Serikali iachane na mabasi ya Mchina BRT

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,940
Kuna pesa nyingi za umma na za mikopo zimewekezwa kwenye usafiri wa mwendokasi Dar lakini ubora wa usafiri ni duni sana na unazidi kuwa duni zaidi kutokana na kutokuwepo kwa mabasi ya kutosha kunakosababishwa na kuharibika na kufa kwa mabasi kwa mara kwa mara.

Duniani kote inafahamika kuwa bidhaa za China ni aghali kuliko za Taifa lolote ingawa unaponunua zinaonekana ni za bei nafuu kuliko za Taifa lolote.

Mathalani, gari la Mchina linauzwa dola 45,000 lakini linalofanana na hilo la Mjapani au lililotengenezwa Ulaya, linauzwa dola 90,000. Gari hilo la Mchina quarenteed life expectancy yake ni miaka 3 wakati la Mjapani au Mjerumani ni miaka 12.

Hii ina maana annual ownership cost ya gari la Mchina ni dola 15,000 na lile la Mjapani, Mjerumani au Mbelgiji ni dola 7,500. Hapa umeangalia ununuzi pekee, hujajumuisha matatizo mengine kwa gari hilo la Mchina ikiwemo kukosekana kwa huduma kutokana na kuharibika kwa mara kwa mara, gharama za Kisaikolojia, gharama zinazopunguza uzalishaji kutokana na watu kukaa kwa muda mrefu vituoni, usalama wa watu (ukweli ni kuwa mabasi haya ya Mchina usalama wake huwa ni mdogo kutokana na tekinolojia iliyotumika. Tuombe isitokee ajali, ni kama karatasi). Ubora mdogo wa kiusalama ndiyo sababu ya baadhi ya mataifa kuzuia mabasi ya Mchina kutumika kwenye safari ndefu.

Kwa miradi mikubwa ya Serikali, kama mradi wa mabasi yaendayo kasi, ni vema kila kitu kikawa katika viwango vya ubora unaotakiwa, yaani kuanzia mabasi yanayotumika mpaka mpangilio wa utoaji wa huduma yenyewe.

Ni vema kila njia ikawa na kampuni inayojitegemea, Serikali iwe mwangalizi wa ubora huduma wa kila kampuni itakayokuwa imewekeza kwenye kila njia ili pesa hizi za wananchi na mikopo, ziwe na ubora. Serikali itoe mwongozo wa mabasi yanayotakiwa kutumika kwenye njia hizi, na wawekezaji wenye uwezo wajitokeze. Zinatumika pesa nyingi ili kupunguza msongamano wa mabasi lakini uduni wa huduma huleta matokeo hafifu.

Siku za huko nyuma, ilikuwa inajulikana kuwa Serikali hununua wakati wote vifaa vyenye ubora wa hali ya juu. Dar iliwahi kuwa na mabasi maakum ya usafiri wa mjini, mabasi yale ya Ikarus. Hata kwa mwonekano tu yalikuwa ni mabasi yenye ubora wa hali ya juu. Ikarus ilikuwa kampuni ya Hungary, ilikuwa ndiyo kampuni kubwa na bira kuliko zote za magari kwa nchi za Ulaya Mashariki. Yaani hapo zamani, Serikali wakati wote ilikuwa inatafuta kilicho the best.

Ikarus was a bus manufacturer based in Budapest and Székesfehérvár, Hungary. It was established in 1895 as Imre Uhry's Blacksmith Workshop and Coach Factory and during the Communist era in Hungary it dominated bus markets of the entire Eastern Bloc and its allies. Wikipedia

Leo, Serikali nayo inaangukia kwenye ununuzi wa bidhaa hafifu!
 
Tusubirie wabinafsishe tuone sekta mbinafsi watakuja aina gani
 
Ni nchi chache Africa zinaweza mkwepa mchina , Tanzania itoe kabisa , hata ungekuwa wewe bado huwez wakwepa
 
Mathalani, gari la Mchina linauzwa dola 45,000 lakini linalofanana na hilo la Mjapani au lililotengenezwa Ulaya, linauzwa dola 90,000. Gari hilo la Mchina quarenteed life expectancy yake ni miaka 3 wakati la Mjapani au Mjerumani ni miaka 12.

Hii ina maana annual ownership cost ya gari la Mchina ni dola 15,000 na lile la Mjapani, Mjerumani au Mbelgiji ni dola 7,500. Hapa umeangalia ununuzi pekee, hujajumuisha matatizo mengine kwa gari hilo la Mchina ikiwemo kukosekana kwa huduma kutokana na kuharibika kwa mara kwa mara, gharama za Kisaikolojia, gharama zinazopunguza uzalishaji kutokana na watu kukaa kwa muda mrefu vituoni, usalama wa watu (ukweli ni kuwa mabasi haya ya Mchina usalama wake huwa ni mdogo kutokana na tekinolojia iliyotumika. Tuombe isitokee ajali, ni kama karatasi)...
Naunga mkono hili..

Tatizo ni kuwa mambo mengi ya serikali yanaendeshwa kisiasa, kufurahishana na kujipendekeza. So, chama cha Kikomunisti cha China kikiomba hiyo tenda kupitia ccm kwa niaba ya kampuni yao ya YUTONG, hakuna atakayechomoa!!
 
Acha hizo..😂😂😂
Fifa world cup 2022 Quatar mabasi ya "mchina"yalitumika👇👇👇👇
 
Kuna pesa nyingi za umma na za mikopo zimewekezwa kwenye usafiri wa mwendokasi Dar lakini ubora wa usafiri ni duni sana na unazidi kuwa duni zaidi kutokana na kutokuwepo kwa mabasi ya kutosha kunakosababishwa na kuharibika na kufa kwa mabasi kwa mara kwa mara.

