Mabasi ya mikoani yaigomea Serikali kuingia Stendi ya Magufuli

racso kaunda

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
246
500
Wadau, habari za Jumapili? Kuna ugomvi wa mara kwa mara au kila siku, kati ya abiria na wahusika wa baadhi ya mabasi kutoka mikoani kuja Dar kuhusu mabasi hayo kugoma kuingia Stendi Kuu ya Magufuli, Mbezi.

Nimewahi kusikia mara kadhaa, lakini jana Tarehe 27/11/2021 nimeshuhudia mwenyewe abiria wa Basi la Tashiriff lililotoka Tanga saa kumi jioni akipigizana kelele na wahusika wake pale Magomeni Mwembechai akitaka basi hilo liende Mbezi Stendi ya Magufuli kwani halikufanya hivyo na lilipita Bagamoyo mpaka Mwembechai, ndiyo ruti yao.

Sijajua nani mwenye mamlaka ya kutoa kauli hiyo, lakini ukweli ni kwamba, abiria wanapata tabu. Yupo abiria mmoja alisubiriwa na mwenyeji wake Stendi ya Magufuli, basi hakikuingia na breki ya mwisho ilikuwa Shekilango. Mbaya zaidi abiria huyo simu yake ilizima chaji na alitegemea kumwona mwenyeji wake kwa sura maana alishamwambia amepanda basi gani. JF tuungane kukemea sintofahamu hii.
 
mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
3,982
2,000
Karbia mabasi 500 au zaidi kwa siku yanatoka na kuingia hiyo stendi kutokea Mikoani.
Vikampuni vyenye Ofisi binafsi ambavyo havizidi 10 kukaidi amri ya kushusha stendi ya JPM kusilete sintofahamu na kukejeli ukweli kwamba ile Stendi inatumika ipasavyo.
Hata hivyo kuna nguvu kubwa sana inatumika kufuta legacy ya JPM, Endeleeni na kufubaza mazuri yake hakuna anayezuia Uhuru wetu wa kutoa maoni japo lengu limeshajulikana.
 
Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
45,441
2,000
Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuna nini stand ya magufuri,maana huenda kukawa kumependikizwa vimelea fulani vya chuki vs M~gang na kuwafanya hata madereva hao kuichukia standa.
KUNA NINI KWANZA KATIKA STAND HIYO?
Ujenzi haujakamilika, that's all
 
Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
9,170
2,000
Wadau, habari za Jumapili? Kuna ugomvi wa mara kwa mara au kila siku, kati ya abiria na wahusika wa baadhi ya mabasi kutoka mikoani kuja Dar kuhusu mabasi hayo kugoma kuingia Stendi Kuu ya Magufuli, Mbezi.

Nimewahi kusikia mara kadhaa, lakini jana Tarehe 27/11/2021 nimeshuhudia mwenyewe abiria wa Basi la Tashiriff lililotoka Tanga saa kumi jioni akipigizana kelele na wahusika wake pale Magomeni Mwembechai akitaka basi hilo liende Mbezi Stendi ya Magufuli kwani halikufanya hivyo na lilipita Bagamoyo mpaka Mwembechai, ndiyo ruti yao.

Sijajua nani mwenye mamlaka ya kutoa kauli hiyo, lakini ukweli ni kwamba, abiria wanapata tabu. Yupo abiria mmoja alisubiriwa na mwenyeji wake Stendi ya Magufuli, basi hakikuingia na breki ya mwisho ilikuwa Shekilango. Mbaya zaidi abiria huyo simu yake ilizima chaji na alitegemea kumwona mwenyeji wake kwa sura maana alishamwambia amepanda basi gani. JF tuungane kukemea sintofahamu hii.

Ukweli ni kwamba ile stand ipo sehemu mbaya sana!

Hivi unategemea magari yanayotoka huko Kaskazini yanayopita barabara ya Bagamoyo yaje yarudi Mbezi kweli? Yatapitia njia ipi itakayoyarudisha Mbezi Stand kama yatakuwa yamepitia Bagamoyo?

Hakuna gari inayoweza kupitia Bagamoyo ifike mwenge iende Ubungo kisha ianze kuitafuta Mbezi!

Inachotakiwa ni dereva na kondakta amwambie abiria kabla hajapanda gari inapitia Bagamoyo na haitapitia Magufuli stand, hivyo abiria abaki na uamuzi wa kupanda then achague sehemu nyingine safe kwake kushuka au apande gari zinazopita Chalinze!

Tatizo abiria nao ni wabishi, anaambiwa hii gari inapita Bagamoyo na anataka kushuka mbezi anang'ang'ania tu gari ikifika mwisho wa safari anaanza kutukana dereva!

Kingine labda ugeni wa abiria, ambapo wengi wakielezwa wanaelewa!
 
Mwaikibaki

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,127
2,000
Well
Kinachotokea ni kawaida and we all knew itatokea, kwa uwepo wa stand mbezi baadhi ya bus zitaendelea kua na ofisi na stand zao huku karibia na mji.

