Mabadiliko ya maana ya familia

Mabadiliko ya maana ya familia

Ofcourse najadili kwa muktadha ambao mume ni mwaminifu na mwenye upendo lakini mke anaona huo upendo kama ni ujinga ( kajipatia zezeta).
Ndiyo msitulaumu sababu wanaume wenyewe mnajitapa humu mitandaoni kuwa hakuna mwanaume wa mwanamke mmoja wote mnachepuka sasa hapo hamuoni kuwa ninyi wenyewe ndo mnatuandaa sisi kisaikolojia kudhani kuwa hatuna wanaume waaminifu na wenye mapenzi ya kweli kwahiyo na sisi hatutakiwi kuwatii wala kuwaheshimu?
 
Upo sahihi, lakini ni vyema turudi kwenye misingi ya bibi zetu tuige baadhi ya mbinu na tabia walizokuwa nazo kwa waume zao,, kasumba inayotuyumbisha ni kusema kwamba itikadi za kizamani haziwezi kufanya kazi nyakati hizi(zipo zisizofanya kazi kweli lakini ni chache)
Mwanaume anahitaji heshima, ukimtii na akakutupa basi chozi lako ni juu yake

Tamaduni tunaziacha kando kwa kuziona zimepitwa na wakati, ilhali kimaumbile tuko vile vile kama wa zamani
We bidada comment zako nimezielewa
Umeolewa lakin? Kama hauna tuje kutoa posa
 
we umeolewa?
No kweli, ila wanawake majukumu yamewaelemea sana ,wanaume wamekuwa 'wanauma'. Siku hizi impact ya mwanaume katika familia ni zero kwa maneno mengine ukiolewa na mwanaume anayejitambua umebahatika mengi yamebaki magalasa..
 
Ustawi wa jamii yeyote huanzia kwa kuimarisha maadili ya mwanamke...na ukitaka kujua jamii iliyoparaganyika angalia mwenendo na tabia za wanawake wa jamii husika...kwa mfano maadili na mwenendo wa wamama wa jamii za wachaga ni kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha familia,hasa watoto wanalelewa hivyo...wakati wanawake wa jamii za pwani..kama tanga au lindi...wao ni kinyume kabisa...na maadili au maendeleo ya vizazi vya jamii hizi mbili yako tofauti kama usiku ma mchana..
 
"Enyi wanawake watiini wanaume zenu,na wanaume wapendeni wake zenu"

Ukiingalia huo ujumbe utaona upungufu wa kila mtu,,,kiasili wanawake hawana utii kwa waume zao hivyo ni ngumu mwanaume kupenda,,na wanaume pia wamekosa upendo kwa wake zao sababu kubwa ni kukosekana utii
Hongera...kwa ujumbe mzuri Sana....hi kitu ilizifanya ndoa za zamani kuwa imara
 
Ukiwa mtii (submissive) unapendeka kirahisi na unampa raha anayekupenda. Tatizo ni kwamba wanawake wengi wa leo hususani wasomi wanaishi kwenye ndoa kama wanaharakati na ni wabinafsi mno
Asante kwa ujumbe.. kiukweli wengi wanawake wa Sasa wana dharau na viburi...na hakuna mwanaume ataonyesha upendo kwa mwanamke mwenye tabia hizo....
 
Mkuu kwani kuna mahali nimesema watoto ni laana? Kila kilicholetwa na Mungu ni chema machoni mwa Mungu..punguza jasba!
Unaonekana umepaniki mkuu baada ya kujichunguza na kujikuta huna sifa za kuitwa mwanaume, mleta mada nimemuelewa na mimi nikachangia sababu ambazo zinamfanya huyo unayemuita single mother asiolewe. Na labda nikuambie tu ingawa simo kwenye kundi la hao single mother haijawah tokea siku nikawasema vibaya kwa sababu watoto ni mibaraka.
 
Sky Eclat;
Siku hizi naona umeamua kuwapa za uso wanawake wenzako. Huyo Singel maza mwenye watoto 4 wote from diferent dady, ameamua kuwa shamba la majaribio au?? Mtoto wa kwanza, babake ukamuona galasa, mutoto ya 2 baba naye galasa. Mutoto ya 3 baba galasa hadi mutoto ya 4. baba galasa. Sasa najiuliza, hapo galasa ni weye au hao wanaume?? Una gubu gani wewe woote hao wakukimbie?? Na hao ni wale sperm donors tu zilizofikia utu. Je wale ambao damu hazikilingana??
Hata kwa dawa huyo huniambii ni singel maza. Ni shamba darasa huyo. Hivyo anaharibu maana ya familia huyo.
 
