Jinsi ya kutengeneza pesa kwa mara ya kwanza online: Here is everything you need to know

GLOBAL CITIZEN

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
767
1,655
Salute bosses!

Kwanza kabisa naomba nianze kwakusema kumradhi nimechelewa kuanzisha thread hii kama nilivyoombwa na baadhi ya watu hapa JF.

Nilikuwa busy na majukumu sasa nikasema nikitulia nitapata wasaa wakufafanua kwa urefu kila kitu unachopaswa kufahamu kuhusu kutengeneza pesa mtandaoni.

Hapa nitazungumzia kuanzia

1• Freelencing

2• Dropshipping

3• Blogging

4 • Affiliate Marketing

5 • Paid survey

6 • Mwisho tutaangalia websites zinazolipa kwa kuangalia matangazo (Ads).

Sitazungumzia Forex kwasababu imeshajadiliwa hapa sana.

Kwahiyo hizo njia sita (6) ndiyo unatakiwa uzifahamu ili usibabaishwe tena kufahamu njia yakutengeneza pesa online.

Pia niseme wakati naelezea nitajitahidi niguse points zote muhimu kuhusu njia nilizotaja hapo juu ili wewe mwenyewe ufanye maamuzi yako kwakuangalia wapi panakufaa.

Are you ready for this?

Ok, sasa tuanze.

Kwanza kabisa niseme tu sasa hivi kila kitu kinahamia mtandaoni.

Biashara, mashirika, watu binafsi kila mmoja anatafuta namna yakujitengenezea "empire" mtandaoni.

Na hapa lengo ni kutengeneza $$$$ money.

Kama haufahamu namna ya kujiingizia kipato mtandaoni soon you will disappear.

Utashindwa kucompete kwasababu utakuwa nyuma ya teknolojia.

Lakini hili si swala lakuhofia.

Hapa swala lakuhofia ni iwapo utajifunza kutake advantage internet imetoa ama lah.

Sasa baada ya kusema hayo naomba nianze kukupa darasa kwa kila njia niliyotaja hapo juu.

Maelezo haya yatakufanya uwe informed na kamwe hutobabaishwa kufahamu kipi kinawezekana na kipi hakiwezekani kuhusu kutengeneza pesa mtandaoni.

1 • Freelancing.

Kuhusu Freelancing naomba niwe straight forward kwakusema hii ndiyo njia "sustainable" zaidi kupiga pesa mtandaoni.

Lakini haiishii hapo.

Ukiniuliza freelancers wangapi unaowafahamu wanatengeneza pesa kupitia freelancing nitakujibu nawafahamu wanatengeneza $500 - $1200 a month na pia nawafahamu wanatengeneza $0 a month.

Guess what?

Freelancer wengi hususani from Tz hawana right mindset.

Wengi wanaingia kwenye Freelance platforms with wrong reasons.

Unakuta mtu ameambiwa unaweza tengeneza pesa ndefu kwakuwa transcriber/translator basi huyo mbio anaenda kujiunga with expectations atatengeneza pesa.

No way.

Siku utakapowekeza kwenye skills zako kwanza na kujua mbinu za kuuza ndiyo utakapoweza kutengeneza pesa.

Buyers kwenye Freelance platforms wanafahamu you are not capable to do the work kwa kuangalia tu profile yako.

Na hapa si kwasababu wewe ni biginner, nop. Sababu kuu ni kwamba you are disorganized.

Siyo tu hauwezi kuandaa profile yako vizuri. Pia hujui namna yakuuza ujuzi wako.

You need to learn how to sell.

Period.

JE, NITAFANYAJE KUPATA MTEJA KWA MARA YA KWANZA KAMA FREELANCER?

Ni rahisi but you need to think out side the box.

Kwanza naomba nianze kwa kuuliza swali.

Je, unafikiri ni kitu gani kinamfanya mteja amchague freelancer mwingine na kukuacha wewe?

Jibu ni rahisi.

Good reviews kwenye profile yako.

Freelancer wengi wanaoanza ili kupata trust ya buyers inabidi watafute mtu/watu nakuwaomba kununua service zao na kisha kuwapa review nzuri.

Hapa unatakiwa uwe smart.

Unaweza muomba rafiki au ndugu ajiunge kwenye platform unayotumia halafu anunue huduma yako na kukupa reviews nzuri.

See how it works?

Ukitumia njia ya kawaida kusubiri mteja asiyekufahamu anunue huduma yako wakati huna review hata moja you will likely end up wasting time.

