Mabomu yarindima uchaguzi wa serikali za mitaa,mtaa wa Bondeni kata ya Masekelo mkoani Shinyanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabomu yarindima uchaguzi wa serikali za mitaa,mtaa wa Bondeni kata ya Masekelo mkoani Shinyanga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sammosses, Jun 25, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ni saa tano na robo usiku matokeo ya uchaguzi wa serikali za mtaa yanatangazwa kwa kumtangaza mshindi wa kiti cha mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa bondeni kupitia CCM na kusindikizwa na mabomu yaliyorindima.Sababu za kurindima mabomu hayo mpaka sasa hazijulikani,hali inayopelekea kuchafua jina la chama tawala kwa kutoweza kutangazwa mgombea wake pasi na mabomu.

  Wananchi wa kata hiyo wameshangazwa na tukio hilo la mabomu kiasi cha kupelekea kupoteza imani na CCM kwa kutumia vyombo vya dola vibaya kwa maslahi ya binafsi na kusahau kuwa chombo hiki ni mali ya umma na kina wajibu wa kulinda mali na raia wake.
  ]

  Iko wapi demokrasia ya kweli ikiwa hata chaguzi za serikali za mitaa zinagubikwa na ukiukwaji mbaya wa vyombo vya dola.Hali hii imeleta picha mbaya kwa uchaguzi mkuu ujao.Nini tufanye kuinusuru hali hii,kama wananchi watachoka na kuamua kujibu mapigo na kutokukubali kuonewa?
   
 2. S

  STIDE JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona husemi sababu ya mabomu kupigwa. Ni mabomu ya machozi au mabomu ya kudungua ndege? Uchaguzi ulikuwa wa mtaa lakini wananchi wa kata wameshangaa! Tuambie basi ilikuwaje hadi polisi, kama ni polisi, wafike huko na mabomu manake si rahisi rahisi kuwa na mabomu.
   
 4. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,296
  Likes Received: 1,216
  Trophy Points: 280
  uchakachuaji dot com,ulitegemea kusiwe na mabomu?
   
 5. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mabomu yaliyopigwa ni mabomu ya machozi.Kwanza muda wa kuhesabu kura ulichukua muda mrefu kiasi uvumilivu uliwashinda wananchi na kuimba,tunataka matokeo.Dalili za polisi kuchafua hali ya hewa zilijionyesha mapema mara baada ya magari yaliyobeba askari polisi kuingia kwa mbwembwe.Kama matokeo tu ya serikali za mitaa yanachukua masaa yote hayo je uchaguzi mkuu utachukua muda gani?

  Pia ni kwanini basi kila panapotokea mgombea kupitia CCM ameshinda askari polisi hujiandaa kwa mapambano kabla ya matokeo husika kutangazwa,hali inayopeleka wapiga kura kutokuwa na imani na wasimamizi na serikali.
   
Loading...