Tuanze hivi;
Samaki walio wengi kama sio wote kwenye ogani zao za ndani wana organi maalum kwa ajili ya kuhifadhi hewa. Mfuko huu huitwa mfuko wa hewa (Air bladder) na huu ndo kwa maeneo ya kanda ya ziwa huitwa bondo.
Mfuko huu hutofautiana kwa ukubwa na ugumu wa kiwambo chake kutokana na aina ya samaki. Mfano sato (tilapia ) wana bondo dogo sana na lina kiwambo chepesi/laini.
Sangara kwa upande wake ana bondo kubwa na kiwambo chake ni kigumu. Ukubwa na ugumu wa bondo lake huendana na umri/ukubwa wa samaki. Samaki mkubwa ana bondo kubwa na kinyume chake.
Bondo linatumika kutengeneza malighafi za kiwandani mfano plastic, viatu, mikanda N.K.
Nadhani walau nimejitahidi kueleza kidogo, japo waweza uliza ambacho hujaelewa.