Duniani kote inafahamika kuwa bidhaa za China ni aghali kuliko za Taifa lolote ingawa unaponunua zinaonekana ni za bei nafuu kuliko za Taifa lolote.

Mathalani, gari la Mchina linauzwa dola 45,000 lakini linalofanana na hilo la Mjapani au lililotengenezwa Ulaya, linauzwa dola 90,000. Gari hilo la Mchina quarenteed life expectancy yake ni miaka 3 wakati la Mjapani au Mjerumani ni miaka 12.

Hii ina maana annual ownership cost ya gari la Mchina ni dola 15,000 na lile la Mjapani, Mjerumani au Mbelgiji ni dola 7,500. Hapa umeangalia ununuzi pekee, hujajumuisha matatizo mengine kwa gari hilo la Mchina ikiwemo kukosekana kwa huduma kutokana na kuharibika kwa mara kwa mara, gharama za Kisaikolojia, gharama zinazopunguza uzalishaji kutokana na watu kukaa kwa muda mrefu vituoni, usalama wa watu (ukweli ni kuwa mabasi haya ya Mchina usalama wake huwa ni mdogo kutokana na tekinolojia iliyotumika. Tuombe isitokee ajali, ni kama karatasi). Ubora mdogo wa kiusalama ndiyo sababu ya baadhi ya mataifa kuzuia mabasi ya Mchina kutumika kwenye safari ndefu.

Kwa miradi mikubwa ya Serikali, kama mradi wa mabasi yaendayo kasi, ni vema kila kitu kikawa katika viwango vya ubora unaotakiwa, yaani kuanzia mabasi yanayotumika mpaka mpangilio wa utoaji wa huduma yenyewe.

Ni vema kila njia ikawa na kampuni inayojitegemea, Serikali iwe mwangalizi wa ubora huduma wa kila kampuni itakayokuwa imewekeza kwenye kila njia ili pesa hizi za wananchi na mikopo, ziwe na ubora. Serikali itoe mwongozo wa mabasi yanayotakiwa kutumika kwenye njia hizi, na wawekezaji wenye uwezo wajitokeze. Zinatumika pesa nyingi ili kupunguza msongamano wa mabasi lakini uduni wa huduma huleta matokeo hafifu.

Siku za huko nyuma, ilikuwa inajulikana kuwa Serikali hununua wakati wote vifaa vyenye ubora wa hali ya juu. Dar iliwahi kuwa na mabasi maakum ya usafiri wa mjini, mabasi yale ya Ikarus. Hata kwa mwonekano tu yalikuwa ni mabasi yenye ubora wa hali ya juu. Ikarus ilikuwa kampuni ya Hungary, ilikuwa ndiyo kampuni kubwa na bira kuliko zote za magari kwa nchi za Ulaya Mashariki. Yaani hapo zamani, Serikali wakati wote ilikuwa inatafuta kilicho the best.

Ikarus was a bus manufacturer based in Budapest and Székesfehérvár, Hungary. It was established in 1895 as Imre Uhry's Blacksmith Workshop and Coach Factory and during the Communist era in Hungary it dominated bus markets of the entire Eastern Bloc and its allies. Wikipedia

Leo, Serikali nayo inaangukia kwenye ununuzi wa bidhaa hafifu!
Hizi basi za mwendokasi ngumu sana na zina vigezo vyote..

Tatizo ni sisi hatufuati taratibu nzuri za ubebaji na kiwango cha uzito wa basi lenyewe.

Service pia haifanyiki kwa wakati in short usimamizi ndio mbovu..
Ni ijinga wa wasimamizi wetu ndio unapelekea hizo basi kuonekana hazifai ila ni standard kabisa hizo basi.
 
Achana na hayo mabus njoo kwenye barabara ya BRT inayojengwa mbagala - kariakoo aisee utastaajabu na kiwango chake yaani hii barabara ni kama matope Tu..
Barabara haijaisha kutengenezwa na imeshakufa tayari
 
We izike tu ikingali Hai, shauri yako😀😀😀😀
 
Cha kufanya hapo kila route waweke kampuni (mwekezaji) tofauti ili baada ya muda wafanye evaluation ni yupi aongezewe zabuni na nani afungashiwe virago. Hivyo ndivyo mfumo wa soko huria unavyoendeshwa kwa lengo la kuhakikisha ubora na ufanisi wa huduma.
 
Ni nchi chache Africa zinaweza mkwepa mchina , Tanzania itoe kabisa , hata ungekuwa wewe bado huwez wakwepa
Ni watu kukariri tu, china wameendelea kwa sababu wana bidhaa za kila level ya uchumi. Ukitaka kitu ngumu nzito utapata, same ukitaka maboya version utapata. Sasa huyu mtoa mada kakariri kila kitu cha china feki amesahau Huawei, Apple, Tesla na tech giants nyingine wanamanufacture vitu vyao huko.

Angesema tu tununue mabasi yenye ubora sio kupondea china directly, ile policy yao ya 'made in china' imewasaidia sana kuiteka dunia kwenye hii sector
 
Alowambia mchina anatengeneza vitu feki ni nani?? Mchina anatengeneza bidhaa kutokana na bajeti yako yaani mchina haachi hela ikaenda.
Umekalili huo ndio uwezo wake mchina wa kutengeneza usimtetee
 
Serikali inamiliki barabara(infrastructure) , bus ni za mwekezaji
 
Umekalili huo ndio uwezo wake mchina wa kutengeneza usimtetee

Huijui China vizuri mmekaririshwa kila kitu kutoka china ni feki, mchina vitu feki bei chee anawaletea waafrica coz hamna pesa ya kununua OG. Vitu OG anapeleka ulaya na uarabuni.
 
Back
Top Bottom