Mabina wa CCM auawa wananchi Mwanza

SAKATABU

Member
Feb 28, 2013
84
95
Hali hiyo, wanaielezea ilisababisha kuanguka chini na wakazidi kumshambulia hadi wakahakikisha amekufa huku vijana wake wa kazi wakiingia mitini.

Ofisa wa Polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa yeye si msemaji wa jeshi hilo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Taarifa hiyo ya Polisi ilieleza kwamba, mgogoro huo ulizuka baada ya wananchi hao kumtuhumu Mabina kuwa ana mpango wa kuuza eneo lao la kijiji
kwa mwekezaji.

Ni mapema mno kuelezea tukio hili kwa undani hasa ikizingatiwa kuwa mimi siyo msemaji. Subiri msemaji wa jeshi atawapa taarifa kwa undani, alisema ofisa huyo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Christopher Fuime alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema wanaendelea kufanya uchunguzi.

Tulipata taarifa ya kuwepo kwa tukio hilo na kutuma vijana wetu kwendakutuliza vurugu, alisema Fuime. Alisema Mabina hakuwa na dhamira ya kuua, ila alijaribu kufyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatuliza na ndipo ilipompata mmoja wao.

By Miguel Suleyman, Mwananchi
Imewekwa Monday, December 16
2013 at 08:05
 

MOORIINGEE

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
381
195
jamani semeni jambazi,au jangili sugu ameuawa mwanza.

tangu miaka ya 1990 alikuwa anatuhumiwa kwa ujambazi na inasemekana aliishia form 2 huko Kenya na aliporudi alifanya ujambazi ndo ukamsaidia kupata fedha! Alikuwa analalamikiwa sana kuwadhurumu wananchi ardhi '' akipenda tu eneo lako lazima anakutafuta visa mpaka analipata'''za mwizi arobaini wananchi wa Kisesa walisha mkosa zaidi ya mara 3 lakin alikuwa akiokolewa na polisi! Huyo ndo mwenyekiti mstaaafu wa CCM wa Mwanza
 

MOORIINGEE

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
381
195
mshahara wa dhambi ni mauti............. Hayo ni matokeo ya kilio cha wanyonge: kwa anayemfahanu CLEMENT GREGORY MABINA hawezi kushangaa kilichotokea na kumpata Mabina
 

MOORIINGEE

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
381
195
Nani ka kwambia risasi kwamba inatuliza watu! Km ndo weledi basi hatuna wataalamu. Alianza kuua yeye.

utasikia '' lilikuwa likipambana na polisi tukalishindaaa wapiiii kumbe wananchi walikuwa wanatafuta haki yao iliyopolwa siku nyingi
 

Uledi

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
583
500
Na huko alikoenda afe tena ikiwezekana kwa kupigwa mawe hivyo hivyo
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
54,515
2,000
jamani semeni jambazi,au jangili sugu ameuawa mwanza.

Nilishawahi kuandika hapa kwamba ni aibu CCM kumuweka jambazi anayejulikana kuwa mwenyekiti wao wa chama wa mkoa.

Sasa naona jamaa hakusahau asili yake ya ujambazi, anataka kumaliza kila kitu kwa bunduki.

CCM. Chama Cha Majambazi. Haya ndiyo mauti ya makada wake.
 

Sizinga

JF-Expert Member
Oct 30, 2007
8,563
2,000
Nilishawahi kuandika hapa kwamba ni aibu CCM kumuweka jambazi anayejulikana kuwa mwenyekiti wao wa chama wa mkoa.

Sasa naona jamaa hakusahau asili yake ya ujambazi, anataka kumaliza kila kitu kwa bunduki.

CCM. Chama Cha Majambazi. Haya ndiyo mauti ya makada wake.

Tuwekee hiyo link
 

BHULULU

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
4,902
2,000
Hakuwa na nia ya kuua??!!Alifyatua risasi hewani halafu hiyo risasi ikakata kona ghafla na kuua mtu??!!Polisi wetu huwa wanachekesha sana!!!
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
54,515
2,000
Hakuwa na nia ya kuua??!!Alifyatua risasi hewani halafu hiyo risasi ikakata kona ghafla na kuua mtu??!!Polisi wetu huwa wanachekesha sana!!!

Kwa wanaomjua Mabina na historia yake, ujambazi na kuua hajaanza jana wala juzi.

Hizo nyingine geresha tu.

Za mwizi arobaini.
 

Schsto

Member
Mar 20, 2013
20
20
Afu huyo mtoa taarifa wa polisi anajuaje kuwa dhamira ya MABINA haikuwa kuuwa hali polisi hawakuwepo kwenye eneo la tukio?, kuuwa kwa kudhamiria au kutodhamiria ni siri iliyokuwa moyoni kwa Mabina na kaondoka nayo, so polisi acheni longolongo zenu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom