''Mabilioni ya mu-italiano'', serikali isimjibie muhusika

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
53,662
120,321
Kumekuwa na kasumba ofisi za umma kutumika kujibu kashfa binafsi. Imefanyika hivyo kwa Balozi Sefue, na leo imetokea kwa Bi.Wangwe aliyetenguliwa NSSF. Badala ya wahusika kujitokeza na kujibu kashka serikali imekuwa ikijibu badala yao.Huu sio utaratibu mzuri na inavunja nguvu mapambano dhidi ya majibu. Na hata ikitokea kashfa hiyo imekuwa dhahiri itakuwa ngumu kwa serikali kula matapishi. Sasa tunashauri hilo lisitokee kwa hii kashfa ya MABILIONI YA MUITALIANO. Tayari wahusika wameanza kujitokeza wakiwa katika ''panick mode'' na kushindwa kabisa kujibu kashfa nzito.
 
Kiukweli nakerwa sana na tabia hii ...tuhuma za Mbowe Chadema wanamjibia, Tuhuma za Wangwe ofisi ya umma inatoa tamko wakati ni issue binafsi, hivyo hivyo kwa Ombeni Sefue ....tuwe na mipaka pale inapoibuka issue au tuhuma binafsi .....taasisi kujihusisha na tuhuma binafsi ikitokea tuhuma ikawa kweli mnachafua na taasisi yenyewe ....
 
Tatizo ni kuwa hizo tuhuma "binafsi" zinazigusa hizo ofisi za umma. Kwa hiyo ofisi haiwezi kuacha kuzijibu.
 
Kumekuwa na kasumba ofisi za umma kutumika kujibu kashfa binafsi. Imefanyika hivyo kwa Balozi Sefue, na leo imetokea kwa Bi.Wangwe aliyetenguliwa NSSF. Badala ya wahusika kujitokeza na kujibu kashka serikali imekuwa ikijibu badala yao.Huu sio utaratibu mzuri na inavunja nguvu mapambano dhidi ya majibu. Na hata ikitokea kashfa hiyo imekuwa dhahiri itakuwa ngumu kwa serikali kula matapishi. Sasa tunashauri hilo lisitokee kwa hii kashfa ya MABILIONI YA MUITALIANO. Tayari wahusika wameanza kujitokeza wakiwa katika ''panick mode'' na kushindwa kabisa kujibu kashfa nzito.
Nimelipenda hili angalizo wale 46 wamo humu naamini watafikisha ujumbe kunakohusika
 
Tatizo ni ccm mfumo walioutengeneza kuwa ukiwa ccm wewe uwezi kuguswa yaani ccm family sio wale wenzangu Na Mimi waliombewa Na mwenyekiti wafikiriwe uku yaani wale 46 ndio maana hawa kuwaibia watu kufanya ufisadi kwa mgongo wa chama kwao ni kawaida Na utasikia lolote zaidi serikali kuwasafisha Na haya ni machache tu sasa ccm kuwa mchafu ndio sifa yao Na watahakikisha Na hao wasafi wachache wawe wachafu ili madili yao ya ufisadi yasonge kwa hiyo ata mzee Wa majibu msiye mkamshangaa kabadilika Na kuanza kucheza Ngoma yao ya mafisadi
 
January keshajibu kasema yeye aliomba hela kwa dada yake! Dada yake ndo kachkua huko Mange kaweka insta page yake voice clip
 
Haya yakujibiwa na serikali kwa niaba ya mtuhumiwa hayakuwepo awamu ya NNE, maana tungesikia serikali ikimjibia Mwigulu pale alipofumwa ana kula Mali za kada mwenzie kwenye kampeni.
Sana sana chama ndio kilitoa tamko kuwa hayo ni mambo ya ndani ya chama katika kuonyesha mshikamano
 
January keshajibu kasema yeye aliomba hela kwa dada yake! Dada yake ndo kachkua huko Mange kaweka insta page yake voice clip

Huyo makamba nae angekaaa kimya dada yake ana kazi gani ya kumpatia mzigo mkubwa waache utapeli hii imekaaa vibaya sana kwao
 
Dhambi ya kuonea vidagaa na kambale wadogo ili kupata 'wasikilizaji' wengi. Bado naikumbuka kauli ya Waziri Mkuu ya kuwa watawafukuza watumishi wazembe na wala rushwa , hawatawahamisha. Leo (siku moja baadaye) uovu wa high table mwenzake ukaangazwa kwa media. Sitaki mtu amwombee poo, kwa kuwa wale manesi, daktari, wale wa bandari, ....hawakuombewa poo.
 
Kumekuwa na kasumba ofisi za umma kutumika kujibu kashfa binafsi. Imefanyika hivyo kwa Balozi Sefue, na leo imetokea kwa Bi.Wangwe aliyetenguliwa NSSF. Badala ya wahusika kujitokeza na kujibu kashka serikali imekuwa ikijibu badala yao.Huu sio utaratibu mzuri na inavunja nguvu mapambano dhidi ya majibu. Na hata ikitokea kashfa hiyo imekuwa dhahiri itakuwa ngumu kwa serikali kula matapishi. Sasa tunashauri hilo lisitokee kwa hii kashfa ya MABILIONI YA MUITALIANO. Tayari wahusika wameanza kujitokeza wakiwa katika ''panick mode'' na kushindwa kabisa kujibu kashfa nzito.
wale vijana 46 wanateseka sana ! wanaopiga hela wengine , wanaohangaika wengine !
 
Back
Top Bottom