Hahaha! Mkuu hapa ulifikiri unatumia ID yako nyingine kuunga mkono thread uliyoanzisha mwenyewe kumbe bado uko kwenye ID uliyoanzishia thread! Pole sana kwa kuumbuka.
I say nyie watu hamna aibu kwenye propaganda zenu. Yaani Africa iwe na heshima kwa kutokwenda USA? Ndio mawazo ya Magufuli hayo, kwamba Tanzania itakuwa na heshima ikiwa hatafanya ziara za nje?
Na enzi za Nyerere mbona alikuwa akitoka nje na Tanzania ikawa na heshima sana? Utaelezaje hilo?
Tanzania kuwa na heshima ni kuacha kutumia nguvu kukaa madarakani kwa kukandamiza siasa za upinzani na kuteka na kuua kila anaekukosoa. Na pia ni kuwa na sera za nchi za nje (foreign policy) ambazo zinatuondoa kwenye ulimbukeni wa kuomba omba vitu vidogo kama kujengewa viwanja na misikiti, na kujikomba kwa mataifa kwa ajili ya misaada yao badala ya kusimamia misingi ya haki za binadamu. Ndicho Nyerere alichotuachia mfano ila tatizo ni nyie, vichwa na masikio makubwa lakini hamuelewi wala kusikia.