Mabasi ya Kilimanjaro yafungiwa kutoa huduma

"Na hii siyo mara moja, wamekuwa wakifanya hivi mara nyingi na tumewaonya mara kwa mara na anaona kulipa faini ni kawaida kwake. Sasa sisi lengo letu ni kutaka wafuate sheria na masharti ya leseni, watoe huduma bora na siyo kutoa faini. Na kama anaona kulipa faini ni kawaida kwake sisi hatuwezi kuvumilia, tumetoa maagizo asitoe huduma kuanzia jumatatu mpaka atakapofanya maboresho na kufuata masharti ya leseni yake."
Na hao waliodhurumiwa nauli zao wanapataje haki yao?
 
Kampuni ina miaka mingi, badala iwe mfano wa kuigwa kwa wengine, imekuwa kinyume chake!

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Basi za Kilimanaro Express tangu zikiwa rangi ya kijani ni matatizo hawataki kulipa kodi kila mara yanakamatwa na bosi naye akakamatwa Temeke akasukumwa ndani akaja na mabasi meupe bado matatizo ni yaleyale.
 
Wahuni hao sina hamu nao. Majuzi stendi yao ya Moshi almanusura nizichape nao baada ya kunikatisha ticket ya basi daraja la juu lakini basi lililokuja ni mkweche kabisa namba "A"

Nikajuta kwanini sikukata ESTHER au TILISHO, baadae nikaamua kukata BM baada ya kurejesha nauli.

Labda wanachoweza kwa sasa ni kusafirisha vifurushi tu ila biashara ya kusafirisha abiria imeshawashinda.

Hao ikiwezekana wafungiwe tu moja kwa moja waanze upya
 
Shida hiyo amri imetolewa ili kesho keshokutwa msome mseme LATRA wanafanya kazi..

Kwani rushwa ilifikia kikomo 2023.. iko hivi Kesho asubuhi watakuwa barabarani business as usual..

Tz hatupo serious na lolote.
 
Back
Top Bottom