Mabomba kwa ajili ya Upanuzi wa Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kutoka Bomba Kuu kwenda Igunga

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,905
945
đź“Ť Igunga, Tabora

IGUNGA: TUTAFIKA MWAKA 2025 TUKIWA TUMEMTUA MAMA NDOO KICHWANI

Mabomba kwa ajili ya Upanuzi wa Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kutoka Bomba Kuu kwenda Vijiji na Vitongoji vya Kata za Mwamashiga, Mbutu, Isakamaliwa, Kining'inila, Mwamakona, Igurubi na Kinungu. Mradi wenye thamani ya Shilingi Bilioni Ishirini (Tshs 20,000,000,000/=) yamefika 'site'.

Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa anaendelea kutoa shukrani za Wananchi kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza ndoto ya kumtua "Mama Ndoo Kichwani" kwa vitendo. Mradi utanufaisha maelfu ya Wakazi wa Jimbo la Igunga na viunga vyake.

Aidha Mheshimiwa Ngassa (MB) anatoa shukrani kwa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Tabora na Wilaya ya Igunga kwa usimamizi wa Mradi.

"KAZI NA MAENDELEO"

Imetolewa na:
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Igunga
13 Mei, 2023
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-05-13 at 10.59.22.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-13 at 10.59.22.jpeg
    83.1 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2023-05-13 at 10.59.21.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-13 at 10.59.21.jpeg
    59.3 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2023-05-13 at 10.59.23.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-13 at 10.59.23.jpeg
    96.4 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2023-05-13 at 10.59.23(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-13 at 10.59.23(1).jpeg
    102.8 KB · Views: 8
Back
Top Bottom