Mabondia wapokezana kilinda ulimi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabondia wapokezana kilinda ulimi

Discussion in 'Sports' started by Mpogoro, Jun 16, 2010.

 1. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu zetu wabeba box wa Diaspora...please assist...haya mambo si sawa jamani!
  Mabondia wapokezana kilinda ulimi
  Thursday, 13 May 2010 22:04 0diggsdigg

  Imani Makongoro
  'UKISTAJABU ya Musa utaona ya filauni' ndio iliyokuwa kwenye kambi ya timu ya ya taifa ya ngumi za ridhaa ambako mabondia wake walilazimika kubadilisha kilinda ulimi wakati wa mazoezi ya kujiandaa na michuano ya jumuia ya Madola.

  Kambi ya mabondia hao inatarajia kuanza mazoezi Jumatatu kwenye Uwanja wa Ndani wa taifa jijini Dar es Salaam, huku Shirikisho la mchezo huo nchini (BFT) ikikabiliwa na ukata.

  Ukata huo ulisababisha mabondia hao kukosa vifaa muhimu vya mazoezi kama vikinga ulimi ambavyo kwa kawaida bondia uweka mdomoni kabla ya kupigana ili kumlinda na tatizo la kujing'ata ulimi alipokuwa ulingoni.

  Lakini kutokana na ukata mkubwa iliyoikumba kambi hiyo mabondia watatu walilazimika kutumia kilinda ulimi kimoja kwa kupokeza kila wanaposhuka ulingoni.

  Pembeni ya ulingo kuliwekwa maji kwa ajili ya kusuuzia kilinda ulimi hicho kabla ya kubadilishana mara baada ya mabondia waliokuwa ulingoni kushuka ili kuwapa nafasi wengine kupimana ubavu.

  Mbali na kukosa vifaa hivyo pia dawa, maji, Vikinga vichwa na Gloves kwa mabondia hao ilikuwa ni tatizo kubwa kiasi cha kufanya mazoezi bila kuwa na vifaa hivyo.

  Hivi karibuni mabondia hao walialikwa kushiriki mashindano ya kupimana ubavu kati ya wenzao wa nchini Burundi, lakini ilishindikana baada ya BFT kukosa shilingi milioni 7 kwa ajili ya kusafirisha mabondia nane na matumizi mengine nchini humo.

  Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga, aliiambia Mwananchi hivi karibuni kuwa wanaendelea na mchakato wa kutafuta wadhamini ili kuweza kuisaidia timu hiyo ambayo inakabiliwa na ukata.

  Alisema kuwa ili kuwa na timu imara basi jitihada zinahitajika ili kuweza kulifanikisha hilo na wanaimani wakipata mfadhili hata mmoja kikosi cha mabondia hao kitafanya maajabu kimataifa.


  "Ingawa tunakabiliwa na ukata, lakini mabondia wetu hawakati tamaa kwa kweli wanajitahidi endapo tukipata mfadhili ambaye atatusaidi tunaimani tutafika mbali na tutarejesha heshima ya taifa katika mchezo huo Kimataifa" alisema Makore.

  Ukata huo umesababisha mabondia hao kabla ya kupewa likizo kuweka kambi ya wazi na kushindwa kuweka kambi ya kudumu wakati wakijiandaa kushiriki katika michezo ya Jumuiya ya Madola mwezi Oktoba mjini New Dehli, India.
   
 2. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kama mabondia wamekubali wenyewe kulana denda kwa kupitia the so-called Kilinda ulimi utawasaidiaje? Kwanini wao wanakubali? Ni dhiki, ujinga au ubabe?
   
 3. senator

  senator JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Duh Hii kwelim kiboko...Yaani ni sawa na kushare naniliii..Hili swala naona ni aibu kubwa kwa chama cha Ngumi.hizo gumshed sidhani kama zinabei labda kama hazipatikani nchini! Hiki chama hakina hata source of income, i mean sponsors etc nakumbuka zaman Boxing ilikuwa na wadhamini wengi tu wakiwemo TBL ila kwa sasa nadhan hakuna Uongozi thabiti wakuendesha chama.Na hivi kesi ya mwenyekiti wao imefikia wapi yule kinara wa mambo ya Unga( alhaj Shaban Mintanga)?
   
 4. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Too bad. unajua watanzania tunatia aibu saaaana. Singida walikua watu wanaazimana kondom na baadae zinafuliwa
   
 5. senator

  senator JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Hata Kigoma iliwahi kutokea na Kipindi hicho huyu Mama Terry alikuwa kwenye mapambano ya hilo goma letu, akadai watu huko KG wanaazimana vifanyio kikitumika kinakwenda kufuliwa then mwingine anachukua kwenye kupasha nacho!! hatari kweli!
  Bongo Kuna michezo wasipoangalia itakufa kabisa kama Mieleka yakina pawa chaka,mtonga na wengineo ,ilikuwa inatupa raha sana zaman
   
 6. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Da! Hii nchi hii!
  Kila kitu tuna shea! Hakuna cha kutumia peke yako, yaani ni kila kitu.
   
Loading...