Sikufundishi "umafia".

Hizi ndiyo mbinu zenyewe za ku-survive as newbie.

Tuendelee...

Je, majukwaa gani ni sahihi kujiunga kama freelancer?

Well, hapa nitapendekeza platforms tatu. Pia kaa mkao wa kula nipo jikoni kuandaa freelance platform ya Kiswahili ambayo itakuwa mahususi kwa wana JF na watanzania. Na mimi binafsi nitakupatia darasa binafsi kukujenga as a freelancer.

Nitumie email through the address makingmoneyonlinetz@gmail.com

I will respond your mail as fas as possible.

Sasa tungalie majukwaa ya Freelancing.

a • UpWork.com

- hawa wapo vizuri. Job offer ya kwanza kabisa (transcription/translation) nilipatia hapa baada ya kuhangaika katika majukwaa tofauti kwasababu sikuwanafahamu mbinu. Kwenye UpWork nimefanya kazi za watanzania watatu (3). Hehee it was amazing kuona waTz wenzangu nakunipa job offer.

b • Freelance.com

- ninayo account but sijaelekeza nguvu nyingi huko. I have few project I'm working on kwahiyo time yangu inakuwa limited. Ila kwa ufupi ni jukwaa zuri na kongwe. You can try them.

c • Fiverr.com

- nani hapendi Fiverr? Kwenye hili jukwaa unachofanya ni kupost a gig. Gig ni service (huduma) unayouza. Na kila gig inathamani ya $5.

- haiishii hapo. Fiverr wanakuruhusu kupost gigs zenye thamani zaidi kwa mfano $50, $100, $120....ukikidhi vigezo.

Hayo ndiyo majukwaa unavyoweza kujiunga as freelancer.

Unachotakiwa ni kuwa strategic. Fuata tricks nilizokuambia and you will be surprised jinsi ilivyo rahisi.

2 • Dropshipping.

- what should I say about this?

- fuata thread hii mada imezungumziwa kwa kina

Drop shipping : Maswali na majibu 10 kila beginner lazima ajiulize - JamiiForums

3 • Blogging (Kuanzisha blog)

- kamwe usi-underestimate uwezo wa blog kukutengenezea pesa. Binafsi najiona mjinga kwanini sijaanza mapema.

Hebu soma haya maelezo chini ufahamu je kiasi gani unaweza tengeneza.

Haya maelezo ni jibu nililolitoa kwa mwanaJF aliyekuwa anahitaji kuanzisha blog.

"Mkuu kwanza niseme tu kuwa na blog ni njia nzuri yakutengeneza passive income.

Unaweza kutengeneza hadi $500 - $1000 a month.

Kwa kifupi ukiwa na strategy nzuri hiko kiasi ni rahisi kufikia.

Sasa twende taratibu.

Ili blog yako iingize hela kwanza inabidi upate AdSense account toka Google.

AdSense kwa lugha rahisi maana yake umeruhusu google waweke matangazo ya biashara kwenye blog yako.

Na ili google wakupatie AdSense inabidi blog yako iwe imekidhi vigezo.

• haina makala/post zilizo tumika sehemu nyingine.

• umeandika makala zakutosha kwenye blog yako. At least 30 posts.

• makala unazopost kwenye blog yako zina-solve matatizo ya visitors.

Ukiweza kutimiza hivyo vigezo basi unaweza ku-apply for AdSense na ukapata kirahisi.

Naomba niende ndani zaidi.

Baada ya kupata AdSense na matangazo kuonekana kwenye blog yako inabidi uelewe je AdSense itakulipa kiasi gani kwa kila visitor?

Kufahamu hili kwa njia rahisi let's do the math.

Let's assume blog yako inapata viewers 1000 kwa siku.

Katika hao viewers 1000 wanao-click matangazo kwenye blog yako ni 200

Pia lets assume kila click inathamani ya $0.10.

Kwahiyo 200 * 0.10

= $20

Hiyo $20 ndiyo unatengeneza kwa hao 1000 viewers.

Kwahiyo kama unauwezo wakupata viewers 30000 kwa mwezi maana yake umetengeneza $600

Lakini kama nilivyosema awali you need guidance"

4 • Affiliate Marketing.

- kwanza kabisa naomba niseme maana ya affiliate Marketing. Hii ni aina ya biashara unayofanya kwa kutafuta wateja na kuwashawishi wanunue bidhaa za kampuni fulani kwa mfano health care products kisha wewe kupata commission.

