Mabasi haya mnayakumbuka?

Write your reply...Umesahau Kiswele DAR SONGEA
 
Kuna lile basi injini ya BEDFORD lile...
 
Mkuu hii widambe wamiliki ni hawa akina widambe wa Ilembula au? Je miaka ya Nyuma walikuwa na magari makubawa maana mi nimewakuta na Coaster kadhaa na walipigwa pigwa mawe kwa wizi sidhani kama hata wana baiskeli
 
Happy nation sauti ya Manka eti nayo historia???? Hii biashara ni sawa na kusomesha mchumba
 
Nimekumbuka miaka hiyo ya1980s mabasi ya mkoa yalikuwa yanapita manzese,niliishi pale kituo kilikuwa manzese msufini,aidha kulikua na mgahawa mmoja uliitwa msumbiji hotel mmiliki alikuwa meneja wa timu ya Simba marehemu Abrahman Hamisi Muchacho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Titico😅
Bunda express,.hivi budget za njombe bado zipo kweli daah!!!
 
Mwinyihijas bus service,Dar mlandizi Ruvu,tajiri alikua anakaa mwananyamala,anatembea kwa mguu na kikapu cha kusukwa kwa ukili,Viatu vyake kandambili,mzaramo wa bagamoyo. 1980-81.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi ni lazima wamiliki wa mabus kwa nje waonekane choka mbaya?? Kuna mmoja namfahamu tajiri wa lindi ana mabus meengi ya dar,lindi na mtwara lakini ajabu kwa kutembea kavaa katambili na kushinda kavaa misuli sio ajabu na ndio kawaida kwake..
 
Umenikumbusha madereva wa Songea Dar enzi hixo Tawaqal unamkuta Giriki, Kiswele unawakuta Yogi, Okalla na Rwambo, Zainabs unamkuta Shida na Special coach unamkuta John Africa na Mapunda......dah ilikuwa ni moto chini!
 
yutong,
Igesa Line, Kwacha, Scandnavia na Comfort Video Coach

Hayo niliyowekea red yalikuwa ndo mabasi yangu ya DAR- Iringa. Hiyo ya kwenye bluu yalikuwa mabasi maarufu sana kati ya Dodoma/Mpwapwa na Dar bila kuwasahau Champion.
Umenikumbusha Mhagama aka baba Omary dereva wa Comfort!
 
Nyota ........Dar to Iringa!
 
Umenikumbusha madereva wa Songea Dar enzi hixo Tawaqal unamkuta Giriki, Kiswele unawakuta Yogi, Okalla na Rwambo, Zainabs unamkuta Shida na Special coach unamkuta John Africa na Mapunda......dah ilikuwa ni moto chini!
Hivi ni dereva gani ambaye ilikuwa kama ni gari mpya inapiga route ya Songea ukiongozana na gari anayo endesha anakata taa za breki.

Ukianza kutoka Njombe kwenda Songea kwenye zile kona na milima unajua jamaa akanyagi breki kumbe taa haziwaki ukijaribu kumfata kwa kasi lazima upige chini barabara ya Njombe Songea ni nyembamba na ina kona na milima mikali.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…