Mabadiliko ya ufanyaji kazi wa ubongo kwa watu wazima (dementia)

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,273
Ni matatizo ya kawaida na huwapata watu kuanzia umri wa miaka 45 lakini wengi husumbuliwa zaidi katika miaka ya 80. Mtu ambae hupata matatizo haya tabia zake hubadilika;
- hutafuta maneno wakati wa kuongea.
- shida ya kumbu kumbu za karibu lakini hukumbuka matukio ya miaka mingi iliyo pita
-kukosea maneno,
- shida ya kutambua vitu au watu wa karibu
-uwezo wa kufanya mambo ya kawaida kama kuoga na kuvaa hupungua.

Ziko aina nyingi za dementia

1. Alzheimer’s ambayo huwapata watu wengi, husababisha na mkusanyiko wa beta amyloid protein kwenye ubongo. Hii huwapata 65+ na matokeo yake huwa ni kusahau watu wa karibu na vitu.
Anaweza kusahau watoto wake au kusahau matumizi ya vitu vya kawaida kama sahani na kijiko.

2. Vascular dementia
Hii husababishwa na ubongo kukosa hewa hasa katika ajali ya stroke. Matokeo yake mgonjwa kupata msongo wa mawazo (depression) mabadiliko ya mood na shida ya kuongea maneno yanayoeleweka.

3. Dementia with Lewy bodies (ALB)
Husababishwa na mkusanyiko wa protein Lewy bodies kwenye ubongo ambao husababisha uharibifu kwenye chembe hai za mawasilianao. Athari zake ni sawa na watu wenye Parkinson disease au Alzheimer’s. Wagonjwa huona vitu ambavyo wengine hawa hawavioni (hallucination).

4. Parkinson dementia
Dalili zake ni sawa na Lewy bodies lakini wagonjwa wa Parkinson dementia pia huwa na matatizo ya mwendo.

5. Front temporal dementia
Hii huwapata watu wa umri wa 65+ kutokana na sababu mbali mbali sehemu ya mbele ya ubongo hupoteza uwezo wa kufanya kazi sawa sawa. Matokeo yake wagonjwa hupoteza uwezo wa kujua madhara ya matendo yao kwa watu wengine.

6. Alcohol related dementia
Hii huwapata watu waliokunywa pombe kwa muda mrefu, umri unavyozidi kusogea madhara ya pombe kwenye ubongo huwa ni kupoteza kabisa uwezo wa kufikiri na pia hupata shida ya kumalizia sentensi wakati wa kuongea.

Dementia haina dawa lakini huweza kuwa controlled na wataalamu wa magonjwa ya ubongo.
 
Sky Eclat uko vizuri .maada kama hii utapata likes chache na michango michache sana maana wengi humu tumo cheap minds , mapenzi na muziki kwenda mbele , ELIMU ahangaike nayo mabeberu kisha aje atutawae kiuchuimi ni kiutamaduni. MTU atakupangia kikosi chote cha Arsenal utadhani mzungu Wa uingereza . watanzania tubadilike . Alzheimer huua baada ya miaka isiyozidi 12 baada ya dalili kujitokeza. Ndio ulimuua Reagan rais Wa Marekani miaka ya 80's lakini hata hivyo aishaula si haba. Maana hata angepata MTU Wa kumtunza hatua ya mwisho mgonjwa hukataa kula. Mwafrika akiugua tunaamini karogwa tu. Tusome nondo za hizi.
 
Nasikia dementia ndio sababu ma pilots wanapunguziwa credits za kurusha ndege kulingana na umri unavyoongezeka ni kweli?
Rubani mwenye umri mdogo ana credits nyingi kuliko anavyozidi kuzeeka?
 
Back
Top Bottom