Kwenye affiliate Marketing utafanikiwa sana iwapo unamiliki blog. Hii inakuwa rahisi kuandika reviews kuhusu product unazopendekeza kwenye blog yako wasomaji watashawishika kununua.

Kingine kuhusu affiliate Marketing nashauri u-promote product zenye commission nzuri. Promote product za makampuni zinazotoa at least 30%.

Kwa mfano ukimshawishi mteja kununua product ya $100 hapo una $30 kama commission.

Kama utashawishi watu 10 tu kwa mwezi basi unaondoka na $300.

Ukibadilisha hii kwa hela yetu ya madafu ni amount nzuri hiyo.

JE, NITAWEZAJE KUWA AFFILIATE MARKETER?

Ni rahisi.

Unachotakiwa kufanya nenda clickbank.

Click bank ni market place ambapo baada ya kujiunga utaweza kuchagua product unayotaka kupromote kama affiliate Marketer.

Kwahiyo kama unataka kuwa affiliate Marketer just go there and create account.

Je, kiasi gani naweza kutengeneza kama affiliate Marketer?

Kujibu swali hili inategemea na idadi ya watu unaoweza kuwafikia na kununua bidhaa kupitia speacial link ambayo ndiyo affiliate link yako.

Kwahiyo hapa unaona iwapo unamiliki blog ni rahisi zaidi kwasababu utaweza kuwashawishi wasomaji.

5 • Paid Survey

- kuhusu Paid Surveys nakushauri uwekeze muda wako kwenye mambo ya maana. Paid Survey wanalipa hela kidogo sana (peanuts). Kwamfano jukwaa kama PaidViewPoint wanalipa $0.03 kwa survey. Kwahiyo unaona kamwe hautoweza kutengeneza chochote.

6 • Website zinazolipa kwa kutazama matangazo (Paid Per Click)

- hii nayo si nzuri sana. Kwamfano NeoBux wanakupa $0.001 kwa kila tangazo utakalo-click. Kwa siku wanaweza kukutumia matangazo hadi 20.

Japo kuna members wanadai wanaweza kutengeneza $30 in a daily basis lakini hii si kwa kitegemea matangazo wanayo-click. Kifupi kuna mbinu hapa na si lengo langu kuelezea leo kwasababu makala itakuwa ndefu sana. Labda naweza kuelezea katika post nyingine.

NENO LA MWISHO.

Nisema tu ili uweze kutengeneza pesa mtandaoni in a constancy manner inabidi ufikirie kujifunza ujuzi unaouzika na ulio kwenye trend.

Jifunze skills hizi na unatengeneza pesa mtandaoni.

1 • SEO

2 • Copy Writing

3 • Content Writing

4 • UX design

5 • Programming

6 • Web development

7 • Transcription & Translation etc.

Kumbuka kujifunza haya yote huitaji muda mrefu. Baadhi ya skills hapo unaweza kujifunza kwa wiki si zaidi ya mbili.

Baada ya kuandika haya yote sasa naomba nimalizie kwakukupata challenge ya kutumiza hayo.

Iwapo unahitaji kujifunza zaidi usisite nitumie email kwenda makingmoneyonlinetz@gmail.com

Asante.
 
Mi nauliza km kiingereza chako ni cha kuunga unga kuna possibility yoyote ya kutengeneza pesa online?
Inategemea ni wateja wapi unataka kuwafikia.

Kama hujui Kiingereza na ukaenda kujiunga na freelance platforms za kizungu basi utakuwa vigumu kutengeneza pesa.

Ndiyo maana nikasema soon nitakuja na freelance platform ya kiswahili kwaajili ya waTz.

Karibu sana mkuu na wewe utengeneze pesa mtandaoni si tu kutumia bundle bure.
 
Ni kipi wewe unafanya kwa sasa ambacho kinakupa pesa. kwa experience niliyonayo ya online business, ni VERY COMPLEX TO MAKE MONEY ONLINE, kwa vitu ambavyo umevi list hapo juu. Sio rahisi kiekweli... By experience
Unashindwa kutengeneza pesa mtandaoni kwasababu zifuatazo

1 • hauna ujuzi unauozika.

2 • haujui mbinu za kuuza.

Period.

Making money online is not hard.

You need to change your mindset about money first.

Yani hadi hapo tu uliposema kutengeneza pesa mtandaoni ni "complicated" tayari umeshajipunguzia maksi.

Mkuu inatakiwa uwe problem solver ili utengeneze pesa mtandaoni.

