Mabomu yaendelea Kurindima Zanzibar! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabomu yaendelea Kurindima Zanzibar!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ni Mimi Msiogope, Jul 20, 2012.

 1. N

  Ni Mimi Msiogope JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 352
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taharuki msibani!
  Baada ya kikundi cha Uamsho kuanza pilika pilika na Jeshi la polisi pale saa 11 jioni, Hadi sasa bado maeneo mengi visiwani Zanzibar hali imeendelea kuwa Tete kwa kuwa watu wengi wamejitokeza na kuanza kuwasha matairi na kufunga Barabara maeneo ya Mkunguni,Darajani na maeneo mengine!..
  Taarifa ni kwamba sasa madai yamegeuka na Watu wanasema Wanataka Uhuru wa Zanzibar!..
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hii nimesikia ITV jamaa wanataka zanzibar yao
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  msiba unahusiana vipi na kuzama kwa meli?
  Udhaifu aliousema mnyika ndio huu!intelijensia haikujua jambo hili?
  Tuombe mungu makanisa yasichomwe.
   
 4. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Kama ni zanzibar yao si wapewe waendelee kufa na meli zao?
   
 5. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  haba na haba hujaza kibaba.serikali dhaifu matunda yake ndiyo haya.wapeni uhuru wao lakini uhuru kamili nikuifahamu kweli.bila kweli hata wakipewa uhuru wakibinadamu wataanzisha madai mengine mara sharia, kadhi,ijumaa wapumzike.yetu macho na masikio na Mungu aturehemu maana misiba na majanga yamekuwa mengi yametulemea
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nawapa hongera waZanzibari wanaosimamia kidete kuidai nchi yao bila ya kuona haya wala kuogopa ogopa ,litakuchwa tu !
   
 7. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kudai uhuru huku tukiomboleza?
   
 8. N

  Ni Mimi Msiogope JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 352
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Binafsi yangu naona Logic kwenye madai yao!
  Badala ya kuruhusiwa kuukubali au kuukataa Muungano tunaambiwa "Tuboreshe" muungano? Kuna haja gani ya kumrekebisha mke ambaye uliozeshwa na baba yako wakati hazai? Mke mzuri ni yule wa kuozeshwa au uliyemtongoza mwenyewe?...

  Wapewe Zanzibar yao ili nasi 'Waoga' tupate Tanganyika yetu kwenye Silver plate.
   
 9. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #9
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Vipi wana andamana kuelekea Ikuru ya Zanzibar? Mapinduzi ya kule Mali yalianza hivi hivi,
   
 10. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hebu endeeni kuchangia kwanza badae ntahitimisha.
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hawadi Uhuru bali wanachokidai ni kuondoa dhulma za kudumazwa na mipango sikivu ya CCM ,mipango isiyo na tija ya maendeleo si kwa Mzanzibari hata Mtanganyika ,UCCM ulioota mizizi na mashina ndio unaotukandamiza ,watu wanakufa kila leo ,syria watu wanakufa kwa mamia kudai kumuondosha dikteta na chama chake.Huu si wakati wa kuiachia Zanzibar bali hata huko Tanganyika mnatakiwa muamke.

  Kama huko uarabuni kulitokea Spring naona East Afrika kunahitaji summer,kuwaondoa vikaragozi wezi mafisadi watesaji ili tupate kusonga mbele.
   
 12. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Ni haki ya watu wa nchi zote mbili kufanya REFERENDUM kuamua uwepo wa muungano. Hicho ndio kipimo pekee cha UHURU wetu. Hii ndoa ya pete haina maisha.
   
 13. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  mbona lisu alijibiwa na viongozi wao bungeni kuwa zanzibar haikuwahi kutawaliwa sasa wanataka uhuru toka wapi?

  waulizeni wachina walichofanywa Tiananmem square 1989

  [​IMG][​IMG]
  [​IMG][​IMG]
   
 14. N

  Ni Mimi Msiogope JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 352
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo letu huku Bara ni waoga!
  Wengine tuko busy na kuganga njaa zetu
  hakuna aliye tayari kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine..
   
 15. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hakuna mwenye wakati wa kura ya maoni ,kwani muungano huu ulipigiwa kura ya maoni ,baba yenu wa taifa alisema wazanzibari wakiuchoka muungano wapewe nchi yao ,dalili zote zinaonyesha wamechauchoka sasa kunasubiriwa kitu gani ?
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Jul 20, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapo umesema kuwa bado Tanganyika ni waoga ,ila kwa mikiki hii ya CCM na CDM naona karibu woga utawaondoka ,wacha hizi risasi na mabomu ya polisi yazoeleke tu.Mjeshi kama hajazoea sauti za risasi na mabomu lazima atakimbia vitani ,lakini akizoea hupenda kila wakati awepo vitani na waZanzibari wameanza kuzoea tena wanazoea kwa kasi ya ajabu na huu ndio muamsho katika sura mpya ya waZanzibari wa kizazi cha leo.
   
 17. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #17
  Jul 20, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Muungano ulisha vunjika kwenye mioyo ya wananchi ya wa zanzibar kinachofanyika sasa hivi ni kuendelea kuulazimisha uzidi kustawi kwenye mioyo ya viongozi ambao kwa kiasi kikubwa wao ndio wanaonekana wana maslahi nao.
   
 18. N

  Ni Mimi Msiogope JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 352
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Exactlly!
  Hakuna marefu yasiyo na ncha!
  Tena ukiona ngoma inalia sana ujue inakaribia kupasuka!
  Serikali hapa ilipo imeshafutwa kwenye mioyo ya Watanzania wengi yenyewe bado haijashtuka tu!.. Usalama wa Taifa na majeshi baadhi yao ni vijana ambao hawapendi uhuni huu uendelee.. Time will tell.
   
 19. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #19
  Jul 20, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  mbona ni swala la wao kutuandikia talaka na wala si kuchoma barabara/kitanda
   
 20. N

  Ni Mimi Msiogope JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 352
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na maslahi ya baadhi ya Wazanzibari ni machache na ya kijinga kuliko uhai na thamani ya Uzanzibari wao.. Sema tu hawajajitambua
   
Loading...