Wadau, habari za Jumapili? Kuna ugomvi wa mara kwa mara au kila siku, kati ya abiria na wahusika wa baadhi ya mabasi kutoka mikoani kuja Dar kuhusu mabasi hayo kugoma kuingia Stendi Kuu ya Magufuli, Mbezi.
Nimewahi kusikia mara kadhaa, lakini jana Tarehe 27/11/2021 nimeshuhudia mwenyewe abiria wa Basi la Tashiriff lililotoka Tanga saa kumi jioni akipigizana kelele na wahusika wake pale Magomeni Mwembechai akitaka basi hilo liende Mbezi Stendi ya Magufuli kwani halikufanya hivyo na lilipita Bagamoyo mpaka Mwembechai, ndiyo ruti yao.
Sijajua nani mwenye mamlaka ya kutoa kauli hiyo, lakini ukweli ni kwamba, abiria wanapata tabu. Yupo abiria mmoja alisubiriwa na mwenyeji wake Stendi ya Magufuli, basi hakikuingia na breki ya mwisho ilikuwa Shekilango. Mbaya zaidi abiria huyo simu yake ilizima chaji na alitegemea kumwona mwenyeji wake kwa sura maana alishamwambia amepanda basi gani. JF tuungane kukemea sintofahamu hii.