Mabasi ya SUMRY

Cha Moto

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
945
153
WanaJF,
Kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa mabasi haya yalisimamishwa na SUMATRA kufanya shughuli zake njia ya Dar - Mbeya, sasa na hii ajali ya hili basi jana kugongana na Prado maeneo ya Al Jazeera, Iringa, imekuwaje? Ina maana yameruhusiwa kuendelea na usafirishaji?
Mwenye taarifa anihabarishe, niweke kumbukumbu sawasawa.
 
Mkuu ajali imetokea jana eneo la Mtandika,Sumry iligongana uso kwa uso na Prado ya Dr specialist wa macho hospitali ya rufaa Mbeya, dereva wa basi alikuwa ana "overtake" lori mahala pana kona ndo akakutana na Prado iliyokuwa inatokea mbeya kueleka Dar. Picha hizi hapa chini: Photo 2[1].jpg Photo 3[1].jpg Photo 4[1].jpg

Picha ya katikati ndo prado na dereva(Dr) anaonekana kashazimika akiwa kafunga na mkanda wake. Hizo ndo Sumry
 
Mbona zenyewe hazifungiwi?? Wanafungia Dar Express ambayo haina rekodi kama hii ya Sumry.
 
Gari za wakubwa. Kuna siku mungu atajitukuza itamaliza familia zao. Dr RIP. Mtaalamu wetu wa macho. Poleni wana familia.
 
.QUOTE=mmbangifingi;2802846]Mkuu ajali imetokea jana eneo la Mtandika,Sumry iligongana uso kwa uso na Prado ya Dr specialist wa macho hospitali ya rufaa Mbeya, dereva wa basi alikuwa ana "overtake" lori mahala pana kona ndo akakutana na Prado iliyokuwa inatokea mbeya kueleka Dar. Picha hizi hapa chini:View attachment 41107View attachment 41108View attachment 41109

Picha ya katikati ndo prado na dereva(Dr) anaonekana kashazimika akiwa kafunga na mkanda wake. Hizo ndo Sumry[/QUOTE]

Kufungiwa ndiyo nini? Hao SUMATRA wenyewe njaa tupu,walisema wameifungia Sumry ya kutoka Ars kwenda Mbeya. Wiki moja baadaye nilkutana na Basi ile ile ikiwa na namba zile zile na dereva yuleyule ikielekea Mza kutoka Dar? Je huku ndio kufungiwa kunakomaanishwa na Sumatra?
 
Ndio tatizo letu TZ politics zimeingia hata kwenye mambo ya msingi, Viongozi kutokana na ushiriki wao ktk biashara wameacha kutenda kwa maslahi ya umma bali yao binafsi
 
Kuna haja ya kusususia haya magari. Lazma wananchi tujithamini wenyewe kama SUMATRA wameshindwa.

Sitaki tena kusikia habari za kufungia, ni usanii mtupu. Hawa jamaa wametuona mazuzu. Unalifungia gari safari za dar-Ars wanabadili njia inakuwa dar-mwanza. SUMATRA WAMELALA.

Pumbafu zao, wametufanya wajinga. Hizi damu zinazomwagika leo ni laana kwao na familia zao.

R.I.P dereva na dokta.
 
poleni wafiwa pamoja na wale wote wagonjwa aliokuwa anawaangalia macho yenu
Mungu zilaze roho za marehemu mahali pema peponi.. amina!
 
Hawa jamaa route za songea to dsm na iringa to dsm bado wanapeta tuu!
Sasa unafungia route au unafungia mabasi?samatara mnatutia aibu!
 
WanaJF,
Kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa mabasi haya yalisimamishwa na SUMATRA kufanya shughuli zake njia ya Dar - Mbeya, sasa na hii ajali ya hili basi jana kugongana na Prado maeneo ya Al Jazeera, Iringa, imekuwaje? Ina maana yameruhusiwa kuendelea na usafirishaji?
Mwenye taarifa anihabarishe, niweke kumbukumbu sawasawa.

Nasikia PM wetu ana share kwenye hayo mabasi...
 
Kama SUMATRA wamelala tufanye maandamao tuandike mabango 'SUMRY UNATUUA' 'SUMRY UNATUMALIZA', labda ndiyo mwenyewe atapata message.
 
jamani basi likipata ama kufanya ajali hufungiwa kipindi kesi yake ipo mahakamani, na ikiisha na bima kuchukua nafasi yake katika suala zima la malipo na mengineyo, basi husika hu resume route zake kama kawaida, haina cha mkono wa PM wala nini jamani
 
kampuni ya sumry naweza sema kwa sasa hapa tanzania ndio kampuni ya mabasi yenye ajali nyingi kuliko yoyote ile-
cha ajabu polisi kama vile hawapo-sijui nani kawafumba macho polisi-au hizi basi zina mkono wa mtu?
 
Mkuu ajali imetokea jana eneo la Mtandika,Sumry iligongana uso kwa uso na Prado ya Dr specialist wa macho hospitali ya rufaa Mbeya, dereva wa basi alikuwa ana "overtake" lori mahala pana kona ndo akakutana na Prado iliyokuwa inatokea mbeya kueleka Dar. Picha hizi hapa chini:View attachment 41107View attachment 41108View attachment 41109

Picha ya katikati ndo prado na dereva(Dr) anaonekana kashazimika akiwa kafunga na mkanda wake. Hizo ndo Sumry

RIP Dr.Abbas Kilima ( Eye specialist at Mbeya refferal Hospital)
 
Back
Top Bottom