo sasa,kanda ya ziwa ni nadra sana kuuziwa sangara akiwa na bondo lake,ukishatoa pesa tu wanampasua na kutoa bondo.
Dah! kumbe siku ukikutana na sangara wazima ni kuwatoboa na kuondoka na bondo nyama ni kuwaachia wanaotaka shibe
 
ukinunua sangara ambaye hajatolewa hicho kiungo,ukimpasua kifuani utapata jitu kama puto lina asili ya ngozi jeupe limejaa upepo,hilo ndo bondo sio jina rasmi ila limetokana na misemo ya kabila la wajita
Nakubali , Libhondo lya Ichengu Wasu.
Ni Dude fulan hivi jeupe likiwa Bichi , likikauka linachange kuwa Brown na linatoa mafuta Sana , Lina matumizi Sana na Huuzwa Bei juu.
 
Back
Top Bottom