chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 21,885
- 29,675
Habari zenu wanaMMU,.
Hii imetokea juzi wakati narejea kutoka mjini kujipatia matumizi yangu kuelekea mwisho wa wiki,.
Baada ya kujipatia mahitaji yangu nilielekea kituo cha basi na kupata siti ya nyuma kwenye basi ambapo kwenye siti hiyo alikuwa amekaa kijana wa kiume ambaye simfahamu akiwa amekaa na binti ambaye huwa namuonaga mtaani nikimaanisha siyo mgeni machoni pangu na bila shaka mimi siyo mgeni machoni pake maana anauza duka la dawa ( pharmacy) na mimi mara nyingine huwa naenda kununua panadol kwake, nikajichukulia siti na kukaa baada ya kuwasalimia ambapo wote walionekana kuwa bize sana na mazungumzo yao na sina hakika kama waliniitikia maana walishazama maongezini utadhani wao peke yao ndiyo waliokuwa kwenye basi!!
Back to the topic,.
Muda ulivyosonga huku mimi nikaendelea na mambo yangu Jf kidume akaagiza soda mbili za chupa (take away) , yaani ya kwake na ya kale kabinti!! Soda zikaletwa na jamaa kwa vile aliagiza mbili ile moja akamkabidhi bibie,. Bibie akaikataa ile soda akasema hakuwa na shida ya soda hivo haihitaji,. Jamaa akambembeleza sana yule binti maana ilishafunguliwa ile soda hivyo jamaa asingeweza kuirejesha kwa muuzaji labda anywe zote mbili mwenyewe,.. Kadri muda ulivyokwenda bibie alishikilia msimamo wake mpaka tunaondoka stendi ndipo jamaa ikambidi aichukue ile soda anywe zote mwenyewe!!
Sasa kidume akabadilisha mada na kuanza kumtongoza yule binti hadharani nikimaanisha tuliokuwa tumekaa siti ya nyuma tulikuwa tukisikia kila neno lililokuwa likitoka kwa yule mwanaume, mrejesho kutoka kwa binti ndiyo ulikuwa kero zaidi maana alikuwa anaropoka kabisa kiasi kwamba abiria wote walikuwa wakimgeukia yule binti,. Hadi nashuka kwenye lile basi hali ilikuwa tete sana maana abiria walikuwa wamekereka sana na kelele za yule binti!!
Ombi:
Mabinti mkitongozwa kuweni wapole basi, haina haja ya kukera wengine au kutoa sauti zenye kukera watu wengine ukizingatia watu wa pembeni hawatakiwi kujua nini kinachoendelea kati yenu wawili!!