Ni rahisi ukiwa na right mindset.
 
Kwenye blog hapo nw day kuna ushindani ile mbaya na changamoto watu wanalipia SEO hadi dola 300 kwa mwezi ili post iweze kuoneka kwenye page ya kwanza sasa kwa masikini ni changamoto
 
Kwenye blog hapo nw day kuna ushindani ile mbaya na changamoto watu wanalipia SEO hadi dola 300 kwa mwezi ili post iweze kuoneka kwenye page ya kwanza sasa kwa masikini ni changamoto
Yes kama huna maarifa yakuweza kuattract visitors kwenye blog yako and you have some money to burn basi ni sawa tu kulipa digital marketers wakusaidie.

Kingine unachotakiwa ufahamu ili blog yako iweze ku-rank vizuri kwenye google ni lazima unandike quality content zinazotatua changamoto za watu. Period.

Search Engine Optimization ni mchanganyiko wa mambo mengi.

Binafsi mimi ni content marketer na ninaweza sana tu kuandaa post inayoweza ku-resonate kwa kuwasaidia katika changamoto fulani.

Kitu wanachokosea bloggers wadogo ni kwamba wanadhani kuandika ni kuandika tu.

Nop.......you need to be strategic in your writing.

Kama unamiliki blog ninaweza kukusaidia kuandaa quality content zitakazo saidia posts zipate rank nzuri google.

Hii ni elimu.
 
Unashindwa kutengeneza pesa mtandaoni kwasababu zifuatazo

1 • hauna ujuzi unauozika.

2 • haujui mbinu za kuuza.

Period.

Making money online is not hard.

You need to change your mindset about money first.

Yani hadi hapo tu uliposema kutengeneza pesa mtandaoni ni "complicated" tayari umeshajipunguzia maksi.

Mkuu inatakiwa uwe problem solver ili utengeneze pesa mtandaoni.

Ni rahisi ukiwa na right mindset.
Hujanijibu swali langu. Unadili na kip kati hivyo ulivyo list ambacho kinakupa pesa kwa sasa?. Then explain how you make money online...

Kuna yupo dar niliunganishwa nae yeye kwa madai yake ni mtaalamu wa SEO. Unauwezo wa kuongeza traffic kwenye blog au website. Nikamwambia nakuja dar tuongee nataka nikupe pesa wewe ufanye tuwe tunagawana % kwa mwezi. Na aliniambia kwa mwezi inawezekana kupata $2000 hadi $3000 . Nikaenda dar kuonana na mtaalamu. Nikamwambia piga budget yako ya kila kitu kinachotakiwa mm natoa pesa , hakujua kama najua haya mambo , mm nikawa najiuliza anatumia plugins gani kwenye wordpress ambacho mm sizjui. Jamaa hakagoma list plugins na bei zake . Akasema ataandika in general budget ya vitu vyote. Nikamuuliza nioneshe kazi uliyowai kuifanya ambayo imeshakupa pesa. Uwezi amain jamaa akaanza ubabaishaji, nikashangaa mtaalam wa SEO hana ata blog aliyofanya. Tulivyoachana kwaajiri mtaalam andike budget uwez amin kesho yake namtafuta anitumie document ya budget kwa email jamaa hapokei simu.

Na wewe pia kama ni mtaalamu wa hivyo ulivyolist hapo juu , mm naomba unipe estimation ya mwezi ni invest kwako tuwe tunagawana % kwa mwezi. Na kama upo dar mm nakuja tunaongea na kusainisha mkataba na unanipa budget yako unaanza kazi.


Kama unaweza vitu na hauna pesa tangaza watu wana invest. Kinacho mata ni return kila mwezi na kutoa estimation ya mwezi.
 
Hujanijibu swali langu. Unadili na kip kati hivyo ulivyo list ambacho kinakupa pesa kwa sasa?. Then explain how you make money online...

Kuna yupo dar niliunganishwa nae yeye kwa madai yake ni mtaalamu wa SEO. Unauwezo wa kuongeza traffic kwenye blog au website. Nikamwambia nakuja dar tuongee nataka nikupe pesa wewe ufanye tuwe tunagawana % kwa mwezi. Na aliniambia kwa mwezi inawezekana kupata $2000 hadi $3000 . Nikaenda dar kuonana na mtaalamu. Nikamwambia pita budget yako ya kila kitu kinachotakiwa mm natoa poa , hakujua kama najua haya mambo , mm nikawa najiuliza anatumia plugins gani kwenye wordpress ambacho mm sizjui. Jamaa hakagoma list plugins na bei zake . Akasema ataandika in general budget ya vitu vyote. Nikamuuliza nioneshe kazi uliyowai kuifanya ambayo imeshakupa pesa. Uwezi amain jamaa akaanza ubabaishaji, nikashangaa mtaalam wa SEO hana ata blog aliyofanya. Tulioachana kwaajiri mtaalam andike budget uwez amin kesho yake namtafuta anitumie document ya budget kwa email jamaa hapokei simu.

