Mabasi ya wanafunzi ya CRDB yahujumiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabasi ya wanafunzi ya CRDB yahujumiwa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by GeniusBrain, Mar 23, 2012.

 1. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  CRDB: Kwa sasa hatuwezi kuizungumzia Uda

  Na Jimmy Mfuru 23rd March 2012

  Wakati Shirika la Usafiri Dar es salaam (Uda), linasema mradi wa mabasi ya wanafunzi yaliyotolewa na Benki ya CRDB, unajiendesha kwa hasara na kufanya mabasi kusimama kutoa huduma kwa wanafunzi Jijini Dar es salaam, benki hiyo imesema kwa sasa hawawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa wanalifanyia kazi.
  Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kampuni ya Simon Group, Robert Kisena, ambae ni mbia katika Uda, alinukuliwa na NIPASHE kuwa mabasi hayo yanajiendesha kwa hasara na kuishauri benki hiyo ili mabasi hayo yaweze kujiendesha nyakati za mchana yabebe abiria wa kawaida.

  Akizungumza na NIPASHE jana jijini Dar es Salaam, Afisa Uhusiano wa CRDB, Nasibu Kalamba, alisema kwa sasa benki hiyo haiwezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa linafanyiwa kazi.

  "Kwa sasa Benki haiwezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa bado linafanyiwa kazi," alisema Kalamba.
  Benki ya CRDB ilitoa mabasi matano mwaka 2010 ambayo yalizinduliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwa ajili kusaidia kubeba wanafunzi jijini Dar es Salaam ili kupunguza kero, lakini mabasi hayo kwa sasa yamesimama kwa zaidi ya miezi miwili bila kutoa huduma.CHANZO: NIPASHE
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Miradi bubu ya wazalendo
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  huu haukuwa mradi wa kibiashara, ilikuwa ni donation kusaidia wanafunzi wa DSM kwahiyo huo mradi ni liability ya crdb

  kisena asitegemee faida kwenye mabasi ya wanafunzi
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwani mapatano ilikuwa mradui ufanye kwa faida au kutoa msaada wka wanafunzi wanaoteseka kwa shida ya usafiri? Huyu Kisena hiyo habari ya hasara anaitioa wapi wakati lengo la CRDB kutoa mabasi na UDA kukubali kuyapokea na kuyaendesha ilikwua ni kusaidia wanafunzi. Kwa nini UDA isikatae tangu mwanzo kwa kigezo kwua itapata hasara?
   
 5. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Yaani nilikuwa ninajiuliza haya mabasi mbona siyaoni cku hizi..! Nikahisi yale yale ya Mabasi ya wanafunzi ya wakati uleee.. Mradi ambao uliuliwa na baadhi ya Viongozi wa Chama kimoja cha siasa hapa Tanzania..
   
 6. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  hesabu za 150/= zilikuwa hazitoshi
   
 7. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Niseme tu kwamba kwa sasa hakuna mradi wowote wa umma unawezafanikiwa Tanzania chini ya Serikali ya CCM! Viongozi wote walafi na hawajali masilahi ya wananchi!
   
 8. only83

  only83 JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Hii nchi kazi tunayo...tunahitaji maombi mazito.
   
 9. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kama hii serekali ya ccm inashindwa kusimamia kamradi kadogo kihivyo hivi tutafika kweli?

  Na hii simon group ni mnyama gani serekali inashindwa kuwaajibisha?

  Halafu Jk anasema wanamuonea wanasema yeye ni dhaifu.
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  who is simon group?
   
 11. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  TUCK FHEM SIMON Gangstersssss...
   
 12. r

  rimbocho Member

  #12
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu mradi toka mwanzo ulikuwa unaharufu ya hujuma. Hebu tambieni nani aliyewapa ushauri wa kibiashara hawa CRDB wakanunue mabasi aina ya TATA eti ndio yatadumu? Bei yenyewe ilikuwa ni ya kuruka eti basi moja zaidi ya m 100 hi si kweli.
  hawa jamaa hawakuwa serius na uwekezaji huu, hata kama ilikuwa ni kuwasaidia wanafunzi lazima uwe mradi ambao ni sustainable au ulikuwa kwaajili ya mtoto fulani kwa hiyo kesha maliza shule na mabasi kwisha kazi yake?

  CRDB mnajiaibisha tulitegemea mngeweza hata kuwa washauri wa serikali katika uwekezaji kumbe nanyi hope less. Mbona mabasi ya shule za binafsi yanaoperate kila siku?

  Ushauri.

  Kama unataka kupunguza nauli ambayo inamfanya mwanafunzi amudu usafiri basi lazima uwe una revolve fund ya kufidia hilo gepu ili biashara hiyo ya kumsaidia mwanafunzi iwe endelevu
  katika faida ya bank kila mwaka kuwe na fungu la kujazia hiyo deficity katika uendeshaji wa mabasi ya wanafunzi

  kuwe na matembezi ya hisani au dinner party za kuchangia usafiri kwa wanafunzi, si tu kwa Dar mnaweza enda hata katika mikoa yenye tatizo kama hilo.

  wazazi wawafaidika katika hiyo business wawe wachangiaji katika sehemu ya uendeshaji si tu katika nauli hata katika michango ya hiari.

  nawakilisha
   
 13. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Toka awali CRDB walikuwa wana lengo la kujitangaza na sio kusaidia wanafunzi. Ni nani awezaye kuendesha mabasi kwa nauli za sh 150? Tuwe wakweli!
   
 14. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,610
  Trophy Points: 280
  Kunakosekana proposal ya kufanya mradi wa mabasi ya wanafunzi yajiendeshe yenyewe hata uvccm walichemsha nadhani bado hatujapata mchanganuo unaostahiki kutatua tatizo hilo,wengi wana nia ila njia hawana.......
   
Loading...