Mabango ya CCM Mjini

Mabango ya CCM Mjini

Wana jamvi ebu nielimisheni kuhusu mabango yalotawala barabarani kwa hapa dar yamejaa mno ya mh magufuli alafu wagombea wengine awapo.

Mabango yanalipiwa, hivyo labda vyama vingine havijalipia na kuweka mabango. Pia inawezekana kuna watu wanayatoa mabango ya vyama vingine usiku!
 
Usikariri mkuu kampeni si lazima vyama vyote vifate mfumo wa kubandika mabango na posters kama wafanyavyo ccm miaka yote, kila chama kina mbinu na mikakati na mtoko wa aina ya kampeni waitakayo yenye tija kwao.
 
Eti Hana sura ya kuweka mabango +!!!+
Eti hauziki!!!!
Hivi anayemjua

Magufuli Nani huko vijijnini????

Hamjajua gharika inayokuja
Acheni USHABIKI

UKAWA 68% cwengine 32%
 
Kwani uliambiwa wanafanya mashindo ya u miss hadi wawe na mvuto?

Its the time of changes
 
Dr. Magufuli aende ikulu.

waigizaji waende kaole.
 
Lowasa picha zenyewe za kuweka kwenye Mabango hana, ndo anazitengenezea Gongolamboto, Tandale, Tandika na kwingineko. Aliisahau hiyo part ya Mabango na matangazo.
watu wanatumia gharama kuubwa kutengeneza hayo mabango nje kwa kitu ambacho kinaweza kutengenezwa hapa nchini halafu wanatuambia watatengeneza ajira kwa asilimia 40? ufinyu wa mawazo huo. bora huyo lowasa ambaye amewapa hiyo kazi vijana watanzania ambao wamenufaika.
 
unaizungumzia dar ipi?? maana mi naishi dar na muda nnao mwingi tu na hayo mabango nimeyaona
 
Magufuli ameinyanyapaa ccm! Mabango yake hayajaandikwa ccm!
CCM ni chafu hata hataki ichafue bango lake!
 
Kwa kawaida tangu zamani nilizoea kuona mabango ya wagombea urais yakimtangaza mgombea na chama chake. Sasa haya ya Mwaka huu naona CCM hawajatangaza kabisa chama, wao wamemtangaza tu Magufuli.

Chunguzeni sana mabango yote, hakuna mahali pana neno chagua CCM. Ina maana CCM imekufa?.
 
Mwaka wa mabadiliko.
Imebidi wabadilike ama sivyo wanajipiga kitanzi
 
Huwezi kuyaelewa kwasababu bado hajaiujua dhamira ya Magufuli
 
Kuna mabango sasa katika kila nguzo ya taa za barabarani katika hii barabara mpya nyembamba ya Morogoro. Hata barabara haijafunguliwa, mabango yamewekwa lukuki. Watuwashie basi taa ili tuweze kuona vizuri usiku?!
 
Kwa kawaida tangu zamani nilizoea kuona mabango ya wagombea urais yakimtangaza mgombea na chama chake. Sasa haya ya Mwaka huu naona ccm hawajatangaza kabisa chama,wao wamemtangaza tu Magufuli. Chunguzeni sana mabango yote, hakuna mahali pana neno chagua ccm. Ina maana ccm imekufa?.
Hujaeewa nini wakati kila kitu kipo wazi?

Wamekwambia hapa kazi tu, maana yake hapa kazi tu ya kuiba na kufanya ufisadi kwa kwenda mbele.

Wakikwambia hapa kazi tu, maana yao nyingine ni kuwa hapa kazi tu ya kufunga magoli ya mikono.

Nadhani hapo utakuwa umenipata.
 
Kuna mabango sasa katika kila nguzo ya taa za barabarani katika hii barabara mpya nyembamba ya Morogoro. Hata barabara haijafunguliwa, mabango yamewekwa lukuki. Watuwashie basi taa ili tuweze kuona vizuri usiku?!

Yana week ya pili sasa
 
Nasikia ccm imebakiwa na watu watano tu. Mkuu wa kaya na marafiki wake wanne tu. Na ndiyo maana hata mangula ameamua kufunga mdomo kabisa. Hasikiki tena. Na kila mwanza cm anasubiri kupiga kura ya chuki.juzi nilicheka sana, kinana mwenyewe sasa hivi ni kama amechanganyikiwa. Juzi nilimsikia akisema ccm imejaa wezi lakini akiingia magufuli ati atawafurusha!
 
Wangebadili na rangi kabisa...
Mwaka huu sisi hatutaki rangi ya kijani
 
Wangebadili na rangi kabisa...
Mwaka huu sisi hatutaki rangi ya kijani
Mkuu hawa watu hakuna rangi wataacha kuona mwaka huu. Halafu mbaya zaidi wale wadhamini wao wahindi mwaka huu wote wameshaondoka to canada, wameacha vumbi tu. Kwa hiyo hali Yao kiuchumi ni mbaya sana. Trip hii najua NSSF watakoma. Hakuna na Daraja la kigamboni wala cha nini yaani wako tee kabisa. Kweli Siku ya kufa nyani ...............
 
Back
Top Bottom