Tarehe 16/02/2012 Mwaka Mmoja Baada ya Milipuko ya Mabomu Gongolamboto!!

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,564
7,970
Mwaka mmoja baada ya milipuko ya mabomu katika kambi ya jeshi gongolamboto umetimia leo huku wananchi walioathirika na milipuko hiyo wakiwa bado wanateseka.

Serikali kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa wa dar es salaam Said Meck Sadiq iliahidi kuwajengea nyumba waathirika eneo la kinyerezi lakini hadi leo hii hakuna kilichofanyika.

Kama serikali imeshindwa kuwajengea nyumba waathirika kama ilivyoahidi, kwanini isiwalipe fedha wajenge wenyewe? Au fedha zimeliwa kama tulivyosikia sh.1 bilioni zimefujwa ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa?
 
Mkuu kumbe hamjajengewa nyumba bado? Mbona mkuu aliagiza nyumba zijengwe na SUMA JKT kama sikosei ina maana agizo halijatekelezwa badala yake limetelekezwa? Yaani afadhali hat wa mafuriko manake mambo yao naona yanaenda tambarare. Fanyeni mchakato mkamuone mkuu mmkumbushe.
 
Nchi hii tukipata watu walio makini tutasonga mbele.
Mimi kwa kweli Pinda na ofiisi yake wamenikera.
Hivi kweli zaid Bil 1.5 hazijulikani zimetumikaje?
Watu wa kilosa na Goms hawana makazi yet!
 
Tatizo tulilo nalo ni hili viongozi kuahidi kufanya kitu fulani halafu hawatimizi
Ahadi zao .. maneno matupu ..

Labda waweke sheria fulani hivi ..
Unaahidi , tekeleza na usipotekeleza
Uchukuliwe hatua fulani za kisheria au
Ulipe faini..

Kama viongozi wetu wote wangekuwa
Wanatilia maanani ahadi zao tungefika
Mbali sana .... ... .... .... .....
 
Nchi hii tukipata watu walio makini tutasonga mbele.
Mimi kwa kweli Pinda na ofiisi yake wamenikera.
Hivi kweli zaid Bil 1.5 hazijulikani zimetumikaje?
Watu wa kilosa na Goms hawana makazi yet!

Uko sahihi spencer January nlikuwa kilosa na kwa macho yangu nimeshuhudia wahanga wa mafuriko wakiendelea kuishi kwenye mabanda ya mabati walojengewa baada ya makazi yao kuharibiwa. Hii nchi inachanganya sana kichwa..ahadi hazitikelezwi watz tunaishi ktk mazingira magumu kana kwamba tumelaaniwa, tumebaki kusema tunamwachia Mungu kana kwamba Mungu atashuka kutupa mabadiliko ya uongozi yatakoyoleta walau unafuu wa maisha. Kichwa kinauma na logoff.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom