Mabomu yarindima Karatu kisa Rose Mhando

Mabomu yarindima Karatu kisa Rose Mhando

...Labda wamekutana. Muuza Cheni bandia na Muuza Noti bandia. Kuna Akiba ya Manerno kuwa labda hiyo Mil 3 ilikuwa ni ya Utangulizi lakini angeongezwa Mil 2 mathalani kabla hajapanda Jukwaani, Promota akashangaa shangaa na Rose akaamua kuingia Mitini kwa sababu anawajua mapromota wa Bongo kuwa Ukitegemea kulipwa BAADA ya Onyesho, Umeula wa chuya!

Lakini pia, Kwani hiz fedha wanakabidhiana Kienyeji bila Mkataba? Kama kuna mkataba si lazima pia kuwe na Kipengele kinachoweka Wazi Nini kifanyike pale Show isipofanyika kutokana na Msanii anapoingia Mitini?

Kama ni kweli Rose Mhando ameishaingia Mitini mara kadhaa pamoja na kulipwa pesa, nini kinachowazuia Mapromota/Wachungaji kumfikisha kwenye Vyombo vya Sheria kudai Chao?

Je hii haitoi picha kwamba ni kama nilivyosema mwanzo kuwa inawezekana kuwa Rose/Msanii yoyote kichwa hukataa kupanda Jukwaani mpaka amaliziwe hela aliyoahidiwa kupewa KABLA hajapandaa Jukwaani?? Nadhani hata Francis Cheka alifanya hivi kwenye game lake la Mwisho na ilibidi Jamaa wajikamue kisawasawa ili kumpa hela yake ndio akapanda Jukwaani kupambana na Kinyozi Mpiganaji wa Marekani!

Anyway, yetu macho na Masikio, Tusikilizie kitakachoendelea maana Njia ya Muongo/Mwizi/Tapeli ni Fupi....!
:A S 39:
 
kweli kabisa, halafu huyu dada Rose bangi kabisa ndio tabia yake ya kupokea hela na kuingia mitini

Sitaki kuwa masemaji wa Rose Mhando
Naamini ana watu wanaoweza kufanya hivyo

Lakini nalazimika kukuuliza haya yafuatayo
Una ushahidi wa Rose kuvuta bangi?
Una ushahidi wa Rose kuwa na tabia hii?
Je unakijua kilichofanya Rose asitokee hapo karatu?

Halafu hivi nyie watu mnaopinga watu kulipia kiingilio mna akili kweli?
Hela za kurekodia anazitoa wapi?
Hela za kujikimu anazitoa wapi?

Mbona kanisani huwa mnatoa sadaka bila kujiuliza matumizi yake?
Mnajidai mnajua sana kuwahukumu wenzenu lakini kusimamia mahali mnapoabudu tu pamewashinda!

Kwenye suala hili la Rose Mhando lina mambo mengi sana
Kuna tabia wanaykuwa nayo watu ya kutangaza kuwa mtu fulani anakuja kumbe hata mawasiliano nae hawajafanya
Hii ni tabia mbaya sana ya kuwapaka matope watu!

Mkija kugundua kuwa Rose Mhando hakuwa na makosa sijui mtakuja hapa kumtaka radhi?
 
Rose mhando wa kipindi kile sio wa sasa, ukijua mambo yake ya ndani utachoka. ki ukweli sikilizeni nyimbo zake mengine mwachieni Mungu. kuna albamu yake mpya iko njiani kuna wimbo unaitwa KUNG' UTA. hili la kutokufika kwenye tamasha wala sishangai.kuimba nyimbo za injili ni tofauti na kuishi kama biblia inavyotaka, leo hii hata dimond plutnum anaweza akaimba nyimbo ya gospel kali na akabamba mbaya,ila kuishi hayo maisha ya Kiimani/ kiroho ni tofauti na uimbaji. kuna mmoja mwimbaji mmoja wa gospel maarufu anakaa tabata ni mchapa bia mzuri tu. na kuna mmoja wa kiume anakula kijiti cha bob,na hawezi ingia studio au stajini bila kijiti. msishangae ila ndio hali halisi ktk tasnia ya wasanii wa nyimbo za injili,ushaambiwa wasaanii,kama wa bongo fleva wanavyokula ngada.
shetani jana na leo hajafa bado yupi kazini

Well said broda,

Chukua tano
 
Inasikitisha sana mtumishi wa mungu anapogeuka tapeli!
 
wachungaji wauza unga,wauaji (kibwetele),walawiti(vatican),wachawi (kakobe) matapeli (mchungaji wa arusha). mpaka sister rose nae?????????!!!!!!!!!
 
Msimshambulie Rose Mhando, shida inakuwa kwa wale wachungaji wanaoandaa matamasha maeneo ya mikoani huwa ni matapeli. Utakuta walishakubaliana na Rose masuala Fulani ya maandalizi na pesa sasa kama ikifika mahali mwandaaji anazingua basi inakuwa issue kama hii. Ukimpata Rose nina hakika atasema ukwel wa kilichotokea. Huwa hawa promoters na wachungaji fake wanaishi kwa migogongo ya waimbaji sana na wana wanyonya vilivyo.
 
hii ni mbaya sana katika tasnia ya nyimbo za injili unless kuna sababu za msingi
 
Dini tena! Hiyo ni burudani sawa na fm academia.

haaaa....haaa.....haaa ! watu walikuwa wamejitayaisha kubebwa na kubembelezwa na Yesu !
huku wengine wakisubiri utamu wake Yesu !
 
Rose mhando wa kipindi kile sio wa sasa, ukijua mambo yake ya ndani utachoka. ki ukweli sikilizeni nyimbo zake mengine mwachieni Mungu. kuna albamu yake mpya iko njiani kuna wimbo unaitwa KUNG' UTA. hili la kutokufika kwenye tamasha wala sishangai.kuimba nyimbo za injili ni tofauti na kuishi kama biblia inavyotaka, leo hii hata dimond plutnum anaweza akaimba nyimbo ya gospel kali na akabamba mbaya,ila kuishi hayo maisha ya Kiimani/ kiroho ni tofauti na uimbaji. kuna mmoja mwimbaji mmoja wa gospel maarufu anakaa tabata ni mchapa bia mzuri tu. na kuna mmoja wa kiume anakula kijiti cha bob,na hawezi ingia studio au stajini bila kijiti. msishangae ila ndio hali halisi ktk tasnia ya wasanii wa nyimbo za injili,ushaambiwa wasaanii,kama wa bongo fleva wanavyokula ngada.
shetani jana na leo hajafa bado yupi kazini

Sahihisho siyo Rose .... aliyeimba Kung'uta

Ushahidi nilio nao huu hapa.

Sarah K - Kung'uta (OFFICIAL VIDEO) - YouTube
 
watanzania tunajua kulalamika na kulaumu bila hata kutafuta ukweli. je tumejaribu kupata ukweli juu ya kilichomfanya asifike tamashani?
 
Karatu ushamba umezidi. ndio maana Dr. Slaa yuko vile alivyo...

Ushamba wao uko wap hapo? Nani mshamba kati yao na wewe unae andika post za kishamba kishamba? Peleka ushamba wako huko,hauna jipya zaidi ya ushamba ushamba ulio kujaa,Mshamba wewe
 
Back
Top Bottom