Muwe mnapost vitu unique vinavyocreate value, wabongo wengi wanaigana kuweka post za scholarship Tena mbaya zaidi wanatumia spinner kama word ai wanajiona wajanja eti content ziwe unique bila kujali kwamba kunakuwa na error za grammer kibao zinazofanya post iwe takataka.
Ukitaka kuendana sawa na hawa wenzetu fanya blog iwe ya kiwango cha juu, yani haiingii akilini mtu hata blog yake haina pages muhimu kama home, contact us, privacy, n.k content za Ku spin kwa word ai au copy paste, mtu kuweka mitangazo iliyofurika website utadhani AdSense ya baba yake, n.k.
Google wapo strict sana saizi, jumamosi kuna panga Kali sana lilipita wabongo wengi sana account zao zililiwa, Google wapo smart siku hizi, yani ukipost mipicha ya uncut uiwekee link kwenye blogspot ili mtu akiminya hio picha wazamie kwenye blog yako imekula kwako, wana robots zinafatilia source ya traffic hata kama ulifupisha link kwa twitter watajua tu.
Kwa hapa bongo wengi wanapenda sana hizi shortcuts za kupost uncut ili wapate traffic ila kwa jinsi google wanavyoboresha mitambo yao hizi mbinu za kupata pagel views kimazabe mazabe zitalalisha watu njaa kwa kulimwa disabled mpaka akili zikae sawa.