Mabadiliko ya Tarehe Ajira za Walimu

Mabadiliko ya Tarehe Ajira za Walimu

tusitegemee sana kwa jirani jaribu kuumiza kichwa kwa kutumia elimu yako uliyoipata katika kujenga mwanzo wa maisha utafanikiwa adi kuajiliwa utakuwa utaki tena kutokana na mafanikio utakayo pata
Unapoongeas neno kujiajiri ni lazima ufikirie mara nyingi sana. kwa mfano mimi ni mwalimu wa history na kiswahili, nitajiajiri katika lipi? ukisema biashara je, nimesomea biashara? Tofauti yangu na yule hajasoma katika biashara itakuwa ni ipi?
 
kila kimebadiliaka maana watanzania wengi tulilia mabadiliko sasa nafikri tutulie haya ndo mabadiliko, hata nafasi za kujiunga n JKT zilikuwa zinatoka mwezi wa kumi mbili lakini mwaka huu mpaka mwezi ya kwanza mwakani
 
Hakuna kitu knachouma kama mtu kutoifanyia kaz taaluma yake na kwenda kufanya kaz kwa kitu ambacho hajakibobea. Mie huwa najihs hatia kubwa sana.
Ni kweli kabisa. Tena ukikaa mtaani muda mrefu sana hata ikatokea tuliowaacha wamehitimu sisi hatutakuwa considered tena maana wanadai kwamba ujuzi wa mwalimu hupungua kulingana na anavyokaa muda mrefu bila kufundisha
 
Unapoongeas neno kujiajiri ni lazima ufikirie mara nyingi sana. kwa mfano mimi ni mwalimu wa history na kiswahili, nitajiajiri katika lipi? ukisema biashara je, nimesomea biashara? Tofauti yangu na yule hajasoma katika biashara itakuwa ni ipi?
Umeuliza swali la msingi sana mkuu. Hii dhana ya kujiajiri itafsiriwe upya na sera zihusuzo ajira na vijana zibadilike. Wanasema vijana wahitimu wa ngazi mbali mbali za elimu wajiajiri, ni jambo jema. Lakini iweje ulazimishe mhitimu wa Sociology au BA History ajiajiri kwenye kilimo au ujasiriamali. Inavyoonekana kuna program nyingi sana zinazotolewa na vyuo kwa ngazi mbalimbali hazihitajiki sana kwa fursa zilizopo. Katika hali hii kuna haja gani ya serikali kuendelea kuwekeza mamilioni kuzalisha wasomi katika hizo taaluma ilhali hawahitajiki kwa kiasi hicho wanachozalishwa (Siasa za kipuuzi).
Ingekuwa vyema serikali ingeelekeza nguvu zake kufundisha vijana jinsi ya kuzitumia fursa zilizopo kwa manufaa yao na taifa ipunguze tatizo la ajira. Kwani ni lazima mtu apate shahada ya uongozi na siasa ndio ajifunze ujasiriamali? Wanasema tu fursa zipo wakati ajira zote wanapata watoto wao, kwanini hizo fursa wasioneshe watoto wao kwanza?
 
Kwa kawaida Ajira za Walimu zilikuwa zikitoka January na Walimu walikuwa wakiwasili vituoni walipopangiwa mapema Mwezi wa Pili, lakini kwa miaka takriban mitatu iliyopita kuna Mwezi mmoja mmoja unasogezwa mbele juu ya Ajira za Walimu! Mathalan; Walimu wapya walienda vituoni kama ifuatavyo:-
2012 reporting ilikuwa February (kama kawaida) ila kuanzia:
2013 reporting ilikuwa March
2014 reprting ilikuwa April
2015 reporting imekuwa May
Mwenye taarifa sahihi juu ya Mabadiliko haya naomba tuelimishane. Maana mimi sielewi ni nini hapo!


Labda ujiajiri kuokota makopo na vyuma chakavu.
 
Ajira 40000 zipo njiani, gazeti la nipashe lina taarifa, ukurasa wa pili.
 
wataanza kuajiri walimu wa masomo ya sayansi, walimu wa masomo ya arts wametosha maana wamegundua wengi wao wana vipidi 4 hadi 6 kwa wiki badala ya vipindi 30
 
wataanza kuajiri walimu wa masomo ya sayansi, walimu wa masomo ya arts wametosha maana wamegundua wengi wao wana vipidi 4 hadi 6 kwa wiki badala ya vipindi 30
ajira wanatoa lini ndugu?
 
Ajira zipo but mpaka July na wataajiri walimu wote wenye sifa stahiki
 
Back
Top Bottom