Mabomu Gongolamboto

Mutta

Senior Member
Mar 24, 2011
101
11
Hivi juzi yalitokea mafuriko jijini Dar na Serikali imejitahidi kuwatafutia viwanja MABWEPANDE ili wanaokaa mabondeni wakae sehemu salama.Lakini watu waliobomokewa nyumba wakati wa MABOMU YA GONGOLAMBOTO mpaka sasa viwanja havijapatikana na nyumba hawajajengewa kama Serikali ilivyoahidi ikidai eneo lililo patikana lina mgogoro(je mabwepande haikuwepo?).Kibaya zaidi hata wale waliosababishiwa VILEMA serikali haijawafidia kama ilivyoahidi wengine wanaishi maisha ya shida kwani Walivunjika MIKONO,MIGUU ,MIGONGO nk. hawana mahitaji yao ya kila siku.Serikali yetu inashangaza sana hasa inapochelewesha kulipa watu wakati pesa nyingi ilichangwa na taasisi mbali mbali.Wana jf tufanyeje ili serikali iwalipe watu wa GONGOLAMBOTO?
 
Watakwambia pesa zimetumika kwenye maadhimisho ya 'miaka hamsini ya uhuru' wao!! On a serious note...... serikali ya jakaya ina mchezo mchafu sana, mpaka leo kuna wananchi hawana makazi na serikali imetulia tu ilhali ni viongozi hao hao na uzembe wao ndo wamesababisha maafa ambayo ni dhahiri kabisa yangeepukika!! Mpaka wananchi watakapoelewa maana ya people's power ndipo watakapoiwajibisha vilivo!!!
 
Watu wa Goms wanateseka sana.wamekaa kwenye mahema karibu miezi 11.Serikali ya JK haieleweki bana.Fikiria mtu kavunjika mguu kabisa amewekewa vyuma hawezi kufanya kazi,angepewa chake angejipanga.Sasa anatamani kufa
 
Back
Top Bottom