Mabalozi wa kigeni wanaohudhuria kesi ya Mbowe waonywa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,832
218,511
Hii ndio Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, Mulamula, ambaye amewataka mabalozi hao kufuata sheria na taratibu za kidiplomasia , hakufafanua taratibu hizo kama zinawakataza mabalozi kuhudhuria kesi mahakamani au la.

========

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amewataka mabalozi wanaokwenda mahakamani kufuatilia mwenendo ya kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kufuata sheria na taratibu za kidiplomasia.

Balozi Mulamula ameyasema hayo leo Agosti 20,2021 jijini Dar es Salaama wakati akizungumza na mabalozi, wakuu wa taasisi na mashirika ya kimataifa mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Lilongwe, Malawi Agosti 17–18.

Katika mkutano huo, Balozi Mulamula amesisitiza kwamba mabalozi wanaokwenda mahakamani kufuatilia mwenendo wa kesi ya Mbowe kufuata sheria na taratibu za kimataifa za kidiplomasia ili kujiepusha na ukiukwaji wa sheria na taratibu hizo.

Chanzo: Mwananchi
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amewataka mabalozi wanaokwenda mahakamani kufuatilia mwenendo ya kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kufuata sheria na taratibu za kidiplomasia.

Balozi Mulamula ameyasema hayo leo Agosti 20,2021 jijini Dar es Salaama wakati akizungumza na mabalozi, wakuu wa taasisi na mashirika ya kimataifa mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) uliofanyika Lilongwe, Malawi Agosti 17–18.

#MwananchiUpdates
 
2865442_JamiiForums1550718452.jpg
 
Siasa za Tanzania sontimes zinafurahisha: Ccm chadema na genge hutokea makundi mawili yanaungana dhidi ya kundi moja.

Kuna kipindi chadema wanaungana na genge dhidi ya ccm.- Tozo

Kuna kipindi ccm inaungana na chadema dhidi ya genge.- Chanjo.

Kuna kipindi ccm inaungana na genge dhidi ya chadema- Kesi ya ugaidi.

Hii ndo raha ya kuwa mtanzania.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Hawana ubavu huo, hususani ukizingatia kesi ya Mbowe inahudhuriwa na mabalozi huru kutoka kwenye nchi za wenye akili timamu. Balozi wa nchi kama Burundi huwezi kumuona mahakamani kamwe.
Halafu ndio eti ndio wanakuaga waangalizi wetu wa uchaguzi mkuu
Hao wenye akili hua hawaalikwi kua waangalizi
Yaani hua wanachagua maboya kuja kutuangalizia uchaguzi
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amewataka mabalozi wanaokwenda mahakamani kufuatilia mwenendo ya kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kufuata sheria na taratibu za kidiplomasia.
Balozi Mulamula ameyasema hayo leo Agosti 20,2021 jijini Dar es Salaama wakati akizungumza na mabalozi, wakuu wa taasisi na mashirika ya kimataifa mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) uliofanyika Lilongwe, Malawi Agosti 17–18.
Katika mkutano huo, Balozi Mulamula amesisitiza kwamba mabalozi wanaokwenda mahakamani kufuatilia mwenendo wa kesi ya Mbowe kufuata sheria na taratibu za kimataifa za kidiplomasia ili kujiepusha na ukiukwaji wa sheria na taratibu hizo.
#MwananchiUpdates
Waziri Mulamula tulitarajia jna uweledi fulani na ukaheshimika sana ila kwa hili agizo siamini. Ila yawezekana kabisa umeagizwa kutoa kauli hii tata! Na kumbuka nadhani unayo safari ya Amerika karibuni.
WaTanzania mlioko huko USA hamna hata haja ya kuwa na maongezi naye kwani ashaunga juhudi imekuwa shida kuanza kutoa matamko yasiyo mshiko.
 
Kesi zote ziko hurru kwa kila mtu na open court why waonywe ??? Hakuna kuonywa wala hawaogopiii
Hii ndio Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Africa Mashariki , Mtukufu Mulamula , ambaye amewataka mabalozi hao kufuata sheria na taratibu za kidiplomasia , hakufafanua taratibu hizo kama zinawakataza mabalozi kuhudhuria kesi mahakamani au la .

View attachment 1900584

Chanzo : Mwananchi
Maskini hana uwezo wa kumuonya tajiri anayemlisha
 
Hii ndio Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Africa Mashariki , Mtukufu Mulamula , ambaye amewataka mabalozi hao kufuata sheria na taratibu za kidiplomasia , hakufafanua taratibu hizo kama zinawakataza mabalozi kuhudhuria kesi mahakamani au la .

View attachment 1900584

Chanzo : Mwananchi
Bora angenyamaza, ameharibu sana sawa na kujamba saa ya meza ya Bwana palipo na utulivu...kila mtu atasikia
 
Back
Top Bottom