Na wewe pia kama ni mtaalamu wa hivyo ulivyolist hapo juu , mm naomba unipe estimation ya mwezi ni invest kwako tuwe tunagawana % kwa mwezi. Na kama upo dar mm nakuja tunaongea na kusainisha mkataba na unanipa budget yako unaanza kazi.


Kama unaweza vitu na hauna pesa tangaza watu wana invest. Kinacho mata ni return kila mwezi na kutoa estimation ya mwezi.
You are asking all the wrong questions.

Unaniuliza je mimi natengeneza vipi hela mtandaoni?

Hapo inaonyesha hauna idea jinsi pesa inavyotengenezwa mtandaoni.

Nikwambie tu, SEO wala haiwezi kukusaidia kitu kwenye blog yako kama hauandiki au hauuzi information au product yenye value.

Period.

Kuhusu mimi natengenezaje pesa, well, hadi sasa hivi hapa nimeshaingiza some cash tena hapa JF achilia mbali kazi zangu kwenye Freelance sites.

I'm not here to brag

Guess what?

I know how to sell.

Ngoja nikwambie kitu.

Watu wengi mnaoanzisha blog kwaajili yakutengeneza pesa most likely you won't make any.

You are focusing on wrong things.

Pia I'm not here to teach you everything for free.

What I'm giving here is basic information that may help you to see things in different perspective.

Kama unahitaji kufahamu zaidi you need to pay.

It is simple as that. Dont complicate your mind.
 
Usikae kimya kama una skills za kuingiza pesa ila wewe hupa pesa kulikamilisha. Usiofie kuibiwa ideas au skills . Ni kuwa smart kwenye kila kitu unachofanya ukienda kwa investors. Tatizo leo watz ni wabinafsi, na ndo maana wengi wetu ni maskini, tuna skills lakin hazitusaidii.

"Change your mind Change your Life"
 
Upo sawa. Kama unahitaji kufanya kazi please send me email kwenye address niliyotoa japo juu tujadili hili kwa kina.

Mimi siyo mbabaishaji. Strickly business.
Usikae kimya kama una skills za kuingiza pesa ila wewe hupa pesa kulikamilisha. Usiofie kuibiwa ideas au skills . Ni kuwa smart kwenye kila kitu unachofanya ukienda kwa investors. Tatizo leo watz ni wabinafsi, na ndo maana wengi wetu ni maskini, tuna skills lakin hazitusaidii.

"Change your mind Change your Life"
 
You are asking all the wrong questions.

Unaniuliza je mimi natengeneza vipi hela mtandaoni?

Hapo inaonyesha hauna idea jinsi pesa inavyotengenezwa mtandaoni.

Nikwambie tu, SEO wala haiwezi kukusaidia kitu kwenye blog yako kama hauandiki au hauuzi information au product yenye value.

Period.

Kuhusu mimi natengenezaje pesa, well, hadi sasa hivi hapa nimeshaingiza some cash tena hapa JF achilia mbali kazi zangu kwenye Freelance sites.

I'm not here to brag

Guess what?

I know how to sell.

Ngoja nikwambie kitu.

Watu wengi mnaoanzisha blog kwaajili yakutengeneza pesa most likely you won't make any.

You are focusing on wrong things.

Pia I'm not here to teach you everything for free.

What I'm giving here is basic information that may help you to see things in different perspective.

Kama unahitaji kufahamu zaidi you need to pay.

It is simple as that. Dont complicate your mind.

Uwezi kumfundisha mtu kama hajajua uwezo wako kufanya online business au namna ya kuingiza pesa online. Hapa ndipo watu wengi wanaonekana scam. Kama forex ilivyo ingiliwa na sasa imeshakuwa biashara ya matapeli. Ni kazi sana kupata pesa kwa kuwafundisha watu ambao hawajui uzoefu wako wa online business. Watz wengi sio wa kweli, ni wazuri kuongea lakin utelezaji wa maneno yao ni SUFURIA. Na wengi wanaingia kwenye mtego huu kwasababu wana njaa na pesa. Nilikwisha sema kipind kile cha ontario kwamba hizi BLUE wanazopost JF ni kuwatamanisha watu waamini Forex ni rahisi na waingie kwenye mtego na ndivyo ilivyokuwa hapo baadae.