Ni suala la abiria kujua tu anapanda gari inapitia bagamoyo na itaishia au kupitia mbezi au la! Tutazoea tu
 
Kalunya

JF-Expert Member
Oct 5, 2021
3,479
2,000
Mwenyeji wake amfate shekilango yaani upite bagamoyo then urudi mbezi stand ni usumbufu.Mwenyeji yupo mbezi stand amchukue abiria ampeleke magomeni si bora mwenyeji amfate mgeni shekilango
 
Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
4,325
2,000
Ukweli ni kwamba ile stand ipo sehemu mbaya sana!
Hivi unategemea magari yanayotoka huko Kaskazini yanayopita barabara ya Bagamoyo yaje yarudi Mbezi kweli? Yatapitia njia ipi itakayoyarudisha Mbezi Stand kama yatakuwa yamepitia Bagamoyo?
Hakuna gari inayoweza kupitia Bagamoyo ifike mwenge iende Ubungo kisha ianze kuitafuta Mbezi!
Inachotakiwa ni dereva na kondakta amwambie abiria kabla hajapanda gari inapitia Bagamoyo na haitapitia Magufuli stand, hivyo abiria abaki na uamuzi wa kupanda then achague sehemu nyingine safe kwake kushuka au apande gari zinazopita Chalinze!
Tatizo abiria nao ni wabishi, anaambiwa hii gari inapita Bagamoyo na anataka kushuka mbezi anang'ang'ania tu gari ikifika mwisho wa safari anaanza kutukana dereva!
Kingine labda ugeni wa abiria, ambapo wengi wakielezwa wanaelewa!
Sehemu mbaya dhidi ya nan? Watu walikuwa wanatoka Mtwara bus linafika Ubungo kipindi hicho licha yakuwa na stand zake uko Sudan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
my own

Senior Member
Oct 15, 2018
105
250
Hata ungekuwa wew ni mwenye gari na inapitia bagamoyo then urudi mbezi nadhani abiria angekuwa mwelewa kabla ya yote angepitia chalinze tu ili ashukie hapo mbezi anapopataka

Sent from my FIG-LA1 using JamiiForums mobile app
 
kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,427
2,000
Haiwezi kuwa wait elephant ni haki ya abilia kufikishwa kwenye kituo kikuu cha mabas
Kutoka Tanga kuja dae kuna ruti mbili
Ya bagamoyo ambayo haipiti mbezi stand na kuna ya
kibaha ambayo inapita ....same way na abiria toka moshi na Arusha.
So hao Tashrif wako sahihi huyo abiria angetaka kupita mbezistand angepanda gari za kupitia Kibaha.
 
nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
874
1,000
Mwenye kufahamu umbali toka Tangibovu hadi Mbezi (via Goba) na Mwenge hadi Shekilango (via Sam Najoma) kuna km ngapi?
 
Bujibuji Simba Nyanaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
63,743
2,000
Wadau, habari za Jumapili? Kuna ugomvi wa mara kwa mara au kila siku, kati ya abiria na wahusika wa baadhi ya mabasi kutoka mikoani kuja Dar kuhusu mabasi hayo kugoma kuingia Stendi Kuu ya Magufuli, Mbezi.

Nimewahi kusikia mara kadhaa, lakini jana Tarehe 27/11/2021 nimeshuhudia mwenyewe abiria wa Basi la Tashiriff lililotoka Tanga saa kumi jioni akipigizana kelele na wahusika wake pale Magomeni Mwembechai akitaka basi hilo liende Mbezi Stendi ya Magufuli kwani halikufanya hivyo na lilipita Bagamoyo mpaka Mwembechai, ndiyo ruti yao.

Sijajua nani mwenye mamlaka ya kutoa kauli hiyo, lakini ukweli ni kwamba, abiria wanapata tabu. Yupo abiria mmoja alisubiriwa na mwenyeji wake Stendi ya Magufuli, basi hakikuingia na breki ya mwisho ilikuwa Shekilango. Mbaya zaidi abiria huyo simu yake ilizima chaji na alitegemea kumwona mwenyeji wake kwa sura maana alishamwambia amepanda basi gani. JF tuungane kukemea sintofahamu hii.
Stand hiyo ni ya kilonya sana
 
kelao

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
7,980
2,000
Ukweli ni kwamba ile stand ipo sehemu mbaya sana!
Hivi unategemea magari yanayotoka huko Kaskazini yanayopita barabara ya Bagamoyo yaje yarudi Mbezi kweli? Yatapitia njia ipi itakayoyarudisha Mbezi Stand kama yatakuwa yamepitia Bagamoyo?
Hakuna gari inayoweza kupitia Bagamoyo ifike mwenge iende Ubungo kisha ianze kuitafuta Mbezi!
Inachotakiwa ni dereva na kondakta amwambie abiria kabla hajapanda gari inapitia Bagamoyo na haitapitia Magufuli stand, hivyo abiria abaki na uamuzi wa kupanda then achague sehemu nyingine safe kwake kushuka au apande gari zinazopita Chalinze!
Tatizo abiria nao ni wabishi, anaambiwa hii gari inapita Bagamoyo na anataka kushuka mbezi anang'ang'ania tu gari ikifika mwisho wa safari anaanza kutukana dereva!
Kingine labda ugeni wa abiria, ambapo wengi wakielezwa wanaelewa!
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
43,391
2,000
Kwa mtu mwenye akili timamu anapaswa kujuwa gari zinazopita Bagamoyo haziendi Mbezi Louis fullstop.

Wanaotokea Zambia, Malawi, Congo, Mbeya, Njombe na Morogoro ni lazima gari ipite hapo kituo cha Mbezi.

Kila binadamu amepewa akili, kuzitumia ni hiyari yako, hata mimi ningekuwa ndio mmiliki au dereva gari yangu inayopita Bagamoyo last stop ni Shekilango, hakuna mtu wa kukubali usumbufu hivyo.

Haya mabasi yanayotoka Arusha na Tanga, kampuni moja imetenganisha njia kwa abiria achaguwe anapanda la kupitia chalinze au Bagamoyo.

Thread za kijinga kabisa hizi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom