Mabinti wa kitanga

kwenzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Posts
669
Reaction score
667
Nilikuwa naskia skia tu mabinti wa kitanga ni noma kwenye mapenzi nikafikir story tu za hapa na pale kumbe kuna ka ukweli.

Nimepata kazi huku na nilicho kugundua kutoka kwa hawa mabinti wa kitanga ni iki;

1: wanajua kupenda
Utapendwa wewe mpaka uone kero kataa Kula ndio utaona moto wake.

2: waaminifu sana kwenye ndoa zao.
3:wanajua kuchakalika kuzitafuta hela kwa nguvu zote ,hasa uku nilipo usambaan yan wanawake wanapiga kazi kwa bidii kuliko wanaume walio fika huku wanaweza kuwa mashaidi.

4: wanawivu kupindukia
Hapa siwezi hata mueleza

5: wanaheshima kubwa kwa waume zao sema tu wanaume wenyewe ndio wanazingua

6:wanajua kukufanya ujiskia fahari kuwa mume na kwao ni marufuku kumpazia sauti mume wake

Kwa wale wasio oa kama kuna binti wa kitanga karibu yako fanya fasta muweke kwapan hauto jutia nakupa guarantee miaka 100 .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja wazoefu wengine nao waje watoe maoni yao
 
Upo sahihi mkuu...ila wanawake wanatofautiana...mabinti wa kitanga sio wote ambao wana sifa hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JF huwa najifunza mambo mengi hili jambo limezungumziwa sana humu, mwingine katoa ushuhuda jana, ngoja nitajaribu na mimi nitareta mrejesho.

_ where ever you are remember me_
 
Tanga kunani jamani.? Hii thread ya tatu naona inaelezea mabinti wa kitanga. Na kuna muhenga mmoja alishawahi kuja na thread akaelezea jinsi alivyo telekeza familia yake Moshi akazamia Tanga. Mimi nasemaje sitaki kusimuliwa tu nitahitaji nishuhudie mwenyewe.
 
Mkuu naomba uniassist kwa mmoja, sijawahi kubahatika kuwa nao..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…