Scam nowadays wamekuwa wengi sana, ambao wanatafuta watu kwa nguvu kuwatapeli kwa maneno mazuri ya kuwashawishi. Ukitaka kupata pesa kwa watz kwa sasa, wafundishe basic kwanza na waone wanapata $$ chache kabla hujaanza kuwa charge pesa. Ni rahis sana watz kukupa pesa kwa kuwa wameona kwenye baisic, hapa ndipo watu wengi wanaonekana scam kwa kutanguliza pesa mbele. Jaribu kutafuta mtu yoyote ambaye ni pro utaona anavyofanya kwa audience wake before kuanza kulipia huduma mfano mzuri BRIAN TRACY.
 
Uwezi kumfundisha mtu kama hajajua uwezo wako kufanya online business au namna ya kuingiza pesa online. Hapa ndipo watu wengi wanaonekana scam. Kama forex ilivyo ingiliwa na sasa imeshakuwa biashara ya matapeli. Ni kazi sana kupata pesa kwa kuwafundisha watu ambao hawajui uzoefu wako wa online business. Watz wengi sio wa kweli, ni wazuri kuongea lakin utelezaji wa maneno yao ni SUFURIA. Na wengi wanaingia kwenye mtego huu kwasababu wana njaa na pesa. Nilikwisha sema kipind kile cha ontario kwamba hizi BLUE wanazopost JF ni kuwatamanisha watu waamini Forex ni rahisi na waingie kwenye mtego na ndivyo ilivyokuwa hapo baadae.

Scam nowadays wamekuwa wengi sana, ambao wanafuta watu kwa nguvu kuwatapeli kwa maneno mazuri ya kuwashawishi. Ukitaka kupata pesa kwa watz kwa sasa, wafundishe basic kwanza na waone wanapata $$ chache kabla hujaanza kuwa charge pesa. Ni rahis sana watz kukupa pesa kwa kuwa wameona kwenye baisic, hapa ndipo watu wengi wanaonekana scam kwa kutanguliza pesa mbele. Jaribu kutafuta mtu yoyote ambaye ni pro utaona anavyofanya kwa audience wake before kuanza kulipia huduma mfano mzuri BRIAN TRACY.
No one wants to steal your money.

Kuhusu kujifunza basics ndiyo maana uzi huu upo hapa.

Nimeona watu ukiwaambia kutengeneza pesa mtandaoni wanadhani ni kitu complicated sana.

Unajua kwanini?

Kwasababu haujawahi kutengeneza pesa mtandaoni kwahiyo you have little to no idea at all.

Kifupi tu nikwambie there no limits how much you can make online.

Kama nilivyosema awali njia ya kwanza kabisa ili utengeneze pesa mtandaoni you need to acquire skills watu watakayokuwa tayari kulipia.

Baada ya hapo unatakiwa ujifunze kuwa seller.

Ukifanikisha hayo you are in the business.

Period.
 
No one wants to steal your money.

Kuhusu kujifunza basics ndiyo maana uzi huu upo hapa.

Nimeona watu ukiwaambia kutengeneza pesa mtandaoni wanadhani ni kitu complicated sana.

Unajua kwanini?

Kwasababu haujawahi kutengeneza pesa mtandaoni kwahiyo you have little to no idea at all.

Kifupi tu nikwambie there no limits how much you can make online.

Kama nilivyosema awali njia ya kwanza kabisa ili utengeneze pesa mtandaoni you need to acquire skills watu watakayokuwa tayari kulipia.

Baada ya hapo unatakiwa ujifunze kuwa seller.

Ukifanikisha hayo you are in the business.

Period.

Ukitaka kufanikiwa zaidi katika maisha jaribu kusaidia watu kutimiza malengo yao. Mfano mzuri AMAZON, FACEBOOK, JF, ALL SOCIAL MEDIA. ATA MM nipo kwenye changamoto ya kutafuta kitu ambacho kitasaidia watu watimize malengo yao. Embu anza kufiria kwanzia hapo namna ya kuwasaidia watz kutimiza malengo yao. Ukiweza ilo umejiweka sehem nzuri katika maisha.
 
Back
Top Bottom