Ustawi wa jamii yeyote huanzia kwa kuimarisha maadili ya mwanamke...na ukitaka kujua jamii iliyoparaganyika angalia mwenendo na tabia za wanawake wa jamii husika...kwa mfano maadili na mwenendo wa wamama wa jamii za wachaga ni kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha familia,hasa watoto wanalelewa hivyo...wakati wanawake wa jamii za pwani..kama tanga au lindi...wao ni kinyume kabisa...na maadili au maendeleo ya vizazi vya jamii hizi mbili yako tofauti kama usiku ma mchana..
Nimekuelewa mkuu lakini kumbuka Pwani dini za Waarabu ziliingia siku nyingi. Kwa malezi ya dini mtoto ni lazima amjue Mungu, Skye sala, aijue dini.

Ukiona mwanamke anaeijua dini hatakuwa nje ya mstari wa maadili.
 
Ndiyo msitulaumu sababu wanaume wenyewe mnajitapa humu mitandaoni kuwa hakuna mwanaume wa mwanamke mmoja wote mnachepuka sasa hapo hamuoni kuwa ninyi wenyewe ndo mnatuandaa sisi kisaikolojia kudhani kuwa hatuna wanaume waaminifu na wenye mapenzi ya kweli kwahiyo na sisi hatutakiwi kuwatii wala kuwaheshimu?

Two wrongs will make nothing right. Unaweza kusikia mengi kuhusu mume au wanaume tena wakati mwingine utasikia hayo kutoka kwa mtu unayemwamini kama mama, dada au Shangazi zako na watakupa na shuhuda hai na ushauri wa kujikinga nasi lakini hayo hayapaswi kuongoza fikra zako. Ukianza kuonyesha dharau utasababisha atafute heshima kwa sababu mioyoni mwetu wanaume kuna nafasi wazi ambayo hujazwa kwa utii (heshima) kutoka kwa mke. Akiitafuta na kuipata nje uwepo wako maishani mwake unakosa maana (the relationship/marriage becomes illogical).
 
hujawahi niangusha kwa points zako.
Mnajua kwanini wanaume siku hizi wanachepuka au hata kukimbia familia?
wanawake wa siku hizi wengi wao ni wababe, hawana utii na midomo mirefu.
Mambo haya mwanaume huyaogopa na kuyachukia, wanawake wengi wanaokula mema ya nchi ni wale watiifu kwa waume zao.
Mke anayenitii ataishi kama malkia, nitamtunza kwa nguvu, moyo na chochote atakacho atapata kwa kadiri ya uwezo wangu
Tukumbuke wanawake wa zamani waliwatii sana waume zao

Kila jinsia isimamie majukumu yake
 
niondoe kwenye kundi lako mkuu
Napinga sana wanaosema wanaume wa zamani walikuwa hardworking. Wanaume wamekuwa wavivu miaka yote(jamii nyingi). Walichojua ni kuzaa watoto wengi ili tu wale watoto wakalime na kuleta mazao mengi. Mama zetu zamani walilima sana, huku wazee wakizurura tu au kufanya kazi kivivu.

Wanaume tumekuwa na tabia za simba dume, tunasubiri wake zetu walime then sisi tule vikiwa tayari.
 
Tutajitahidi kubadilika

Inatakiwa tushushe silaha chini kila jinsia na nadhani wa kwanza kushusha ni mwanamke maana ye ndiye anayeumia kutokana na haya mabadiliko
hujawahi niangusha kwa points zako.
Mnajua kwanini wanaume siku hizi wanachepuka au hata kukimbia familia?
wanawake wa siku hizi wengi wao ni wababe, hawana utii na midomo mirefu.
Mambo haya mwanaume huyaogopa na kuyachukia, wanawake wengi wanaokula mema ya nchi ni wale watiifu kwa waume zao.
Mke anayenitii ataishi kama malkia, nitamtunza kwa nguvu, moyo na chochote atakacho atapata kwa kadiri ya uwezo wangu
 
Naomba hilo andiko tafadhali!
Waefeso 5:22 hadi 25

22 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.

23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.

24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.

25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
 
Wanawake wenyewe wajeuri Sana siku hizi.
Ni afadhali uishi mwenyewe uwe unanunua tu huduma kuliko kuishi na mtu anakuletea stress tu kila siku.
 
Nakazia hapo kwenye mstari wa 24 wanawake tuwatii waume zetu kama kanisa linavyomtii kristo sasa jiulize makanisa ya siku hizi yanamtii kristo au wewe tu hapo ulipo unamtii kristo kama ambavyo unataka mke wako akutii?

Back
Top Bottom